Katika hili Google wamefanikiwa sana

James88

JF-Expert Member
May 14, 2017
1,700
1,754
Kwanza naomba tu nikiri kwamba sina muda mrefu sana tangu nimezifahamu simu za Google pixel, nilianza kuijua simu ya google pixel 2Xl, baada ya kuwatch video fulani youtube ambapo Kuna jamaa mmoja anaitwa Lew (Channel yake inaitwa Unbox therapy) aliwakusanya Youtubers wenzake ambao huwa wanafanya Unboxing ya electronics mbalimbali lakini sana huwa wamebase kwenye mobile phones.

Ile video ilikuwa na title inayosema which smartphone do you use?
Katika video ile huyu jamaa Lew alikuwa anawauliza youtubers wenzake kama Kina Marques Brownlee, Super Saf na wengine wengi kwamba ni simu gani ambazo wanatumia?

Aisee, nilitegemea kila mtu aseme anatumia simu kama s8+, note 8, iphone X au iphone 8+ lakini kitu nilichokutana nacho nilikuwa suprised kwa kweli, believe it or not, users wengi walikuwa ni watumiaji wa Google pixel 2XL and the reason kwanini wanatumia simu hiyo ilikuwa ni Quality of the Camera. hapa ndio nilianza kuzipa attetion hizi simu na hii Kampuni

Nilishangaa kwamba inakuwaje Google pixel zina only a single Camera lakini inacompete na high end devices zingine ambazo unakuta zina dual Camera mfano iphone 10 na bado kwa mtazamo wangu naona ilikuwa ikizipiga gap.

Naomba tu nikiri kwamba Camera za hizi simu za Google pixel ni kali balaa, lakini bado nikawa najiuliza swali moja, kwamba hawa jamaa wa Google hizi Camera zao wanatengenezea wapi? Lakini kinachokuja kuonekana ni kwamba hardware ya Camera ya hawa jamaa ni kama tu smartphones za makampuni mengine.

Now kama ni sawa na Makampuni mengine, Je ni kwanini Google pixel wawe na Camera nzuri kuliko simu nyingine hasa ukizingtia kwamba yeye ana single camera mbele na nyuma except kwenyw hizi simu alizorelease week hii ambazo ni 3 na 3XL ambazo mbele ndio zina duo camera while nyuma ni single kama kawa.

Ishu inakuja kuonekana kwamba kinachopelekea Google pixel wawe na Camera nzuri ni Software yao na siyo hardware. Am hili naliona linamake sense kiasi fulani kwa sababu hebu fikiria, Google ndio mtengenezaji na mmilikiwa wa software ya Android, kwa maana ya kwamba android phones zote wanamtegemea jamaa. Kama ni hivyo kwanini ashindwe kujipendelea yeye kwenye issue za softaware kwenye simu zake? Na kama ni kweli basi anaweza kutumia kigezo hichohicho kuwadondosha makamouni mengine makubwa ua simu kwa kuziboresha simu zake zaidi katika vitu vingine lakini kwenye swala la Camera tu tayari ameshateka soko ...

Anyway ngoja tuendelee kumuangalia may be kwa miaka mingine mitatu mbele.
 
Kwa simu zinazo-run on market now bado huawei p20 pro anashika usukani kwa ubora wa kamera ndio hao wengine wanfuata!
Boss ninatambua kwamba hiawei 20 pro ana camera nzuri... lkn hebu fanya comparison ya hata google pixel 2XL na hiyo p20 pro then ona difference iliyopo ilivo ndogo halafu piga hesabu kwamba unacompare simu ya single Camera kwa simu yenye tripple camera.... Simu moja ina 12MP while nyingine ina 40MP na mbele mwingine ana 8MP while mwingine ana 24MP.....
 
Mkuu umeshajaribu tumia Sony xperia zx2?
Hapana sijaitumia lakini what I know Sony ni moja ya simu ambayo ipo underrated sana. Mfano tu Sony Xperia XZ3 imezioutperform simu nyingi sana ukiangalia reviews zake...
 
simu yoyote inayotumia Highend soc za 800 series mfano sd845 ama 835 inaweza kurun software ya camera ya Google. Simu za kichina kama xiaomi ambao hawawezi ku afford technology kama hizo zinapata port ya hio camera na ku improve quality ya picha.
 
Back
Top Bottom