Katuni ya wiki katika siasa: Hakika imebeba ujumbe mzito

Katuni ya wiki katika siasa: Hakika imebeba ujumbe mzito

manizzle

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2015
Posts
3,421
Reaction score
4,324
10421203_10153318771192482_661480468602427064_n.jpg

Una maoni gani juu ya picha hii? Unadhani nini kitatokea? Chambua kadiri ya uwezo wako, sema lolote unalojisikia kwa sababu hakuna jibu lililo sahihi la moja kwa moja.

Karibuni
 
nashauri hiyo iwe part 1 jina litakapo katwa iltolewe katuni nyingineitakayo onesha jinsi atakavyo kuwa anaporomoka baada ya hiyo kamba kukatika ndorooooobo...
 
Umbali wa kuelekea ardhini ni mfupi
 
Steringi hauawi,na akiuawa ndo mwisho wa sinema/onyesho.
Maadam huyu mtu vaa jezi ya timu flani,
Ni jukumu lao kuomba kamba isikatike
ikikatika mwenye huzuni sio steringi ni waangaliaji
wa picha na wanufaikaji na kuendelea kuonyeshwa
kwa hiyo sinema eg.wauzaji wa vinywaji,sinema ikiisha
mapema biashara yao inadoda.

Hicho kitambi kwenye hiyo katuni kimebeba wengi
kamba ikikatika huenda timu anayoichezea steringi
ikapotea kabisa kwenye ulingo wa viwanja vya siasa
hapa nchini,ila yy atakuwa salama itategemea kaangukia nini.

Ipo michezo ya kichina ya kuvuka kamba
chini yanawekwa magodoro,mchezaji akianguka
haumii ila timu yake inakosa maksi na ushindi.

Nimalizie kwa kusema,hakuna mtu
wa kuiokoa timu ya jezi iliyovaliwa na
katuni kama mwenye sura ya kichwa cha katuni ataanguka.
 
hiyo inaonyesha kamba ikikatika wengi wataumia ila inaweza ikanyoka wengi watafurahi
 
Hii kamba inayumba, haijakazwa sawasawa, na inakatika wakati usiojulikana na imeshikiliwa na INVISIBLES. Invisibles( supporters) wa ENL hawaonekani/hawajulikani na wamemwacha akatize juu ya kamba hataree huku wakiwa waaangalia kwa mbali.
 
Back
Top Bottom