Katu sitakula makombo hata yawe ya Biriani

Katu sitakula makombo hata yawe ya Biriani

Anold

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2010
Posts
1,456
Reaction score
615
Ni lazima nibaki na msimamo huu pamoja na ukweli kuwa rafiki zangu wamenishauri ni tafakari lakini hii haiwezekani, nilitokea kumpenda binti mmoja ambaye toka yupo kidato cha tatu tumekuwa marafiki.

Baada ya kubainika na wazazi wa binti kuwa mimi ndiye niliyemenya ndizi kwa binti, wazazi wake hawakuwa na papara, makubaliano nikuwa nimtunze, nimsomeshe vinginevyo waende mbele (tulikubaliana niishi naye).

Nilikubali yote, binti alimaliza kidato cha nne kwa bahati akafaulu akaenda kidato cha tano na kumaliza kidato cha sita kwa ufaulu mzuri, pamoja na ugumu wa pesa nilijitahidi aende kwenye Chuo kimoja Kikuu kilichoko mkoa wa Morogoro.

Mambo yalibadilika alipokuwa mwaka wa tatu ambapo alikutana na wajanja wanaojua mapenzi wasiojali kuwa mpaka kufika hapo alipofikia kuna mtu aliteseka na kuhangaika, sikujua kilichoendelea lakini nilihisi kuwa kuna kitu.

Kwanza siku moja usiku wakati tumemaliza kuwasiliana na mpenzi wangu huyu simu yake alisahau kuizima nilisikia kama sauti ya mwanaume ikinon'gona ikimtaka ageuke, lakini baadae kidogo nilisikia binti akisema weka mafuta kwanza.

Kwa namna ya sauti ilivyotoka ilionyesha wazi kuwa mpenzi wangu huyu yupo na mtu na wanafanya mapenzi, baadae simu ilikatika na sikuelewa tena kilichoendelea.

Pamoja na kuwa idadi ya mawasiliano aliyoyokuwa anayafanya kwangu yalipungua sana na mara nyingi nikimpigia simu iliita na hata akipokea alinishauri nimcheki baadaye

Maana wapo kwenye discussion (kumbuka mimi ndiyo mlipaji ada na kila kitu unachojua chuo maana yeye hakupata mkopo kwa asilimia 100).Baada ya binti kurudi likizo nilimuona kama mtu asiye na furaha.

Hata hivyo jioni moja nikamuuliza kuwa mbona amebadilika alinyamaza kimya tu siku ya pili niliporudi kutoka kibaruani akaniambia ana neno lakini nisimuelewe vibaya.

Alianza kwa kuniambia kuwa kwa kweli tumeishi vizuri toka yupo kidato cha tatu na anashukuru kwa moyo wangu wa kusaidia lakini alinieleza kuwa kwakweli huko(chuoni) amepata mtu anampenda na moyo wake ndiyo unampenda na wameshakubaliana wafunge ndoa.

Kwakweli nilisikitika na nilimweleza kuwa anachokifanya sio sawa na kuwa tumetoka mbali nk, kwa kweli hakunisikiliza na kwakuwa wazazi wake hawakai mbali na hapo tulipokuwa tukiishi nilimshauri twende kwa wazani wake ambapo baadaye niligundua kuwa hata wazazi wake wanaunga mkono binti kunibwaga.

Basi binti aliondoka ila kilichotokea ni kuwa ule muda ambao alisema angeolewa hakuolewa aliendelea na Chuo akamaliza na baadaye akarudi mtaani kwao, akijaribu kutafuta kibarua kwa njia mbalimbali, mimi nimekuwa nikiendelea na maisha yangu na kwa bahati Mungu alinishushia neema fulani kwa kweli nafurahia maisha kiasi cha kumiliki kauafiri kangu tena sio ka mkopo.

Majuzi binti amekuja kuniomba radhi kuwa yale yaliyotokea ilikuwa ni shetani tu ila anatubu na kuwa siku zote hapati usingizi akijutia kosa alilolifanya na anajisikia vibaya ukizingatia toka kidato cha tatu mimi ndiye nilikuwa namlipia ada na matumizi yote muhimu, sasa imekuwa ni kero maana hata wazazi wake wanataka nisamehe.

Ila mimi nilishajipanga kivingine pamoja na ukweli kuwa huyu binti wakiitwa warembo hawezi kuacha kutoka lakini nahisi kumrudia ni sawa na kula makombo kauli yangu sasa ni kuwa "katu sitakula makombo hata yawe ya biriani".

Nakaribisha ushauri!
 
Bro apa mjin,mchumba hasomeshwi labda awe ni mke wako na ana mtot wak,azawaiz lazm aliwe bt ucjal ndo maisha
 
Amesha tambua kosa lake, mimi nakushauri umsamehe kwa mwanamke hawezi kwenda chuo akakosa mpnz hata kama amemuacha mume Nyumban,
 
Mmh ungekuwa hutaki kula makombo hata ushauri usingeomba. Binti aliponzwa na tamaa akadhani the pasture was greener on the other side. But mwisho wa siku kajikuta amekosa vyote. Na Hao wazazi wake ni wazazi waliojaa tamaa, hawana utu na hawana shukrani hata kwa yale uliyoyafanya kwa ajili ya binti yao. Ndo maana hata hawakumshauri binti alivyotaka kukubwaga. Asiyeshukuru kwa kidogo...

Haya hapo kuna mawili. 1. Binti ameona makosa yake, akajutia na ndo maana amerudi kwako kuomba msamaha
2. Mambo yamemchachia, alidhani amewin kumbe kapotea, so kaona bora tu ajirudishe kwa mfadhili wake. Sasa kujua kama anamaanisha huo msamaha ndo shughuli. Mwisho wa siku kaa, ufikiri kwa makini kabla hujaamua chochote juu ya huyo binti. Kila la kheri.
 
Kwanza geuka nyuma, pili paka mafuta.. Asee huyo binti kaliwa tigo.. Yani hapo hata ukimuoa hilo doa la kuliwa tigo litamsuta. Na ipo siku atakuambia utumie tigo na wew...
Kama huyo binti anajiona amebadirika basi amtafte bwana mwingine na sio wew..
 
Kwanza geuka nyuma, pili paka mafuta.. Asee huyo binti kaliwa tigo.. Yani hapo hata ukimuoa hilo doa la kuliwa tigo litamsuta. Na ipo siku atakuambia utumie tigo na wew...
Kama huyo binti anajiona amebadirika basi amtafte bwana mwingine na sio wew..
Astakafllahu
 
Amesha tambua kosa lake, mimi nakushauri umsamehe kwa mwanamke hawezi kwenda chuo akakosa mpnz hata kama amemuacha mume Nyumban,
Kwa namna alivyokuwa ananieleza kwa nyodo na kubinua midomo uwezo na ujio wa mpenzi mpya usingedhani kuwa sasa hivi hata hela ya pedi ni ishu.
 
Kitu kimoja ambacho unatakiwa kujua ni umecheleweshwa kuwa na mafanikio kwa kubeba majukumu ya baba wakati wewe ni mpenzi (baby hasomeshwi) lakini kwa maelezo yako ukimrudia huyo binti basi wewe ndio Mwenye matatizo sio binti na familia yake.
 
Kuna kitu unaweza fanya nacho kimoja tu mtumie tu na sio
Kumuoa elewa kabisa huyo sio mke na hawezi Tafuta mke Ila
Sio
Huyo!!
 
Ushauri wa nini tena na umesema huli makombo..... :A S embarassed:
 
pole mkuu

1. hao wazazi wa bint wamenishangaza kumkabidhi bint umsomeshe toka form 3 nawe ulikubali kwa makubaliano gani
2. wazazi kumkubalia binti aolewe na mweingine baada ya kuona wewe sio chochote wala lolote wala hawakuona kwamba umefika hapo ulipo kwa kujitoa kumsomesha binti yao
3. umeshaamua kutokula matapishi yako huna haja ya kutaka ushauri songa mbele utampata atakayekuthamini.
4. wamekuona na usafiri wamerudi huna thamamani kwao ni tamaa
 
Huyo alikuwa katika foolish age na sasahivi akili ya kiutuuzima ndipo inapomrudia, kama hauko committed unaweza kumsikiliza zaidi na mkaendelea na maisha lakini kama una maisha mengine mpishe apite tu atafika anakoelekea, sometimes people don't notice the things we do for them until we stop doing it
 
Endelea na maisha yako na usirudi nyuma,ukirudi tu jua kuwa umeumia maana huyo mwanamke hakufai na atakuharibia maisha.Wanawake wazuri wa tabia na sura wapo wengi hivyo tafuta mwingine maisha yaendelee.
 
Wakati Mwingine Shetani Tunamuonea Sana Hata Sehemu Ambayo Hahusiki Basi Lazima Tumuweke tu
 
Msamehe!! Anatambua alichokifanya na atakuwa royal kwako maisha yake yote!!! Labda useme humpendi tena lakini kama bado unapenda chukua mzigo wako!! Toka kidato cha 3 sio mchezo.....!! Zimwi likujualo halikuli likakumaliza!!! Utaanza kutafuta mwanamke mpya changamoto nyingine hiyo!!!
 
Anold

pole shetani poleee- kwa kusingiziwa polee shetani poleeee. Ivi shetan atasingiziwa mpaka lin? Mtoto wa primary ni rahis kupitika na shetan, hata wa chuo???? Wee kaka think big otherwise utakuja jutia maisha yako yote.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom