Katika ripoti ya mafanikio ya awamu ya 6 tuwekewe na Idadi ya Chawa wapya waliozalishwa.

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,496
37,789
Kila mara wapambe, mawaziri, Makatibu na hata wakuu wa mikoa na wilaya wanaposimama kuhutubia tunaambiwa Kwa miaka 2 (2021-2023) ya Rais Samia Mambo mengi yefanywa Kwa ufanisi na maendeleo Makubwa kuliko miaka 5 ya Magufuli. Tunaojua Uchawa ulianzishwa enzi za Magufuli na Samia kaona wanafaa akaruhusu wasajiliwe rasmi. Kwa hiyo haya nayo ni sehemu ya Maendeleo Kwa miaka hii 2 zaidi ya miaka 5 ya nyuma.

Kwa hiyo tunaomba mnapotoa takwimu za Mambo ya kujibunia toeni na Idadi kubwa ya Machawa wiozalishwa awamu ya sita Hadi kufikia hatua ya kuunda NGO (Chawa wa Mama).
 
Ila naamini hadi chawa kuzidi kuzaliana kwa wingi zaidi mara nyingi mazingira ujue ni machafu sana. Ebu tuhamishie huu uhalisia katika hilo yawezekana ikawa ni hivyo??
Hali itakuwa ni hivyo. Kusingekuwepo na mazingira ya wao kuzaliana kwa wingi, wasingezaliana kwa kiwango cha kutisha kiasi hiki.

Kwa sasa kila mtu anaamini kufanikiwa kimaisha kupitia uchawa! Na siyo kitu kingine chochote kile! Jambo ambalo ni hatari sana kwa mustakabari wa maisha yetu hapo baadaye.
 
Weka na
Kila mara wapambe, mawaziri, Makatibu na hata wakuu wa mikoa na wilaya wanaposimama kuhutubia tunaambiwa Kwa miaka 2 (2021-2023) ya Rais Samia Mambo mengi yefanywa Kwa ufanisi na maendeleo Makubwa kuliko miaka 5 ya Magufuli. Tunaojua Uchawa ulianzishwa enzi za Magufuli na Samia kaona wanafaa akaruhusu wasajiliwe rasmi. Kwa hiyo haya nayo ni sehemu ya Maendeleo Kwa miaka hii 2 zaidi ya miaka 5 ya nyuma.
Kwa hiyo tunaomba mnapotoa takwimu za Mambo ya kujibunia toeni na Idadi kubwa ya Machawa wiozalishwa awamu ya sita Hadi kufikia hatua ya kuunda NGO (Chawa wa Mama).
Weka na idadi ya nyani tulinganishe
 
Ufaransa imeweka wazi kuwa imezalisha Mamilioni ya Kunguni mbona hawa wa hapa wana ona aibu kutuambia idadi ya Chawa waliozalishwa na hii awamu?

Umeme Zero lakini Chawa millioni ishirini.
 
Awamu naamini kuna laana inatunyemelea kwa kasi. Maana binadamu wa kawaida mwenye utashi huwezi kujivunia ubaya.

Mtu mzima ana nywele kila sehemu lakini anajisifia kuwa yeye ni chawa. Unamwonaje mtu anapojisifia kuwa yeye eti ni chawa? Mtu kujiita chawa ni sawa na kujiita wewe ni kunguni, nzi au hata kinyesi.

Safari hii tusishangae kuna watu baadaye watajiita wao ni kinyesi cha mama, na kwao wataona ni sifa ya kuupata uongozi.
 
Back
Top Bottom