The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 837
Waziri wa Ulinzi wa Israel ameionya Iran leo Jumamosi kuwa mji wake mkuu Tehran "utawaka moto" iwapo itaendelea kuvurumisha makombora ya masafa kuelekea Israel.https://p.dw.com/p/4vu3p
SiasaMashariki ya Kati
Katz: Tehran itawaka moto makombora ya Iran yakiendelea
Iddi Ssessanga | Rashid Chilumba
Saa 3 zilizopitaSaa 3 zilizopita
Waziri wa Ulinzi wa Israel ameionya Iran leo Jumamosi kuwa mji wake mkuu Tehran "utawaka moto" iwapo itaendelea kuvurumisha makombora kuelekea Tel aviv
Waziri Israel Katz ameyatoa matamshi hayo baada ya kufanya tathmini ya uharibifu uliofanywa na mashambulizi ya makombora ya masafa yaliyofyetuliwa na Iran usiku wa Ijumaa na Jumamosi alfajiri kujibu hujuma nzito za Israel dhidi ya miundombinu yake ya nyuklia na vituo vya kijeshi.
Mashambulizi hayo yamewaua watu wasiopungua watatu nchini Israel na kuharibu majengo ya maakazi kwenye miji kadhaa husasani mji mkuu Tel Aviv. Katz amesema Iran italipa gharama kubwa kwa kuwadhuru raia wa Israel.
Amemnyooshea kidole cha lawama Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ambaye aliapa jana Ijumaa kuwa Iran itajibu vikali mashambulizi ya Israel kwenye ardhi yake.
"Dikteta wa Iran anawaingiza hatarini raia wa Iran na kufungua mlango wa jambo ambalo -- hususani wakaazi wa Tehran -- watalipia gharama kubwa kwa sababu ya uhalifu unaotendwa dhidi ya raia wa Israel," amesema Katz katika taarifa iliyonukuliwa na mashirika ya habari ya kimataifa.
"Iwapo (Ayatollah Ali) Khamenei ataendelea kufyetua makombora kuyalenga maeneo muhimu ya Israel -- Tehran itawaka moto."
Afisa wa Iran asema nchi hiyo ilihamisha vifaa vyake vya nyuklia kituo cha Fordo
Katika hatua nyingine Israel imeendelea kufanya mashambulizi ndani ya Iran huku ripoti za hivi karibuni zikisema ndege zake za kivita zimekilenga kituo cha kusafisha mafuta cha Iran cha Tabriz.
Mikanda ya video imeonesha wingu zito la moshi limetanda kwenye kituo hicho. Mashambulizi hayo ni mwendelezo wa hujuma za Israel ndani ya Iran zilizoanza siku ya Ijumaa. Wakati huo huo afisa mmoja wa Iran amesema nchi hiyo ilihamisha vifaa vyake muhimu na vya kimkakati kutoka kwenye kituo chake cha nyuklia cha Fordo kabla ya Israel kukishambulia.
Afisa huyo Behrus Kamalwandi ambaye ni msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran amesema uharibifu uliotokea nje ya kituo hicho hauna athari kubwa na unaweza kushughulikiwa.
Akinukuliwa na Shirika la Habari la Iran, IRNA, Kamalwanfi amesema sehemu kubwa ya vifaa na malighafi muhimu vilihamishwa kwenda eneo salama.
Kituo cha nyuklia cha Fordo kinajumisha mitambo ya kurutubisha madini ya urani na kikakutikana kiasi kilometa 100 kutoka mji mkuu wa Iran, Tehran.
Kituo hicho kimejengwa chini kabisa ya mlima mkubwa na kinalindwa na mizinga ya kijeshi.
Iran yajibu mapigo dhidi ya Israel usiku wa Ijumaa
Mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na Israel dhidi ya Iranna mashambulizi ya kulipa kisasi kutoka Tehran yamesababisha vifo vya mamia, uharibifu mkubwa, na kutishia kulipuka kwa vita kamili Mashariki ya Kati.
Israel ilitumia ndege za kivita pamoja na droni zilizosafirishwa kwa siri hadi ndani ya Iran kushambulia maeneo nyeti na kuua majenerali na wanasayansi wa juu wa kijeshi.
Israel ilisema mashambulizi hayo yalikuwa ya lazima kabla Iran haijafikia hatua ya kutengeneza silaha ya nyuklia, ingawa Marekani na wataalamu wa kimataifa walikuwa wamekadiria kuwa Tehran haikuwa ikifanyia kazi silaha hiyo kwa wakati huo.
Haya yalijiri siku chache kabla ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia, na sasa yameingia katika hali ya sintofahamu.