Katles za samaki

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,753
2,000
Mahitaji


Viazi kilo 1

Samaki asie na miba

Limau 1

Karot 1 ndogo ipare

Pilipili mboga 1 rangi upendayo kata ndogo ndogo

Kitunguu maji 1 kidogo kata ndogo ndogo

Kitunguu saumu 1/2 teaspoon

Tangawizi 1/2 teaspoon

Pilipili manga 1/2 teaspoon

Bizari ya pilau 1/2 teaspoon

Pilipili ya kuwasha 1/2 teaspoon

Mdalasini 1/2 teaspoon

Mayai 2

Bread crumbs/unga wa ngano

Namna ya kutaarisha

Menya na chemsha viazi vyako weka chumvi kidogo

Vikiwiva mwaga maji then bonda bonda weka pembeni

Safisha samaki wako vizuri then mueke chumvi,kitunguu saumu,pilipili manga na ya kuwasha,tangawizi na limau kipande na maji kidogo sana ....acha achemke

Akikaribia kuwiva weka pilipili mboga,karot na kitunguu maji

Epua na mchambue chambue samaki

Mimina samaki na vegetables zote katika viazi ulivobonda

Changanya vizuri

Ongeza chumvi na limau kama vinahitajika

Tengeneza round au oval kwa kutumia huo mchanganyiko

Pakaa unga wa juu yake

Vunja mayai katika bakuli

Weka mafuta kwenye karai jikoni

Chukua huo mviringo wa viazi pakaa yai

Weka katika karai

Kaanga hadi ziwe brown


Katlesi tayar kwa kuliwa


 

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Mar 21, 2013
37,145
2,000
asante farkhina unajua kupika hadi raha

ile keki nilijaribu ila ilikua kama inajiachia kuweka ufa kwa juu
 
Last edited by a moderator:

rasai

Senior Member
Jun 24, 2013
147
225
Safi sana, shukran kwa upendo wako kwetu, hutunyimi ujuzi, tunaerevuka. Mapishi muhim kwa afya zetu na kwa ndoa zetu
 

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,753
2,000
Safi sana, shukran kwa upendo wako kwetu, hutunyimi ujuzi, tunaerevuka. Mapishi muhim kwa afya zetu na kwa ndoa zetu

Shukraan pia kwa sote tunavojumuila hapa kubadilishana ujuzi inapendeza kwa kweli tujitahidi hili jukwaa tulitumie vilivo ili tunufaike
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom