brave one
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 4,879
- 7,393
Leo tarehe 4 march kulikwa na mechi kati ya yanga vs jkt ruvu lakini tff kupitia bodi ya ligi kuu imeufuta mchezo huo na kuupeleka mbele mpaka tarehe 11 yaani jumatano ijayo, tarehe 8 yanga itacheza na simba siku 2 mbele itabidi wacheze na jkt ruvu siku 2 mbele tena itabidi wasafiri mpaka zimbambwe kucheza na platnums stars kombe la shirikisho yaani tff imewapa yanga siku 2 za maandalizi katika mechi ya kimataifa tena inayochezwa ugenini bora ingekuwa inachezwa nyumbani kusingeitaji maandalizi makubwa.
Kuna watu watasema mbona ulaya wanafanya ivo timu zinacheza ivo uefa lakini wote tunajua miundombinu ya mpira wa africa hujuma za kila namna kuanzaia usafiri timu inapowasili, hoteli, viwanja vya mazoezi na mambo kibao sasa kama mnaipa yanga siku mbili ya kufanya yote haya ni kweli tff ina nia ya dhati kusaidia timu zetu zifanye vizuri? Ikumbukwe yanga walicheza na BDF siku ya ijumaa iliyopita tarehe 27 walikuwa na siku 5 za mapumziko mpaka tarehe 4 ili wacheze na ruvu jkt, tff kulikuwa na ulazima gani kubadilisha ratiba? Na kubebesha yanga mzigo mkubwa usiokuwa na lazima? Kila siku timu zetu zinalalamika hujuma lakini muda mwingine tff inachangia kudhoofisha maendeleo ya mpira wetu, Rais wa Tff ndugu Jamal Malinzi mambo kama haya yanafanyika unakaa kimya au ndo aina ya mabadiliko uliokuwa unazungumzia?.
Yanga wanalalamikia mabadiliko haya ya ratiba tena bila kupewa taarifa mapema na kutishia kupeleka timu uwanja wa taifa leo, sasa izi vurugu tff mnazizalisha bila sababu ya msingi au mabadiliko haya ni kwa manufaa ya nani?