Katu usicheze na hisia za mtu

Katu usicheze na hisia za mtu

Ukiachana na hela, one should always wish for TRUE LOVE that you yourself can love back the same.

The bond u make wit ur soul mate / true love unlocks many success doors u have never imagined one day will ever manifest in ur life.

Mtu ambaye unaenda mzigoni asubuhi unarudi nyumbani huna hata 100 still anakuambia usijali kesho ukikosa utapata kesho kutwa. Unaanzaje kumtesa kiumbe wa namna hii ?? Daah
 
Kuna mambo lazima yatokee ili maisha ya kibinadamu ya kamilike. Unachosema ni sawa na kuwaambia simba wasiwinde swala kisa si kitendo cha haki, nachomaanisha hata ungeandika article ya page milioni mbili bado mambo hayo yatatokea leo, kesho, miaka 10 ijayo ni kizazi chote kijacho.
 
Kweli kabisa mtu unamwambia nimeolewa Lakin bado ana n'ga n'gania
 
Halafu unajua huwa sielewagi sakolojia ya mtu anayemtenda mwenzake. Yaani bora mtu ambaye from 1st mnakutana alishakutell kuwa yeye hajakuelewa na hawezi kuwa nawe. Ila sasa kuna yule ambaye anakuwa anasita mwanzoni halafu anakukubalia ukishaingia nae umeshajua utamu wa kuwa nae tena baadae anakubadilikia anakwambia hawezi kuendelea na wewe yaani anakuacha unahang hata haujielewi wapi pakushika yaani sometimes unatamani hata umteke maana hajui tu namna uwepo wake kwenye maisha yako ulivyo na umuhimu. Mimi kuna kasichana kalinifia utadhani kalirogwa na mimi. Kakawa kanafanya kila lililopo ndani ya uwezo wake kawe na mimi. Kalikuwa tayari hata tutafute chumba ili tukakae hue na kipindi hicho me ni denti wa form five.

Nikajitahidi sana kukapa lecture kuwa inabidi atafakari upya kuwa na mimi. Ila alikuwa haelewi. Nilichomsaidia ni kutojionyesha na mtu mwingine kwake yaani kama nipo single tu muda wote. Na kalikuwa sometimes kanakuja nikape hug tu na kiss ili kapate usingizi. Ila nashukuru baada ya muda nilikwenda chuo na yeye akahama mkoa ndio ikawa ponea yangu kumuumiza hisia.

Ila kama ningemkubalia halafu nikamgegeda akaenjoy then nikaamua mtema hapo sasa ndipo ningekuwa nimezingua maana sasa imagine mtu amejua tayari mnalianzisha halafu unakuja mchenjia katikati ya safari.....unaweza muuwa kwa presha mtoto wa watu.
Kiongozi yani ni tabu hali si nzuri kwangu naona mapichapicha kila napomuona na siwezi kumuepuka ni lazima nimuone kila siku maana tupo jirani sana
 
sometimes haina haja ya kuwalaumu hao tunaosema wanachezea hisia za watu, maana mapenzi kitu cha ajabu sana, unaweza ukampenda mtu sana tu ila unakuta as days go hawi vile unavyotaka awe, yuko static, sasa inabidi tu kuliko kuendelea naye unamchana makavu( hapo unakuta tayari mmeishi wote hata mwaka hivi), sasa ukifikia maamuzi hayo mtu anaona ni kama vile ulikuwa unachezea tu hisia zake kwa mwaka mzima.... kumbe ni akili tu imegoma kuendelea kumpenda mtu.

NB: hakuna mtu anayechezea hisia za mtu.
 
Mapenzi bwana...ningekuwa na uwezo nisinge penda tena [emoji22][emoji22] Maana sijui kama kunabinadamu alie tendwa na kuumizwa kama mm ....MAPENZI yanakufanya unalia kama mpumbavu unashindwa kula kama ...unakuwa kama mwendawazimu aagh.
Penda kiasi na unatakiwa ukumbuke mwanadamu sio mkamilifu
 
MMMh jamani mapenzi yanauma hapa nilipo niko hoi na maumivu ya moyo Mdada amenipiga stop hata kumtumia ujembe.nimekunywa pombe lakini bado moyo unauma hatari aisee hali niliyonayo ni mbaya wakuu Dogo mkali kila eneo ila ndio ivyo kanipiga chini mazima
Piga moyo konde maisha yaendelee
 
Tukifika Wakati watz tuweze kutofautisha mapenzi na matamanio yetu ya kimwili au tamaa za Mali hapo ndipo tutakuwa na pair imara za watu wanaopendana kwa dhati na familia bora.

Muda wa mapenzi ya kukurypuka na kuvulia watu nguo hovyo umepita na wakati tujali utu wetu na kutafuta maisha standard. Kupoteza mali na muda kuhonga mtu asiye jitambua ni ujinga kama ujinga mwingine. Kwanza mlikutana wapi, mmefahamiana muda gani, mliwahi kusaidiana nini kabla. Penzi likiisha ni kitu gani kitabaki kuwaunganisha kama watu wengine.

Penzi ni Furaha ni Amani ni kujitoa na kujinyima kwa yule umpendae kwa dhati bila kuathiri MIPANGO yako ya utafutaji. Kama hakuna ni bora kuishi kujitoa mapema kwa kumueleza uwazi mwenzio. Mapenzi siyo Utumwa ni Hiari.
 
Back
Top Bottom