Katika kumuenzi Baba wa Taifa

Katika kumuenzi Baba wa Taifa

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
Suala la Siasa Safi Bado tunachechemea Sana Taifa Limekosa muelekeo sahihi wa siasa kana kwamba hakuna misingi ya siasa Ndani ya Taifa letu.

Huwezi kuzungumzia siasa Safi pasipo kuwepo Uongozi Bora ambao ni "Utawala Bora". Siasa iliyo safi ni matokeo ya misingi bora ya Uongozi na Uongozi ulio Bora ndio huzalisha wanasiasa Walio Safi.

Na kinyume chake siasa Safi ndio huunda Uongozi Bora. Kwa maana hii vitu hivi viwili ni mapacha wanaofanana katika misingi ya Taifa Bora.

Je nini kifanyike Kufikia siasa Safi haya yanaweza kuwa suluhisho;
Uongozi Bora ulio chini ya misingi ya Sheria na kanuni, mfumo wa kuwapata wanasiasa utokane na misingi ya Sayansi ya siasa na utumishi wa umma ikiwa taaluma inayo tolewa na vyuo mbalimbali hapa nchini.

Kuwepo na utaratibu unao wafunza Vijana kuwa wazalendo wa kweli wenye manufaa kwa Taifa sio Vyama vyao vya siasa Wala matumbo yao.
Kuwe na ulinzi mkali wa katiba na kanuni zote zinazoongoza utendaji wa serikali na Viongozi wake.

Siasa iwe sehemu ya weledi na isionekane Kama fursa ya watu Wenye njaa na hulka ya kuheshimiwa pasipo kutekeleza wajibu wao katika jamii.

Kuwe na utaratibu wa kuwawajibisha Viongozi kwa mujibu wa sheria pale ambapo wataenda kinyume na Maadili Yao ya uongozi. Siasa Safi inahitaji mambo mengi Sana ili kuifikia na hayo Ni machache Kati ya mengi.

Nyerere atabaki kukumbukwa sio tu kwa kuasisi mambo mazuri bali pia kuishi na misingi mibovu pasipo kuleta maumivu kwa watu wake.

Kwani hata yeye wakati wa uhai wake aliwahi kutamka wazi kuwa katiba yetu ina madhaifu mengi, iwapo atatokea kiongozi mbabe anaweza kuitumia atakavyo kwakua inampa madaraka makubwa.

Andiko la mwaka 2021 limefanyiwa nyongeza 2022.

Peter Mwaihola kitaaluma ni Mwandishi, Mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii.
 
Back
Top Bottom