Katuni ya Gado yamchana chana Samia na CCM yake

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Hii katuni ya Gado ni shughuli nzito. Picha ya Rais Samia imetupwa kwenye jalala na nafasi ya picha yake imetwaliwa na Mtawala wa Dubai.

Polisi pia hawakuachwa nyuma nao wamewekwa mfukoni mwa mwarabu huku wanasheria wakijaribu kujenga khoja bila mafanikio.

Kama hawajaielewa hii katuni basi wajiandae kuwakabidhi wapinzani Ikulu maana kazi si tu imewashinda bali pia hata HAWAIJUI ya kuwapeleka watanganyika Kaanani.

PSX_20230730_102407.jpg
 
Babu ambacho hukutarajia vijana wa siku hizi wanajivunia kuwa CHAWA wa mama na huko uliko watabiria hawana nia au uwezo wa kupafikia.

IMG-20230730-WA0005.jpg
 
Gado ni mtanzania kwa msiomjua ni mtoto wa ostabey long time, kenya alienda kikazi tu ni mtoto wa mjini kwa waliozaliwa mkoani hawawezi kumfahamu, ameruka mbanga zote za kino hadi temeke, ndio maana hua anahisia sana na mambo ya nchi yake mambo ya kenya hayamuhusu sana
Tunamjua Sana tu
 
Na kubwa kuliko yote tumejisalimisha uhuru wetu wa kujitawala kwa waarabu eti wana tekinolojia na mtaji!

Tangia lini mwarabu alikuwa na tekinolojia? Sana sana ana tekinolojia ya kununua na hata sisi tunaweza kuinunua

Tangia lini mwarabu alikuwa na mtaji wa kutuzidi?

Nchi hii ni tajiri kupindukia tatizo letu ni tuna laana ya viongozi vibogoyo hatuna tatizo jingine
 
Back
Top Bottom