Katika Mapambano Yoyote, Mafanikio ni Kutengeneza Mazingira ya Kuzungumza

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Baada ya Mbowe kufutiwa kesi na mahakama, kufuatia ombi la DPP kutotaka kuendelea na kesi, wengi wameongea mengi. Wengine wameongea kwa kuegemea weledi wa kisheria, wengine kwa kuegemea ujinga wao wa kutojua sheria, na wengine kwa kulalia ushabiki wao wa kisiasa.

Litakalokuwa kuwa ni kweli:

1) Mahakama imewafutia kesi Mbowe na wenzake

2) DPP ameomba kesi iondolewe, na hataki kuendelea nayo

3) Rais Samia amemwalika Mh. Mbowe ikulu na kuzungumza naye kirafiki kwa nia ya kujenga mshikamano wa kitaifa

Kwa ujumla, huu ni ushindi mkubwa kwa Freeman Mbowe ambaye hana dola. Freeman Mbowe ameiomba nafasi ya kukutana na Rais mara kadhaa, kuanzia enzi za Magufuli, hakuipata hiyo nafasi, lakini jana ameipata bila ya kuomba, bali kwa kualikwa.

Kwa chama cha siasa, ambacho kinatafuta nafasi ya kuongoza au kushiriki kwenye uongozi wa nchi kwa njia ya kisiasa, silaha yake kubwa ni uwezo wake kuyatengeneza mazingira ya kuwalazimisha wenye dola wakubali kukaa na kujadiliana. Na hili limefanyika, na huko mbeleni huenda kukawa na kukutana zaidi.

Kwa upande mwingine, Samia naye amepata ushindi. Ameweza kutengeneza mazingira ambayo yanamnyima Mbowe na CHADEMA kumsema vibaya yeye binafsi au serikali yake, iwe na yeye Mbowe au CHADEMA. Hii ni mbinu ya kisiasa. Hakutaka kutoa nafasi kwa Mbowe kuanza kuongea na wapenzi wake kwanza, kabla ya yeye kukutana naye, na kupunguza munkari, hasira na chuki.

Samia ni Rais, je tunamtarajia aje kwenye TV aseme kuwa namwomba msamaha Mbowe? Au Serikali iseme inamwomba msamaha Mbowe? Hilo halitatokea, ila matendo ya Rais Samia yanaongea zaidi kuliko maneno.

Sisi wengine, tumekuwa tukimwunga mkono kwa kiasi kikubwa Rais Samia katika mengi, tatizo pekee lilikuwa hili la kumwonea Mh. Mbowe. Sasa, Samia hili kalimaliza. Kama hili lilikiwa ndiyo kizingiti kikubwa, niendelee kumchukia Samia kwa kitu gani?

Cha muhimu kwa sasa, hoja ya Mbowe ya katiba mpya, ni hoja ya Watanzania walio wengi wanaoipenda Tanzania. Na hilo lilitamkwa wazi na ile Tume ya Jaji Warioba. Cha muhimu kwa sasa, ni Rais na Mh. Mbowe, kwa moyo wa umoja na uzalendo na mapenzi kwa Taifa letu, kuhakikisha tunafikia kupata katiba mpya bora bila ya misuguano, tukiruhusu utofauti wa mawazo, lakini mwishoni tukifikia maamuzi kwa njia za kidemokrasia.

Legacy ya Samia ipo kwenye kuipatia Tanzania Katiba Mpya.

Hongera Mbowe kwa sadaka uliyoitoa, na sadaka hii isiishie kwenye majuto bali katika faraja ya kukipata ulichokipigania kwa manufaa ya Taifa letu.
 
Back
Top Bottom