katika Utawala chini ya #MfumoJiwe kuna teuzi za adhabu na teuzi za zawadi

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
wakuu hii nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kipekee sana kwa sasa. kuna nafasi nyingi za uteuzi zinatumika kama adhabu ukiona mtu kapelekwa huko ujue hajamrishisha mkuu au hajautumikia vema #MfumoJiwe. utaalamu na ujuzi umewekwa chini na hauna nguvu tena ndani ya #MfumoJiwe. kati ya nafasi zinazoongoza kwa adabu ni ukatibu tawala na ubalozi.

fikiria uteuzi wa leo. hebu niambieni kwa ukubwa wa matatizo ya waalimu vyuo vikuu yani unaanzaje tu kumchukua profesa mwenye phd ya IT ( prof kamuzora) akafawe katibu tawala wa mkoa. hizi ni kazi za kawaida sana amekua akiwapa makada wa chichiemu, kuwahonga kina kafulila, na kuwatupa huko watu waliowadhibu kwa kutomridhisha kama yule aliyekua anaongoza kikosi cha watu wasiojulikana na baadhi ya makamanda wa polisi.

au niambieni wakuu ni busara au umaalumu gani unamtuma magufuli kuteua daktari mwenye maadili na ujuzi wa hali ya juu kama dr mpoki na ambaye kwenye fani yake wako wachache nchini kuwa balozi wa ubalozi usiojulikana? na haya ni maamuzi ya rais mwenye phd . tuna shida kama nchi maana anayeamua vipaumbele vyetu ana yake.

pia mukumbuke kimkakati kutanganzwa kwa teuzi za leo kunapotezea kiana mjadala wa CAG kuitwa jana kama kibaka na ndugai maana kuna kila dalili kwamba yeye alitumwa tu na bosi wake.

nawe orodhesha teuzi zingine unazojua ni za adabu au zawadi. ngoja nikupe za kuanzia

Teuzi za adhabu.
1. Robati Makungu (mkuu wa wasiojulikana) - RAS tabora
2. Prof F kamuzora - RAS Tabora
3. Dr. Ramadhani Dau - Balozi
4.
5.

Teuzi za zawadi.
1. Mwita Mikabwe
2. Paul Makonda.
3. Kafulila
4. Buteko
5.
 
Back
Top Bottom