Katika Ukristo, kitendo cha msamaha ni cha lazima, si hiari!

Weakman

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
1,092
Reaction score
1,702
Nawasalimu nyote!

Niwakumbushe wakristo, hususani wakatoliki kujibidisha katika kusamehe watu, kabla nyakati za hatari hazijafika!

Ukumbuke Sala yako ya kila siku, ile Sala ya "Baba Yetu..." iliyoachwa na Yesu Kristo, ile inayofundishwa na kanisa kwa vijana wa kanisa, kwenye mafundisho ya Holy Communion!

Sala hii inatutaka tumuombe Mungu Msamaha, Kama sisi wenyewe tunavyowasamehe wale wanaotukosea!

Kama hauwezi kusamehe, jiepushe kusali ile Sala! Utakuwa unaongea udanganyifu!

Kama hauwezi kusamehe, hauna namna ya wewe kusamehewa na Bwana Mungu wetu!

Mungu Mwenyezi, atuhurumie Sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
MSISITIZO WA BIBLIA ZAIDI YA MISTARI 120 INASISTIZA KUSAMEHE.

MIFANO MICHACHE.

Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.

Zaburi 86:5
Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.

Mithali 19:11
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

Mathayo 6:12
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

Mathayo 6:14
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Mathayo 6:15
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.

Mathayo 9:6
Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?

Mathayo 18:21
Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]

Marko 11:26
Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].

Luka 11:4
Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.

Luka 17:3
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.

Luka 23:34
 
Hapo ndio utaona utofauti wa Mungu wanaomwabidu Wakristu na wanaomwabidu Imani nyingine. Kutamka Mungu haimaanishi wote wanasifa Moja lazima mmoja ni kitu tofauti na hata katika Maisha ya kawaida unaweza kumtambua mtu Mwema kwa matendo yake na Wala siyo asemayo Wala umahiri wake wa kuimba vifungu vya kitabu chake, mara kifungu hiki kinasema hivi, mara hivi.

Mfano huna dini yoyote, unakutana na watu wawili ,Wana dini tofauti wanakushawishi ujiunge na Imani Yao.

Mmoja anakuambia msamaha ni tiba, msamehe mwenzako mara Saba mara sabini.

Mwingine anakuambia Mungu wao anawaambia "Enyi mlio AMINI😄😄 kutibahalei kum il qisas . Al qisas haq" wewe utamfuata Mungu yupi?
 
Nawasalimu nyote!

Niwakumbushe wakristo, hususani wakatoliki kujibidisha katika kusamehe watu, kabla nyakati za hatari hazijafika!

Ukumbuke Sala yako ya kila siku, ile Sala ya "Baba Yetu..." iliyoachwa na Yesu Kristo, ile inayofundishwa na kanisa kwa vijana wa kanisa, kwenye mafundisho ya Holy Communion!

Sala hii inatutaka tumuombe Mungu Msamaha, Kama sisi wenyewe tunavyowasamehe wale wanaotukosea!

Kama hauwezi kusamehe, jiepushe kusali ile Sala! Utakuwa unaongea udanganyifu!

Kama hauwezi kusamehe, hauna namna ya wewe kusamehewa na Bwana Mungu wetu!

Mungu Mwenyezi, atuhurumie Sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wenye kutoa msamaha ndiyo vinara wa kuuzuia
 
Kwa hiyo tunakubaliana ukaidi ndio ukiomuondoa marehemu duniani..
 
Msamaha hauji automic lazima ujue kosa lako na uombe msamaha bila hivyo maana yake wewe ni kiburi.
Na ndio maana IBILISI hakusamehewa kwa sababu ya Kiburi chake.
Kama msamaha inakuja automatic kusingeandaliwa Jahanamu.
Yametokea. Kakuita ukapate adhabu ya dunia
 
Msamaha hauji automic lazima ujue kosa lako na uombe msamaha bila hivyo maana yake wewe ni kiburi.
Na ndio maana IBILISI hakusamehewa kwa sababu ya Kiburi chake.
Kama msamaha inakuja automatic kusingeandaliwa Jahanamu.
Huu nao ni uongo wa kuzimu. Hebu fikiria, wewe unaweza kuzitaja dhambi zako zote mbele ya Mungu ili akusamehe? Kama Mwenyezi Mungu akikuwekea standard hii utatoboa? Kwa maana hiyo hatutoi msamaha ili kumfaidia tunaye msamehe bali tunasamehe ili sisi tupone!! Msamaha ni kwa faida ya anayesamehe, si vinginevyo, kwani anayesamehewa bado anayo kesi ya kujibu mbele ya Mungu kama hatofanya toba. Na hiyo ndio maana ya kusema HUKUMU ATOAYE NI MUNGU PEKEE.

NB: hukumu ya shetani haina uhusiano na kutambua makosa yake na hivyo kuomba msamaha. Kumbuka IKO DHAMBI YA MAUTI, hata wewe unaweza kuitenda hiyo nawe hutasamehewa hata kama utawasamehe wengine.
 
Nawasalimu nyote!

Niwakumbushe wakristo, hususani wakatoliki kujibidisha katika kusamehe watu, kabla nyakati za hatari hazijafika!

Ukumbuke Sala yako ya kila siku, ile Sala ya "Baba Yetu..." iliyoachwa na Yesu Kristo, ile inayofundishwa na kanisa kwa vijana wa kanisa, kwenye mafundisho ya Holy Communion!

Sala hii inatutaka tumuombe Mungu Msamaha, Kama sisi wenyewe tunavyowasamehe wale wanaotukosea!

Kama hauwezi kusamehe, jiepushe kusali ile Sala! Utakuwa unaongea udanganyifu!

Kama hauwezi kusamehe, hauna namna ya wewe kusamehewa na Bwana Mungu wetu!

Mungu Mwenyezi, atuhurumie Sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kama unamwongelea Membe kwa lugha ya mzunguko basi ni kwamba Membe ana haki ya kufidiwa kama mahakama ilivyoamua kisheria. Wewe ukibomolewa nyumba yako na mtu na mahakama ikaamuru ulipwe ni uhuru wako kuchukua fidia hiyo au kuacha (kusamehe).
 
Huu nao ni uongo wa kuzimu. Hebu fikiria, wewe unaweza kuzitaja dhambi zako zote mbele ya Mungu ili akusamehe? Kama Mwenyezi Mungu akikuwekea standard hii utatoboa? Kwa maana hiyo hatutoi msamaha ili kumfaidia tunaye msamehe bali tunasamehe ili sisi tupone!! Msamaha ni kwa faida ya anayesamehe, si vinginevyo, kwani anayesamehewa bado anayo kesi ya kujibu mbele ya Mungu kama hatofanya toba. Na hiyo ndio maana ya kusema HUKUMU ATOAYE NI MUNGU PEKEE.

NB: hukumu ya shetani haina uhusiano na kutambua makosa yake na hivyo kuomba msamaha. Kumbuka IKO DHAMBI YA MAUTI, hata wewe unaweza kuitenda hiyo nawe hutasamehewa hata kama utawasamehe wengine.
Nadhani tunatofautiana kwenye Imani, nikiendelea kueleza kwa mujibu wa Imani yangu tunaweza kukesha na tusiufikie muafaka.
 
Halafu watu wanapaswa kuelewa kuwa kumsamehe mtu ni jambo moja lakini kuwajibika kwa makosa yake mkosa ni jambo lingine.

Unaweza ukamsamehe mtu moyoni saa na mlikutana mnasalimiana kawaida lakini kuwajibika kuliko pale pale.

Mfano mtu amekukopa hela halafu hajakulipa kwa wakati mlokubaliana,
Akija akaomba msamaha utamsamehe Kwa utapeli na uongo lakini deni lazima alipe.
 
Nadhani tunatofautiana kwenye Imani, nikiendelea kueleza kwa mujibu wa Imani yangu tunaweza kukesha na tusiufikie muafaka.
Yap, you're right. Mimi nineelezea imani yangu kwa Kristo, unconditional love, unconditional forgiveness. Kwa hilo nakubaliana nawe
 
Back
Top Bottom