Katika hili, Star TV walipotoka

Katika hili, Star TV walipotoka

Ni vizuri vyama vya siasa vikawa na vyombo vyake vya habari. hii yakutegfemea mtu inachelewesha ukombozi wa kweli
Ni majuzi 2
ulifanyika mkutano wa CHADEMA katika viwanja vya sahara jijini mwanza,
katika taarifa ya vyombo vya habari ITV ilitoa habari yenye kichawa
"CHADEMA NA UMOJA WA WAMACHINGA JIJININI MWANZA WAMPA SIKU 14 WAZIRI
MAKUU KUMWONDOA MKURUGENZI WA JIJI HILO BWANA BWANA KABWE KWA KUMTUHUMU
KUWA CHANZO CHA MIGOGORO" katika taarifa yao, ITV walimwonyesha mbunge
wa nyamagana wenjeakisoma barua kwa niaba ya wamachinga.

Kwa upande mwingine STAR TV, kichwa cha habari kilikuwa "SERKALI
YAHIMIZWA KUSIMAMIA RASILIMALI VIZURI KWA MANUFAA YA UMMA" na
wakawonyesha viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutanoa
huo.

sikuridhika na kichwa cha habari cha STAR TV, hata kama sio mtaalamu wa
uandishi wa habari, kwa sababu moja kubwa kwamba usimamizi bora wa
rasilimali za nchi na serikali umezungumzwa sana tena sana, hivyo kuwa
na kichwa cha habari cha namna kama ile si kutuletea habari kwa ni
habari iliyo kufa tayari, hivyo nikapenda ile ya ITV kwangu ilikuwa ni
habari.

Pili, likanijia wazo kuwa STAR TV, inamilikiwa na kada na mwenyekiti wa
CCM mkoa bwana Diallo na CCM na wakurugenzi ktka nchi hii huwezi
kuwatofautisha hivyo STAR TV wasingependa kutoa habari inayomwangusha
mwajiri wao.

Jana ndo nikawagundua jamaa hawa wa STAR TV kuwa wanamlengo wa kisiasa
wa upande wa CCM pale walipoleta habari inayoonyesha viongozi wa
wamachinga wa mwanza wakimtuhumu Wenje kughushi barua, na
kuwachonganisha na serikali na wakamtaka wenje aombe radhi ndani ya siku
14, na hapo STAR TV wakalazimika kuonyesha kipande cha ile habari
ambacho kinamuonyesha wenye akisoma barua ya wamachinga.

Hata hao wamachinga kama ile barua si ya kweli lakini kwa yeyote
anayeishi mwanza mwenye kutumia akili yake vizuri anafahamu jinsi
mkurugenzi huyu anavyolalamikiwa na wanachi kama mtu mwenye kiburi cha
madaraka, fisadi (reje mgogoro wake na mwananchi mmoja wa luchelele kwa
madai kuwa kavamia kiwanja chake), soko la mwaloni, ni mtu mwenye kutaka
kuibeba CCM muda wote na mengine mengi, hivyo kwangu nikisikia watu
hawamtaki sitashangaa kwani hapa mwanza yamekuwa yakiongelewa kwa muda
mrefu sna.

Binafsi ningependa kuwaasa/kuwaomba STAR Tv, kwangu kimekuwa ni kituo
changu cha kwanza cha habari kwa muda mrefu, then Channel 10, ITV, na
mwisho TBCCM, hivyo wasiharibu sifa nzuri waliojijengea kwa jamii kwa
kukubari kutumika.
 
Kila chombo cha habari kina 'internal ideologue' ndio maana unaweza kutofautisha gazeti la UHURU, TAZAMA, JAMBO LEO na TANZANIA DAIMA, MWANAHALISI, RAIA MWEMA nk. Tusiwalaumu Star TV. Jambo jema ni kuwa uwanja ni mpana ukiona chombo fulani kinamwelekeo fulani uanageukia upande mwingine. Ndio maana kuna watu wameshasahau kuwa bado kuna magazeti ya UHURU na MZALENDO lakini huko nyuma tulikuwa hatuna uchaguzi lazima uyasome hayo labda ukikwepa utasoma MFANYAKAZI (halipo sasa). Na wengine wameshasahau kama kuna redio inaitwa TBC (zamani RTD) wengi huikumbuka inapotangaza mpira wa Simba na Yanga. Waacheni watasahaulika taratibu!
 
Si hivyo tu, jana Star Tv wamezuiliwa na boss wao, Diallo kurusha hewani Live uzinduzi wa M4C kanda ya ziwa toka gold crest hotel- mwanza kinyume na makubaliano ya awali.
 
tv ya ccm sasa unashangaa nini
Ni majuzi 2 ulifanyika mkutano wa CHADEMA katika viwanja vya sahara jijini mwanza, katika taarifa ya vyombo vya habari ITV ilitoa habari yenye kichawa "CHADEMA NA UMOJA WA WAMACHINGA JIJININI MWANZA WAMPA SIKU 14 WAZIRI MAKUU KUMWONDOA MKURUGENZI WA JIJI HILO BWANA BWANA KABWE KWA KUMTUHUMU KUWA CHANZO CHA MIGOGORO" katika taarifa yao, ITV walimwonyesha mbunge wa nyamagana wenjeakisoma barua kwa niaba ya wamachinga.

Kwa upande mwingine STAR TV, kichwa cha habari kilikuwa "SERKALI YAHIMIZWA KUSIMAMIA RASILIMALI VIZURI KWA MANUFAA YA UMMA" na wakawonyesha viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliokuwa kwenye mkutanoa huo.

sikuridhika na kichwa cha habari cha STAR TV, hata kama sio mtaalamu wa uandishi wa habari, kwa sababu moja kubwa kwamba usimamizi bora wa rasilimali za nchi na serikali umezungumzwa sana tena sana, hivyo kuwa na kichwa cha habari cha namna kama ile si kutuletea habari kwa ni habari iliyo kufa tayari, hivyo nikapenda ile ya ITV kwangu ilikuwa ni habari.

Pili, likanijia wazo kuwa STAR TV, inamilikiwa na kada na mwenyekiti wa CCM mkoa bwana Diallo na CCM na wakurugenzi ktka nchi hii huwezi kuwatofautisha hivyo STAR TV wasingependa kutoa habari inayomwangusha mwajiri wao.

Jana ndo nikawagundua jamaa hawa wa STAR TV kuwa wanamlengo wa kisiasa wa upande wa CCM pale walipoleta habari inayoonyesha viongozi wa wamachinga wa mwanza wakimtuhumu Wenje kughushi barua, na kuwachonganisha na serikali na wakamtaka wenje aombe radhi ndani ya siku 14, na hapo STAR TV wakalazimika kuonyesha kipande cha ile habari ambacho kinamuonyesha wenye akisoma barua ya wamachinga.

Hata hao wamachinga kama ile barua si ya kweli lakini kwa yeyote anayeishi mwanza mwenye kutumia akili yake vizuri anafahamu jinsi mkurugenzi huyu anavyolalamikiwa na wanachi kama mtu mwenye kiburi cha madaraka, fisadi (reje mgogoro wake na mwananchi mmoja wa luchelele kwa madai kuwa kavamia kiwanja chake), soko la mwaloni, ni mtu mwenye kutaka kuibeba CCM muda wote na mengine mengi, hivyo kwangu nikisikia watu hawamtaki sitashangaa kwani hapa mwanza yamekuwa yakiongelewa kwa muda mrefu sna.

Binafsi ningependa kuwaasa/kuwaomba STAR Tv, kwangu kimekuwa ni kituo changu cha kwanza cha habari kwa muda mrefu, then Channel 10, ITV, na mwisho TBCCM, hivyo wasiharibu sifa nzuri waliojijengea kwa jamii kwa kukubari kutumika.
 
Wanao fikili kimas......i ni nyinyi cdm kila kitu mnata upendeleo hamna hata aibu, vyombo ya kuanzia simnavyo vile vya disco au yale mafuso yenu si yanatosha kabisa? Au mchaga kaisha weka stoo maana hakawii kusema anawadai!
 
Wanao fikili kimas......i ni nyinyi cdm kila kitu mnata upendeleo hamna hata aibu, vyombo ya kuanzia simnavyo vile vya disco au yale mafuso yenu si yanatosha kabisa? Au mchaga kaisha weka stoo maana hakawii kusema anawadai!

Hehehe swadaktaa jamaa wanazogo hawa sasa mbona kuna vyama hata kuoneshwa havioneshwi wala hawalalamiki hichi chama kweli cha promo wanapenda kuuza sura
 
Yap, ni kweli Star tv ina mapungufu mengi kwa sasa, hasa baada ya mzee kupewa cheo. Anyway hatusemi wapendelee watu flan, kinachotakiwa ni kuwa fair kama mwanzo, yan kuanzia pale Dialo alipoanguka mpaka juz juz alipopata uenyekiti mkoa. KWENYE MADA; Hamkutangaza habar husika siku ya tukio, lakin baada ya viongoz kumpinga Wenje ndo mnatoa habar zote, hiyo ni aibu kwa kituo kama hiki, mana kama alichosema Wenje haikuwa habar kwenu, iweje waliompinga iwe ndo habari.
 
Wakati ITV na Channel ten wanasonga mbele katika kutoa habari za uhakika na mijadala huru ya kisiasa na kijamii, Star TV na TBC zinakufa taratibu kwa kueneza propaganda chafu za kupotosha umma.

Lakini kwa kuwa watanzania wanauelewa mpana kwa sasa, wanajua mbichi na mbivu, Kwa mwendo huu TBC na Star TV vitakufa taratibu(Natural Death).

TBC haiwezi kufa, hujui inaendeshwa kwa kodi yako???
 
Information is power so Suluhisho la kudumu ni CDM kuwa na Radio plus TV ...Otherwise tutaendelea kupotoshwa, kunyimwa taarifa sahihi...Sijui kwanini CDM hawalioni hili...
 
Chadema, hivi ni kweli hamuwezi kuanzisha tv yenu? star tv, itv, chanel ten zote ni mali za makada wa ccm.
 
Hii star Tv tangia Dialo awe Mwenyekiti wa CCM mkoa, wamebadilika sana, ni tofauti na mwanzo kabla hajaawa, Mimi nashauri Viongozi wa CHADEMA wafikilie kuanzisha TV na Redia Mapema sana, tuko tiyali kuchanga hata sent tano ilimuradi iwe hivyo,

Hizi TV mbili Stare TV na TBC kwa sasa sio kabisa, kidogo imebakia ITV na Chanel Ten,
mkuu umesema vema viongozi wa cdm naona wamejisahau na wanategemea media za magamba kama star tv.badala ya kuanzisha vya kwao!
 
Wanao fikili kimas......i ni nyinyi cdm kila kitu mnata upendeleo hamna hata aibu, vyombo ya kuanzia simnavyo vile vya disco au yale mafuso yenu si yanatosha kabisa? Au mchaga kaisha weka stoo maana hakawii kusema anawadai!
Kila binadamu kapewa ubongo wake
 
Star T.V. wangetusaidia kwa kuhoji upande wa pili ili Wenje akiri au akanushe taarifa hiyo kabla ya wana JF hatujachangia hapa jamvini.
 
Makamanda msile lie kama demu aliyebanwa gheto, hebu anzisheni basi hata karedio watu tuskie sumu zenu lakin sio kulalamika daily na kuomba huruma humu kama watoto, hivi maela yote ya M4C mmeshindwa hata kuanzisha kagazeti ka kurasa 1 tu au ndo kusema ubahiri au zile fedha mumempa yule mnafiki Zitto akale xmas uswisi mwezi huu..

Chadema acheni kulilia na kutafuta huruma kama demu.
Heh!Huyu naye ametoka wapi?
 
Anzisha yenu kwenye ule ukumbi wa disco wa mh. Mbowe

Wewe ndo vijana wa katibu mkuu mpya nini hapa jamvini maana kasi yako siyo mbaya sana? Naona kazi nzuri posho utakayopokea leo kweli utakuwa umeifanyia kazi! Keep it up ila hutaweza kubadilisha waliobadilika na wala kutaweza kuzuia kubadilika wanaotaka mabadiliko. Timiza wajibu wako ukapate posho yako mkuu!
 
Si hivyo tu, jana Star Tv wamezuiliwa na boss wao, Diallo kurusha hewani Live uzinduzi wa M4C kanda ya ziwa toka gold crest hotel- mwanza kinyume na makubaliano ya awali.

Watanzania bwana, Dialo baada ya kusota nje ya system kwa muda kupewa mwenyekiti wa nyinyiemu basi sasa anataka kuharibu na biashara yake tena kwa ajili tu ya chama! Wafanyabiashara wetu siku ccm inaingia kaburini na biashara zao zitaisindikiza ccm maana sidhani kama kunamfanyabiashara aliye kada wa ccm biashara yake itapona.
Hakuna TV iliyokuwa na taarifa ya habari nzuri kama starTV lakini kuanzia siku chache hata watangazaji naona hawana motisha tena maana naona anakuwepo sijui mtangazaji mmoja tu siku hizi kwa taarifa nzima. TV hii itapoteza watangaz;I wazuri lazima maana naamini mtu kama Angero Mwoleka sidhani kama atakubali kutetea ccm wakati amekuwa akiiponda siku zote!

Kuna mtangazaji mmoja wa StarTV ni member humu labda atajitokeza kujibu!
 
Back
Top Bottom