Hebu angalia gharama hizi za huu muamala hapa chini
👉Gharama ya muamala(kodi) = 3500/=
👉Tozo ya mshikamano = 7500/=
Hii uliona wapi? Hata kama ni uzalendo huu sasa ni unyanyasaji, hata kama ni mshikamano huu sasa ni mshikwamano. Yani tozo ambayo kiuhalisia ilipaswa iwe hiari inakuwa mara 2 ya kodi ya muamala husika?
Katika uhalisia tuu wa maisha, hata kwa ambaye hajasoma uchumi, angeambiwa apendekeze tozo ya mshikamano basi angependekeza japo nusu ama robo ya kodi husika kwenye kila muamala. Kwanza nusu ni kubwa sana, angeanzia kwenye robo na kurudi chini.
Mfano kama kodi ya muamala husika ni 4000/= basi nusu ni 2000/= na robo ni 1000/=. Kama tozo ya mshikamano ni robo ya kodi ya muamala husika basi jumla ya makato ingepanda kutoka 4000/= mpaka 5000/=. Hii tozo ingekuwa himilivu na isingeleta shida sana.
Lakini eti tozo ya mshikamano inakuwa mara 2 ya kodi ya muamala husika? Hii hata mjinga ambaye hajaenda hata darasa la kwanza asingethubutu kupendekeza aina hii ya tozo. Asingethubutu hata kidogo.
Ina maana serikali hapa ilitaka itengeneze faida mara 2 ya makampuni husika? Ama lengo lao ni nini hasa? Yani kodi nilipe 3500/= kisha tozo ya mshikamano nilipe 7500/=? Like seriously? Yani tozo ni mara 2 ya kodi ya muamala husika? Aisee Mwigulu hauwezi kuwa serious hata kidogo.
Ningekuwa mimi ndio waziri niliyeleta hii kanuni na basi ningeshaachia ngazi mapema sana, maana hapa ni zaidi ya kuboronga.