Katika hizi kauli mbili za Viongozi wetu wenye dhamana ni ya nani ipo sahihi na ipi imekengeuka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,425
120,772
" Namwomba huyo Msanii Ney wa Mitego atolewe huko Police na tena kama anaweza akaongeze baadhi ya mistari katika wimbo wake mzuri niliousikiliza wa WAPO kwani bado tuna matatizo mengi yanahitaji kuzungumzwa ili Jamii ijue na nchi isonge mbele ". Hii ilisemwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

" Tena natoa ONYO KALI kuwa kuanzia sasa hakuna na si ruhusa kwa Msanii yoyote yule nchini Tanzania kuimba nyimbo za Siasa bali waangalie maeneo na mambo mengine ya kuyaimba ili kuepusha uvunjifu wa amani wowote unoweza kujitokeza kwa kuimba Kwao Siasa " Hii ilisemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Nawasilisha na ama hakika ' This is Tanzania '.
 
Kauli ya Mkuu wa kaya ndo ya mwisho ila nilivyomuelewa mim waziri kama anawashauri tu kutokana na yaliyotokea,ni maoni yangu tu,
 
Huyu mwakiembe nadhani ana tatizo kubwa kuliko tunavyodhani!
Halafu sio mda tutawashuhudia hao wasanii kwenye mikutano ya ccm....trust me!
 
Na vipi nyimbo za mipasho amabazo zina maudhi kuliko za siasa....ie wembe ule ule nk.Napendekeza Mh. Waziri azipige marufuku kabisa.
 
Wizara yake inamatatizo mengi ya kushugurikia zaidi ya matamko yasio kuwa na maana..
Hivi tangu aingie hiyo wizara katatua tatizo gani ?
 
Nina uhakika Doctor hakusoma vizuri somo la Siasa wala hakusoma kabisa Historia ya Ukombozi katika mataifa mbalimbali.....

Angeelewa nafasi ya Muziki katika siasa za ukombozi.....

Angelewa pia Siasa maana yake ni nini na kwa tafsiri halisi ya Siasa, Siasa haina mtu maalum mwenye ruhusa ya kuizungumza na wengine wakaikosa....Katiba inatupa Uhuru wa kutoa maoni na hii ni kwa njia mbalimbali ikiwamo Sanaa mbalimbali kama Muziki, uchoraji n.k

Hawa PhD holders wengine wanatuweka mahali pagumu sana wasomi.......
 
Katatua tatizo la siku zote kutokwenda Gabon mpaka Kombe la Dunia.
 
yani utadhani ni kauli za watu wawili tafauti kumbe ni Dr. Mwakyembe amazitoa kauli mbili zinazokinzana kabisa.

wasomi wa hii nchi wanasababisha udokta na uprofesa uonekane ni ukichaa flani hivi.
 
Nina uhakika Doctor hakusoma vizuri somo la Siasa wala hakusoma kabisa Historia ya Ukombozi katika mataifa mbalimbali.....

Angeelewa nafasi ya Muziki katika siasa za ukombozi.....

Angelewa pia Siasa maana yake ni nini na kwa tafsiri halisi ya Siasa, Siasa haina mtu maalum mwenye ruhusa ya kuizungumza na wengine wakaikosa....Katiba inatupa Uhuru wa kutoa maoni na hii ni kwa njia mbalimbali ikiwamo Sanaa mbalimbali kama Muziki, uchoraji n.k

Hawa PhD holders wengine wanatuweka mahali pagumu sana wasomi.......

Mwenzako tokea zamani nimeshakataa na kupiga marufuku kuanzia katika Familia yangu, Kazini na kwingineko Watu kuniita ' Msomi ' kwani naogopa kuwa kama hopeless intellectuals tulionao sasa Tanzania ambao kutwa wanatutisha tu kwa ' titles ' zao ama Udaktari wa Falsafa au Uprofesa. Tena Mkuu ukitaka ' ugombane ' na Mimi Wewe niite Msomi nakuambia ' patachimbika ' hapo mubashara.
 
Acha uongo Msomiii...
 
" Namwomba huyo Msanii Ney wa Mitego atolewe huko Police na tena kama anaweza akaongeze baadhi ya mistari katika wimbo wake mzuri niliousikiliza wa WAPO kwani bado tuna matatizo mengi yanahitaji kuzungumzwa ili Jamii ijue na nchi isonge mbele ". Hii ilisemwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

" Tena natoa ONYO KALI kuwa kuanzia sasa hakuna na si ruhusa kwa Msanii yoyote yule nchini Tanzania kuimba nyimbo za Siasa bali waangalie maeneo na mambo mengine ya kuyaimba ili kuepusha uvunjifu wa amani wowote unoweza kujitokeza kwa kuimba Kwao Siasa " Hii ilisemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Nawasilisha na ama hakika ' This is Tanzania '.
Iwekwe humu sehemu ya hotuba aliyoitoa Waziri kisha ulinganishe na hayo maneno uliyomlisha.

Neno marufuku au onyo hakuna hata sehemu moja lilikotumika.

Alichokisema Waziri amewashauri vijana kuwa wanamuziki waliofanikiwa katika entertainment industry hakuna hata mmoja aliyewahi kupambana na utawala.

Dawa ya U.T.I acha kupotosha.
 
" Namwomba huyo Msanii Ney wa Mitego atolewe huko Police na tena kama anaweza akaongeze baadhi ya mistari katika wimbo wake mzuri niliousikiliza wa WAPO kwani bado tuna matatizo mengi yanahitaji kuzungumzwa ili Jamii ijue na nchi isonge mbele ". Hii ilisemwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

" Tena natoa ONYO KALI kuwa kuanzia sasa hakuna na si ruhusa kwa Msanii yoyote yule nchini Tanzania kuimba nyimbo za Siasa bali waangalie maeneo na mambo mengine ya kuyaimba ili kuepusha uvunjifu wa amani wowote unoweza kujitokeza kwa kuimba Kwao Siasa " Hii ilisemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Nawasilisha na ama hakika ' This is Tanzania '.
Mwakiyembe; kitaka kuoa hau kuolewa lazima huwe na cheti cha kuzaliwa.

Magufuli: ukitafuta cheti cha kuzaliwa utafanya watu wasioane, hivyo nimetengua agizo la waziri.

Magufuli: mwacheni huyo ney mwabieni aendelee kuimba tena aogeze na maneno yanayohusu ufisadi.

Mwakyembe: Ni marufuku msanii kuimba nyimbo zinazohusu siasa wakiendelea wataishia pabaya.

Hapo ngoma droo mwakyembe keshamjibu magufuli tayari, na malipo ni hapahapa duniani.
 
Back
Top Bottom