Katika hili la Wamachinga Mheshimiwa Rais utanisamehe sijazoea unafiki!

magu ni mjanja sana ! uwongozi wake ni wakutafuta kiki kilazima yaan utake usitake lazima umkubali ! inshort anakitendea haki cheo chake
 
kutokana na tamko la jana tu kutoka kwa muheshimiwa Raisi kuwa Machinga wasibugudhiwe, leo hii hapa mkoani kwetu kanda ya Kaskazini hapatoshi, yaani tunaendesha magari juu ya bidhaa za hawa jamaa, kwanza ni wabishi hata unasubutu kumuomba wasogeze bidhaa zao yaani wanakuangalia kama nyaya mbichi!
 
Mimi kwa kweli namuunga mkono, ni wakati wa mlala hoi nae kufurahia nchi yake. Miongo mingi iliyopita matajiri ndio waliofaidi keki ya taifa.
Kutesa kwa zamu.
Issue Mkuu hawa watu wamesamehewa hadi Kodi wenye biashara halali watauzaje? wengine wanauza kama mini super market!! Ila barabarani? Je wapewe efd machine pia? nchi itajiendesha na kodi ya wafanyakazi tu ya mshahara? Hebu kwanza watupe makusanyo ya Novemba ili tujue kama tunaweza kusimama bila mchango wa machinga hawa kwani wanatakiwa na wao walipe kodi
 
kutokana na tamko la jana tu kutoka kwa muheshimiwa Raisi kuwa Machinga wasibugudhiwe, leo hii hapa mkoani kwetu kanda ya Kaskazini hapatoshi, yaani tunaendesha magari juu ya bidhaa za hawa jamaa, kwanza ni wabishi hata unasubutu kumuomba wasogeze bidhaa zao yaani wanakuangalia kama nyaya mbichi!
By the way walishauwa mwendesha gari pale kariakoo alikanyaga nyanya kwenye Dart Road ya pembeni!! Halafu ubungo junction wamerudi kwa fujo na palikuwa pametulia kwa mbali
 
Mtoa Mada ni mchawi naomba narudie tena ni mchawi, maana haiwezekani Kama mzazi ameamua ugomvi useme kakosea kuamua eti ulimzaa unaona!! Hivi baya ni machinga kuondolewa au Mhe Rais kuzuia machinga kuondolewa? Binadamu bwana hana kiangazi wala masika
We ndo mchawi huelew A wala B,soma vizur uwelewe,ukweli hakuna mawasiliano mazuri kati ya mkuu wa mkoa na mkuu wake
 
Maeneo ya Magogoni ni maeneo mazuri kwa machinga maana limezungukwa na ofisi nyingi za serikali pia kuna chuo cha utumishi wa umma sina uhakika wamachinga wataruhusiwa kufanya biashara maeneo hayo
Kwa katazo lililotolewa wamachinga ni kuangalia penye fursa!! Naimagine after a week hali itakuwaje?
 
Nianze tu kwanza kwa kukupongeza kwa kujitokeza jana ukiwa na Makamu wako kuweza kulizungumzia na kulitatua kwa muda tu tatizo la Wafanyabiashara wadogo wadogo waitwao Wamachinga juu ya hatima yao ya kufanya biashara ILA kuna mambo ambayo bila kukuficha nitapingana na Wewe bila aibu wala unafiki kwa hoja zangu zitakazokuja mbele.

  • Mheshimiwa Rais kila Mtu anajua kuwa Wewe ndiyo umewateua hawa Wakuu wa Mikoa, wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo nchi nzima ili wafanye Kazi kwa niaba yako na ni kitu cha wazi tu kuwa hata hayo wanayoyafanya pengine yana baraka au maelekezo yako sasa iweje tena jana ' ukapovuka ' vile hadi kuonyesha kuwa hawa Watendaji wako ' wateule ' walikurupuka?

  • Mheshimiwa Rais nikikumbuka ile ' kauli ' yako ambayo uliitoa pale katika Viwanja vya ' Furahisha ' tena ukiwa ' umefura ' kabisa ulimtaka huyu huyu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na hawa hawa ' Watendaji ' wako kuhakikisha kuwa hawa ' Wamachinga ' uliowatetea jana ' waondolewe ' mara moja kwani walikuwa wanasababisha na kuleta ' usumbufu ' mkubwa pale Mwanza mjini halafu nilipokuona jana ukiwa tena ' umefura ' kwa ' kuwatetea ' hao ' Wamachinga ' na kuwalaumu ' Watendaji ' wako ambao Wewe mwenyewe uliwapa ' maelekezo ' nimeshangaa mno.

  • Mheshimiwa Rais jana nimekusikia vizuri sana ' ukitiririka ' mbele ya uliokuwa nao hapo ' Ikulu ' kwa kusema kuwa usingependa kuona hawa ' Wamachinga ' wakionewa kwakuwa ' wao ' narudia tena kwa kusisitiza ulisema kwa kuwa ' wao ' ndiyo waliokupigia ' Kura ' na kukuweka ' madarakani ' mwaka jana. Naomba kukuuliza je Mheshimiwa Rais ina maana unataka kusema kuwa kama hawa ' Wamachinga ' wasingekupigia hizo ' Kura ' zilizokuweka ' madarakani ' hapo ungekubali waondolewe na ungeridhika na hiyo hatua?

  • Mheshimiwa Rais kwa ' maelezo ' yako ya jana ya kuonyesha kuwapigani hawa ' Wamachinga ' na ustawi wao wa ' kimaisha ' ndiyo unataka kusema kuwa sasa utakuwa ' unawakumbatia ' Wamachinga hawa kwakuwa ni wapiga ' kura ' wako ili mwaka 2020 wakuweke tena ' madarakani ' hivyo uko radhi kuwaona wakivunja ' sheria ' na taratibu zilizopo na ambazo zinatakiwa zifuatwe na kila Mtanzania bila kujali yeye ni nani?

  • Mheshimiwa Rais nadhani jana baada tu ya kutoa lile ' tamko ' lako ' tetezi ' kwa wapiga ' kura ' wako pekee na waaminifu Tanzania nzima waitwao ' Wamachinga ' uliona jinsi ambavyo walifurahi na pale pale wakaanza kuonyesha ' jeuri ' yao kwa kuanza kujichukulia hatua wao kama wao pasipo hata kufuata ' taratibu ' ambapo wengi wao walianza ' kujichorea ' vizinga pembezoni mwa barabara na ' kuta ' za Nyumba za ' Watu ' kitu ambacho kwa ' jicho ' langu la ' tatu ' nililobarikiwa nalo na Mwenyezi Mungu naona ' mtafaruku ' na ' uhasama ' mkubwa wa ' Kimaslahi ' unakuja kati ya hawa Wapiga ' kura ' wako ' waaminifu ' Wamachinga na wenye maeneo yao na Wafanyabiashara ' wakubwa ' na ambao pengine ndiyo wanalipa ' Kodi ' nyingi ambazo zinasaidia kwa namna moja au nyingine kuendesha ' Uchumi ' wa nchi hii.

  • Mheshimiwa Rais nina ' uhakika ' usio na ' shaka ' kabisa kuwa kwa ' tamko ' lako lile la jana utakuwa umewapa ' kiburi ' na ' jeuri ' ya ' kutukuka ' kabisa hawa wapiga ' kura ' wako ' waaminifu ' Wamachinga kote nchini na sasa wanaweza wakawa wanajifanyia ' wanavyotaka ' kwa ' kigezo ' kuwa Wewe ' mtetezi ' wao upo na pia kwa kauli yako ile sitoshangaa sasa kuona ' Vijana ' wakijichanga kukimbia kutoka ' vijijini ' na kuja ' mijini ' ili kufanya ' umachinga ' kwani tayari umeshawaonyesha njia nzuri jana je upo tayari pia kupokea ' misururu ' ya ' migogoro ' Ofisini Kwako?

  • Mheshimiwa Rais hili ' sakata ' la hawa ' Wamachinga ' lilianza nadhani tokea ' wikiendi ' iliyoisha hadi hawa ' Wafanyabiashara ' kuanza ' kuvunjiwa ' vibanda vyao huku wengine wakinyanyaswa na bahati nzuri sana karibu ' media outlets ' zote nchini Tanzania zilifanya ' coverage ' ya kutosha juu yake ila hukutokea na binafsi nimeshangaa sana kukuona jana ndiyo ' umejitokeza ' vile ' kuwatetea ' wakati tayari wameshaingia ' hasara ' kubwa. Je Mheshimiwa Rais huoni kwamba pengine hili ' tamko ' lako la jana ungelitoa tu siku ile ile ya mwanzo lingesaidia sana kuliko kusubiri ' Wamachinga ' wafukuzwe, wavunjiwe vibanda vyao ndipo ' ujitokeze ' kuwatetea na kuwapigania tena kwa ' kigezo ' cha kusema kuwa ndiyo wapiga ' kura ' wako?

HITIMISHO LANGU LA KIUSHARI KWAKO.

Mheshimiwa Rais ni ukweli usiopingika kuwa kwa huu mwaka mmoja tu wa ' Uongozi ' wako umeweza kufanya ' mambo ' mengi makubwa na mazuri ambayo nadhani kila Mtanzania ameridhika na kufurahishwa nayo kwani umeweza ' kuthubutu ' na ' tunakupongeza ' sana kwa hilo na tunakuomba zidisha bidii ILA nadhani pia kuna ' tatizo ' dogo mno ama kutoka kwako kuwa pengine labda hupendi ' ushauri ' kutoka kwa ' Wasaidizi ' wako au hao hao ' Wasaidizi ' wako wanakuogopa labda kwa haiba yako ya ' ukali ' ambayo nakushauri ' ipunguze ' kidogo kwani hata Role Model wako Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ' mkali ' ila tofauti yake na yako Mwalimu alikuwa ana heshimu sana ' ushauri ' kutoka kwa ' wasaidizi ' wake huku akiwa anawaamini pia.

Kama jana umeweza kuwasema Viongozi wako uliowateua mwenyewe wa Mkoa wa Mwanza kwa ' utendaji ' wao ambao umekuudhi basi naomba huo ' ukali ' wako usiishie tu kwa huyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Watendaji wake bali uende pia kwa Wakuu wa Mikoa wengine na Watendaji wao ambao na wao katika hiyo Mikoa yao wanafanya mambo ya ' ajabu ' na ya ' hovyo hovyo ' Kiutendaji tena kushinda hata hao wa Mwanza huku wengine sasa wakitaka hata kuonekana kama ni ' Miungu ' watu na ' Wafalme '.

Wajengee ' kujiamini ' sana Watendaji wako hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kwani kwa ' utafiti ' wangu mdogo tu wengi wao hawafanyi ' Kazi ' za Kimaendeleo hasa huko walipo na badala yake wanafanya Kazi ili tu kuweza ' kukuridhisha ' Wewe na ' usiwatumbue kitu ambacho hakina ' afya ' wala ' tija ' katika administrative / management perfomance na mwisho uwe unazisikiliza sana ' taarifa ' muhimu unazopewa kwani nimegundua kuwa ' tatizo ' kubwa la ' kimawasiliano ' ambalo pengine linakupelekea ' kujichanganya ' sana katika ' maelezo ' / ' matamko ' yako.

Naomba niishie hapa na narudia tena kusema kwa hili la jana la Wamachinga sijakubaliana na Wewe na bado kunatakiwa kuwa na ' mjadala ' mpana juu ya uwepo wao na ufanyakazi biashara wao na siku zote ' Siasa ' zisitupeleke ' kubaya ' hadi tukaonekana ' vituko ' mbele ya macho ya wenye ' akili ' na ' upeo ' wa ' kutukuka ' ILA nisikufiche ' tamko ' lako la jana lina ' utata ' mwingi na ' limejichanganya ' mno na wengine ' likituduwaza '.

Nikutakie tu kila la kheri na ' majukumu ' mema Mheshimiwa Rais wangu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ILA utanisamehe tu kuwa sijazoea wala kufundishwa kuwa ' mnafiki ' mbele ya ' ukweli ' au ' mtazamo ' ninaouona.

Who are you? Leave our President alone! Shut up!
 
Labda kwa sababu hapititagi mtaani ajionee chinga wanavyopanga bidhaa bararani halafu itokee bahati mbaya ukanyage hiyo biashara yake uone huo ugomvi utakaotokea.
 
Tunapandikiza chuki isiyo na maana tuu kwa machinga na mkuu wa mkoa na wilaya....viongoz poleni kwa maana hii aibu

Tusubir akija hiyo next week atasema nn
wamwachie kila kitu afanye yeye. ikibidi wawaruhusu machinga kuweka bidhaa zao kila jingo ili aridhike kuwa Nchi hii yeye ndio kila kitu.
 
Mie nilifurahia Mama Samia alivyo na nidhamu kwa Boss wake, yeye wakati wote alikuwa anaitikia "ndio" au "sawa mkuu" ....wasiwasi wangu ni kwamba angeweza kujibu sawa tu mahali ambapo alitakiwa aseme..."hiyo hapana"!
 
anacho zungumza mtoa mada ni ukurupukaji uliotumika katika kutoa maagizo ya jana ilhali huko nyuma alishatoa maagizo kinzani na haya ya jana.Halafu rungu linawaangukia watendaji kwa kufuata maagizo. Wewe jiweke katika hivyo viatu mkuu acha ushabiki wa kiitikadi.Hapa kinachofanyika ni kujaribu kuwafurahisha kundi ambalo limekuwa linasababisha "mayhem" katika majiji yetu kwa kukosa kutii japo kutopanga bidhaa katika barabara za watembea kwa miguu.Ni hawahawa ndio walioua mtu kwasababu aligonga bidhaa za mmoja wao kwa bahati mbaya ilhali ni wao ndio wanaopanga barabarani.Wao ni mabigwa wa kujichukulia shera mikononi. Mimi ninawaheshimu na kuwapenda sana lakini kwanini wasitengewe maeneo tengefu ndani ya jiji au katika vituo vikubwa vya mabasi iliwaondoe hii adha mabarabarani na nje ya nyumba/maduka ya watu watanzania wengine?
 
Nianze tu kwanza kwa kukupongeza kwa kujitokeza jana ukiwa na Makamu wako kuweza kulizungumzia na kulitatua kwa muda tu tatizo la Wafanyabiashara wadogo wadogo waitwao Wamachinga juu ya hatima yao ya kufanya biashara ILA kuna mambo ambayo bila kukuficha nitapingana na Wewe bila aibu wala unafiki kwa hoja zangu zitakazokuja mbele.

  • Mheshimiwa Rais kila Mtu anajua kuwa Wewe ndiyo umewateua hawa Wakuu wa Mikoa, wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo nchi nzima ili wafanye Kazi kwa niaba yako na ni kitu cha wazi tu kuwa hata hayo wanayoyafanya pengine yana baraka au maelekezo yako sasa iweje tena jana ' ukapovuka ' vile hadi kuonyesha kuwa hawa Watendaji wako ' wateule ' walikurupuka?

  • Mheshimiwa Rais nikikumbuka ile ' kauli ' yako ambayo uliitoa pale katika Viwanja vya ' Furahisha ' tena ukiwa ' umefura ' kabisa ulimtaka huyu huyu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na hawa hawa ' Watendaji ' wako kuhakikisha kuwa hawa ' Wamachinga ' uliowatetea jana ' waondolewe ' mara moja kwani walikuwa wanasababisha na kuleta ' usumbufu ' mkubwa pale Mwanza mjini halafu nilipokuona jana ukiwa tena ' umefura ' kwa ' kuwatetea ' hao ' Wamachinga ' na kuwalaumu ' Watendaji ' wako ambao Wewe mwenyewe uliwapa ' maelekezo ' nimeshangaa mno.

  • Mheshimiwa Rais jana nimekusikia vizuri sana ' ukitiririka ' mbele ya uliokuwa nao hapo ' Ikulu ' kwa kusema kuwa usingependa kuona hawa ' Wamachinga ' wakionewa kwakuwa ' wao ' narudia tena kwa kusisitiza ulisema kwa kuwa ' wao ' ndiyo waliokupigia ' Kura ' na kukuweka ' madarakani ' mwaka jana. Naomba kukuuliza je Mheshimiwa Rais ina maana unataka kusema kuwa kama hawa ' Wamachinga ' wasingekupigia hizo ' Kura ' zilizokuweka ' madarakani ' hapo ungekubali waondolewe na ungeridhika na hiyo hatua?

  • Mheshimiwa Rais kwa ' maelezo ' yako ya jana ya kuonyesha kuwapigani hawa ' Wamachinga ' na ustawi wao wa ' kimaisha ' ndiyo unataka kusema kuwa sasa utakuwa ' unawakumbatia ' Wamachinga hawa kwakuwa ni wapiga ' kura ' wako ili mwaka 2020 wakuweke tena ' madarakani ' hivyo uko radhi kuwaona wakivunja ' sheria ' na taratibu zilizopo na ambazo zinatakiwa zifuatwe na kila Mtanzania bila kujali yeye ni nani?

  • Mheshimiwa Rais nadhani jana baada tu ya kutoa lile ' tamko ' lako ' tetezi ' kwa wapiga ' kura ' wako pekee na waaminifu Tanzania nzima waitwao ' Wamachinga ' uliona jinsi ambavyo walifurahi na pale pale wakaanza kuonyesha ' jeuri ' yao kwa kuanza kujichukulia hatua wao kama wao pasipo hata kufuata ' taratibu ' ambapo wengi wao walianza ' kujichorea ' vizinga pembezoni mwa barabara na ' kuta ' za Nyumba za ' Watu ' kitu ambacho kwa ' jicho ' langu la ' tatu ' nililobarikiwa nalo na Mwenyezi Mungu naona ' mtafaruku ' na ' uhasama ' mkubwa wa ' Kimaslahi ' unakuja kati ya hawa Wapiga ' kura ' wako ' waaminifu ' Wamachinga na wenye maeneo yao na Wafanyabiashara ' wakubwa ' na ambao pengine ndiyo wanalipa ' Kodi ' nyingi ambazo zinasaidia kwa namna moja au nyingine kuendesha ' Uchumi ' wa nchi hii.

  • Mheshimiwa Rais nina ' uhakika ' usio na ' shaka ' kabisa kuwa kwa ' tamko ' lako lile la jana utakuwa umewapa ' kiburi ' na ' jeuri ' ya ' kutukuka ' kabisa hawa wapiga ' kura ' wako ' waaminifu ' Wamachinga kote nchini na sasa wanaweza wakawa wanajifanyia ' wanavyotaka ' kwa ' kigezo ' kuwa Wewe ' mtetezi ' wao upo na pia kwa kauli yako ile sitoshangaa sasa kuona ' Vijana ' wakijichanga kukimbia kutoka ' vijijini ' na kuja ' mijini ' ili kufanya ' umachinga ' kwani tayari umeshawaonyesha njia nzuri jana je upo tayari pia kupokea ' misururu ' ya ' migogoro ' Ofisini Kwako?

  • Mheshimiwa Rais hili ' sakata ' la hawa ' Wamachinga ' lilianza nadhani tokea ' wikiendi ' iliyoisha hadi hawa ' Wafanyabiashara ' kuanza ' kuvunjiwa ' vibanda vyao huku wengine wakinyanyaswa na bahati nzuri sana karibu ' media outlets ' zote nchini Tanzania zilifanya ' coverage ' ya kutosha juu yake ila hukutokea na binafsi nimeshangaa sana kukuona jana ndiyo ' umejitokeza ' vile ' kuwatetea ' wakati tayari wameshaingia ' hasara ' kubwa. Je Mheshimiwa Rais huoni kwamba pengine hili ' tamko ' lako la jana ungelitoa tu siku ile ile ya mwanzo lingesaidia sana kuliko kusubiri ' Wamachinga ' wafukuzwe, wavunjiwe vibanda vyao ndipo ' ujitokeze ' kuwatetea na kuwapigania tena kwa ' kigezo ' cha kusema kuwa ndiyo wapiga ' kura ' wako?

HITIMISHO LANGU LA KIUSHARI KWAKO.

Mheshimiwa Rais ni ukweli usiopingika kuwa kwa huu mwaka mmoja tu wa ' Uongozi ' wako umeweza kufanya ' mambo ' mengi makubwa na mazuri ambayo nadhani kila Mtanzania ameridhika na kufurahishwa nayo kwani umeweza ' kuthubutu ' na ' tunakupongeza ' sana kwa hilo na tunakuomba zidisha bidii ILA nadhani pia kuna ' tatizo ' dogo mno ama kutoka kwako kuwa pengine labda hupendi ' ushauri ' kutoka kwa ' Wasaidizi ' wako au hao hao ' Wasaidizi ' wako wanakuogopa labda kwa haiba yako ya ' ukali ' ambayo nakushauri ' ipunguze ' kidogo kwani hata Role Model wako Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ' mkali ' ila tofauti yake na yako Mwalimu alikuwa ana heshimu sana ' ushauri ' kutoka kwa ' wasaidizi ' wake huku akiwa anawaamini pia.

Kama jana umeweza kuwasema Viongozi wako uliowateua mwenyewe wa Mkoa wa Mwanza kwa ' utendaji ' wao ambao umekuudhi basi naomba huo ' ukali ' wako usiishie tu kwa huyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Watendaji wake bali uende pia kwa Wakuu wa Mikoa wengine na Watendaji wao ambao na wao katika hiyo Mikoa yao wanafanya mambo ya ' ajabu ' na ya ' hovyo hovyo ' Kiutendaji tena kushinda hata hao wa Mwanza huku wengine sasa wakitaka hata kuonekana kama ni ' Miungu ' watu na ' Wafalme '.

Wajengee ' kujiamini ' sana Watendaji wako hasa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kwani kwa ' utafiti ' wangu mdogo tu wengi wao hawafanyi ' Kazi ' za Kimaendeleo hasa huko walipo na badala yake wanafanya Kazi ili tu kuweza ' kukuridhisha ' Wewe na ' usiwatumbue kitu ambacho hakina ' afya ' wala ' tija ' katika administrative / management perfomance na mwisho uwe unazisikiliza sana ' taarifa ' muhimu unazopewa kwani nimegundua kuwa ' tatizo ' kubwa la ' kimawasiliano ' ambalo pengine linakupelekea ' kujichanganya ' sana katika ' maelezo ' / ' matamko ' yako.

Naomba niishie hapa na narudia tena kusema kwa hili la jana la Wamachinga sijakubaliana na Wewe na bado kunatakiwa kuwa na ' mjadala ' mpana juu ya uwepo wao na ufanyakazi biashara wao na siku zote ' Siasa ' zisitupeleke ' kubaya ' hadi tukaonekana ' vituko ' mbele ya macho ya wenye ' akili ' na ' upeo ' wa ' kutukuka ' ILA nisikufiche ' tamko ' lako la jana lina ' utata ' mwingi na ' limejichanganya ' mno na wengine ' likituduwaza '.

Nikutakie tu kila la kheri na ' majukumu ' mema Mheshimiwa Rais wangu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ILA utanisamehe tu kuwa sijazoea wala kufundishwa kuwa ' mnafiki ' mbele ya ' ukweli ' au ' mtazamo ' ninaouona.

Umejenga hoja yako kwa msingi wa uongo, hivyo lazima upate hitimisho la uongo. Mfano wa uongo wako umesema Rais alitoa amri akihutubia Furahisha kuwa wamachinga waondolewe, huo ni uongo. Pia ulipowataja wateule wa rais ukasema pengine aliwatuma. Umemsikia rais hakuwatuma. Hoja zimemung'unyuka tu pale ulipoaanza. Kama tunapenda kukosoa si mbaya, lakini kabla hatujakosoa wengine tujikosoe kwanza sisi wenyewe uwezo wetu, hii ndio ya boriti na kibanzi. Unafiki ni dhambi mbele za Mungu
 
anacho zungumza mtoa mada ni ukurupukaji uliotumika katika kutoa maagizo ya jana ilhali huko nyuma alishatoa maagizo kinzani na haya ya jana.Halafu rungu linawaangukia watendaji kwa kufuata maagizo. Wewe jiweke katika hivyo viatu mkuu acha ushabiki wa kiitikadi.Hapa kinachofanyika ni kujaribu kuwafurahisha kundi ambalo limekuwa linasababisha "mayhem" katika majiji yetu kwa kukosa kutii japo kutopanga bidhaa katika barabara za watembea kwa miguu.Ni hawahawa ndio walioua mtu kwasababu aligonga bidhaa za mmoja wao kwa bahati mbaya ilhali ni wao ndio wanaopanga barabarani.Wao ni mabigwa wa kujichukulia shera mikononi. Mimi ninawaheshimu na kuwapenda sana lakini kwanini wasitengewe maeneo tengefu ndani ya jiji au katika vituo vikubwa vya mabasi iliwaondoe hii adha mabarabarani na nje ya nyumba/maduka ya watu watanzania wengine?

Anachosema mtoa mada ni uongo. Hakuna maagizo yaliyowahi kutolewa ambayo ni tofauti na maagizo ya jana. Maagizo ya jana ni msisitizo tu wa maagizo kama hayo aliyoyatoa tena akihutubia taifa live kutoka viwanja vya Furahisha. Hata kama huna kumbukumbu nzuri usikubali kudanganywa kama chekechea, jifanyie ka utafiti kako, hata mb za mia tano zinatosha!
 
Mimi kwa kweli namuunga mkono, ni wakati wa mlala hoi nae kufurahia nchi yake. Miongo mingi iliyopita matajiri ndio waliofaidi keki ya taifa.
Kutesa kwa zamu.
Sawa ndugu mlitaka machinga waende wapi KENYA? Machinga pia ni Watanzania ila cha kufanya watafutiwe maeneo sio kuwafukuza kama mbwa. Hawa ndugu zetu tumewazalisha sisi wenyewe kwa hiyo ni mzigo wetu lazima tuubebe. Machinga hawapo hata kwenye plan ya Tanzania ya viwanda sababu hawana elimu ya kuajiriwa. Cha msingi kila raia ahahakikishe ndugu wote wanapata elimu ya kutosha
 
Back
Top Bottom