Katika hii dunia yanaweza kukusibu mpaka ukakufuru

Katika hii dunia yanaweza kukusibu mpaka ukakufuru

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,425
Kuna mzee alikua na maisha ya kawaida, mke na watoto. Akiwa na miaka 40+ alishajenga nyumba, watoto wanasoma na miradi yake inayoingiza mkate kila siku inaendelea. Kama binadamu kuna siku aliombwa msaada wa lifti na dada mmoja wa 30’s hivi. Alimpeleke alikokwenda na baadae aligundua hata nauli ya kurudia hakua nayo. Alimpa nauli na kuachana nae. Yule dada baada ya kufanikisha yake baada ya siku alimfuata yule mzee kwenye biashara na kumpa asante. Mzee alishukuru sana na kumwambia anakwenda kupata chakula cha mchana wanaweza kwenda wote.

Baada ya hapa walianza mapenzi. Mzee alikua msaada mkubwa kwa yule dada. Alimpangishia nyumba na walipata watoto watatu. Huyu mzee hakuwahi kulala nje. Alimheshimu sana mke wake.

Maisha aliendelea mpaka pale mke wake alipokuja kugundulika na maradhi ya saratani. Alimuuguza mke wake kwa muda mrefu. Alitumia pesa nyungi sana katika kuuguza na miradi yake iliyumba sana. Wakati huu ndiyo anafahamu kuwa bi mdogo wazazi wake walihamia nchini kutoka Zambia. Alizaliwa hapa lakini hafahamu ndugu zake. Ni kama mtoto yatima baada yakufiwa na wazazi wake.

Wiki mke wake anafikwa na mauti na bi mdogo anapata ajali ya gari. Huyu mzee amepata misiba miwili kwa pamoja. Wale watoto wa ndoa ni wakubwa na ndugu wa mama yao wanajiweza. Walijitokeza kuwasaidia. Tatizo sasa hawa watoto watatu wadogo atawaleaje.

Amaeamua kuoa mke atakae walea watoto watatu. Wakati huo biashara hazijakaa sawa na watoto wakubwa wamemwambia nyumba alijenga mama yao. Kama anaoa atafute makazi mapya na mke mwingine.

1620646804986.png

​
 
Nilikuwa najua ni ishu ya Bi Mkubwa kusitisha kabisa mwendelezo wa miradi bora ya JPM. Yaani amebaki kusafirisafiri tuuuuu na kuchekacheka kama yule wa Phase 4, huku mali zikifujwa hovyo. Hivi ile buttom ya kuakselereti muda uende fast forward to 2025 tumchague Rais, ikoga wapi kwenye PC jamani!???
 
Mtoto anapangaje maisha ya baba/mama yake ya kimahusiano??

Upuuzi huu wadhungu walishindwa zamani
Mitoto imekuwa imeacha ku focus na mahusiano yao inaanza kumpangia baba maisha.
Mitoto imeshindwa kujenga mahusiano yao inakalia kusumbukia mistakes za baba zake.Ni kukosa kazi na heshimA.

Baba kavurunda sasa mnatakaje? Nyie hamnA mahusiano huko ya ku focus?Mnataka baba yenu awe single..

Ningekuwa mimi nawaita kikao wote hlf nawaambia naoa mwanamke mwingine na atakaa hapa,mtoto atakaebisha siangalii umri na jinsia namzibua bonge la kofi la uso hlf namwambia sijakusomesha uje unipangie maisha yangu,panga maisha yako ili usijekosea km mimi.
 
Nilikuwa najua ni ishu ya Bi Mkubwa kusitisha kabisa mwendelezo wa miradi bora ya JPM. Yaani amebaki kusafirisafiri tuuuuu na kuchekacheka kama yule wa Phase 4, huku mali zikifujwa hovyo. Hivi ile buttom ya kuakselereti muda uende fast forward to 2025 tumchague Rais, ikoga wapi kwenye PC jamani!???
Mtateseka sana ngoma hii itakesha hadi 2030 haha
 
Back
Top Bottom