Katika Kuboresha huduma za jamii....lazima wadau wakuu walazimishwe kutumia huduma za umma

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
865
Ndugu wanajukwaa!!!
Nimekuwa nikiwaza sana jinsi ambavyo utakuta afisa elimu wa ngazi mbalimbali akiwasomesha watoto wake shule za private wakati huku anasimamia na kuhamasisha shule za kata. Hii inahusu wadau wote wa huduma kama afya na mengine kwamba lazima sheria iwabane. Kama wewe ni waziri wa elimu ambapo ni msimamizi mkuu wa elimu ya public ingawa pia private ni lazima usomeshe watoto wako shule hizihizi so that upate kujua adha na kwahiyo utapambana kuzitatua.
Hii ni pamoja na mkuu wa nchi yetu na ikiwezekana watu wanaolenga nyadhifa mbalimbali moja ya kigezo cha kujua ni wenzetu basi wasome na watumie huduma zetu. sio wewe unatibiwa private wakati ni msimamizi mkuu wa afya tanzania.

lazima tuiweke kama sharti moja.. hawa makatibu wakuu pia tuwapime kama wanandugu zao katika elimu ya tanzania au wao wanasomesha majuu tu huku wakituharibia elimu yetu...

wakuu ni wazo langu naomba tuliboreshe...

Mandokwa Nangu
 
Back
Top Bottom