Katika Ukristo, kitendo cha msamaha ni cha lazima, si hiari!

Nawasalimu nyote!

Niwakumbushe wakristo, hususani wakatoliki kujibidisha katika kusamehe watu, kabla nyakati za hatari hazijafika!

Ukumbuke Sala yako ya kila siku, ile Sala ya "Baba Yetu..." iliyoachwa na Yesu Kristo, ile inayofundishwa na kanisa kwa vijana wa kanisa, kwenye mafundisho ya Holy Communion!

Sala hii inatutaka tumuombe Mungu Msamaha, Kama sisi wenyewe tunavyowasamehe wale wanaotukosea!

Kama hauwezi kusamehe, jiepushe kusali ile Sala! Utakuwa unaongea udanganyifu!

Kama hauwezi kusamehe, hauna namna ya wewe kusamehewa na Bwana Mungu wetu!

Mungu Mwenyezi, atuhurumie Sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Umenukuu misitali hinayo mtaka mtu kusamehe lakini pia hipo misitali inayo mtaka mja kulipiza kisasa kama yalivyo fanyiwa jino kwa jino
 
Halafu watu wanapaswa kuelewa kuwa kumsamehe mtu ni jambo moja lakini kuwajibika kwa makosa yake mkosa ni jambo lingine.

Unaweza ukamsamehe mtu moyoni saa na mlikutana mnasalimiana kawaida lakini kuwajibika kuliko pale pale.

Mfano mtu amekukopa hela halafu hajakulipa kwa wakati mlokubaliana,
Akija akaomba msamaha utamsamehe Kwa utapeli na uongo lakini deni lazima alipe.
Sio kwenye Ukristo ndugu yangu, ngoja nikupe andiko:

Luka 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³⁵ Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
³⁶ Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
 
Na kwenye uislam je?

"Na Tumewaandikia sharia humo kwamba nafsi kwa nafsi, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino, na majaraha ni kisasi. Lakini atakayesamehe kwa kutolea sadaka, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu".
-Quran(5:45)
 
Kitendo Cha hiyari,uamuzi ni wa mhusika
Kuchukua hatua au kusamehe
Hii ni mojawapo ya tofauti kubwa kati ya Ukristo na Uislamu. Kwenye Ukristo mwenye kuhukumu ni Mungu pekee, kwani Yeye ndiye mwenye kuona rohoni. Mwanadamu huhukumu kwa jinsi ya mwili lakini Mungu huitazama roho ya mwanadamu.
 
Nawasalimu nyote!

Niwakumbushe wakristo, hususani wakatoliki kujibidisha katika kusamehe watu, kabla nyakati za hatari hazijafika!

Ukumbuke Sala yako ya kila siku, ile Sala ya "Baba Yetu..." iliyoachwa na Yesu Kristo, ile inayofundishwa na kanisa kwa vijana wa kanisa, kwenye mafundisho ya Holy Communion!

Sala hii inatutaka tumuombe Mungu Msamaha, Kama sisi wenyewe tunavyowasamehe wale wanaotukosea!

Kama hauwezi kusamehe, jiepushe kusali ile Sala! Utakuwa unaongea udanganyifu!

Kama hauwezi kusamehe, hauna namna ya wewe kusamehewa na Bwana Mungu wetu!

Mungu Mwenyezi, atuhurumie Sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
ni lazima kuomba ama kutoa msamaha?
 
Hii ni mojawapo ya tofauti kubwa kati ya Ukristo na Uislamu. Kwenye Ukristo mwenye kuhukumu ni Mungu pekee, kwani Yeye ndiye mwenye kuona rohoni. Mwanadamu huhukumu kwa jinsi ya mwili lakini Mungu huitazama roho ya mwanadamu.
Kwa mantiki hiyo hakuna haja ya kuwa na mahakama duniani.
Kila anaefanya dhulma asamehewe.
Mwizi asamehewe.
Wahaini wasamehewe.
Wauaji wasamehewe n.k

Tukiwa na mtazamo huo Dunia haitokalika Mkuu, kila kitu kinataka kiasi kama unamhukumu mtu umhukumu Kwa kiasi na kama unasemehe samehe Kwa kiasi.

Ukiwa msamehevu sana basi watu watakupanda mpaka kichwani wakufanyie wanachotaka.
 
kisasi kisasi kisasi ni cha lazima
 
Dunia ya wakristo, haihitaji, mahakama, Wala jeshi la ulinzi!
Dunia ya wakristo Ni ya upendo na Amani!

Dunia hii itapatikana baada ya kuondolewa kwa dunia hii ya Sasa!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
K
Hii ni mojawapo ya tofauti kubwa kati ya Ukristo na Uislamu. Kwenye Ukristo mwenye kuhukumu ni Mungu pekee, kwani Yeye ndiye mwenye kuona rohoni. Mwanadamu huhukumu kwa jinsi ya mwili lakini Mungu huitazama roho ya mwanadamu.
Kwa hivyo ukristo unatofautisha mwili na roho?
So nahitaji ya mwili Nani anayatimiza?
 
Yesu hakuwahi kucondemn justice insstitutions Bali abuse yake (injustice). In fact yeye mwenyewe alijua kuna watu magerezani na ndio maana aliamuru kuwatembelea wafungwa. Mfumo wa jamii lazima uwe na justice system. Kusamehe kupo lakini justice inahitaji kulipa makosa. Unaweza kusamehewa lakini you have to pay. Na msamaha wa kweli Hata kwa Mungu unakuhitaji kufanya malipizi. Huwezi kusamehewa dhuluma bila kurudisha kwa uliowadhulumu. Pia kuna watu ambao Hata wakipata msahama wa kiroho lazima watengwe na jamii ili iwe salama. Mfano rapists, serial killers. Huwezi kuwa mjinga eti Lisa msamaha wabaki kwenye jamii kiss msamaha. That's why life imprisonment is justifiable. Hakuwezi kuwepo sheria bila penalties.

NB. Faith and reason vinaenda pamoja. Kumbuka kwenye kila tendo tunaangalia lengo, mtendaji, mtendwa, na lengo. Msiwe fundamentalist reading of the bible. Msamaha unabaki lakini puns gemmy for offence is indispensable for social coherence. Hata makanisani kuna mifumo ya adhabu usipofanya jambo.

Pengo mwenyewe alishawahi kumfukuza usista sister mmoja. Ingawa ilibatilishwa since hakuwahi na mamlaka naye.

Kila kanisa (pamoja na haya mapya) kuna taratibu zake na usipofuata there is some form ya penalty. Sembuse secular world?
 
Huwa najiuliza sana huu msamaha kama watu wote, tutakuwa wakristo, dunia itakuaje?
 
Nawasalimu nyote!

Niwakumbushe wakristo, hususani wakatoliki kujibidisha katika kusamehe watu, kabla nyakati za hatari hazijafika!

Ukumbuke Sala yako ya kila siku, ile Sala ya "Baba Yetu..." iliyoachwa na Yesu Kristo, ile inayofundishwa na kanisa kwa vijana wa kanisa, kwenye mafundisho ya Holy Communion!

Sala hii inatutaka tumuombe Mungu Msamaha, Kama sisi wenyewe tunavyowasamehe wale wanaotukosea!

Kama hauwezi kusamehe, jiepushe kusali ile Sala! Utakuwa unaongea udanganyifu!

Kama hauwezi kusamehe, hauna namna ya wewe kusamehewa na Bwana Mungu wetu!

Mungu Mwenyezi, atuhurumie Sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Huyo Mungu wako mbona hatoi msamaha wa jumla na akatengeneza Jehanum kisha akaua kwa kimbari dunia nzima kwa mafuriko
 
Back
Top Bottom