Katika hatua kama hii unaweza kuvunja mahusiano??

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,979
1,413
Nimekuwa na urafiki na dada mmoja kama miaka saba hivi imepita baada ya hapo nikamwambia mie napenda huwe mpenzi wangu mungu akipenda tuwe pamoja..yule dada akakubali tuakaanza safari ya mahusiano ki kimapenzi..tumendelea kwa kipindi kirefu tukavumiliana katika kila hari na kuombeana misamaha kibao kila mmoja wetu anapokosea kwa mwenzake,tumendelea nikafikia hatua ya kutoa mahari na familia zetu zikakutana na kufahamiana na kuwa kama ndugu baada ya hapo tukatangaza rasmi ndoa,wazazi wakafurahi wakasherekea kwa sana,
Shida sasa inakuja hivi huyu dada nimetokea kumchoka ghafla na upendo umepotea ghafla..ajaniudhi wala sijamuudhi..na wala hakuna shida yoyote,yaani nikimuona namchukia si mchezo hadi najuta kwa nini nimemposa,nilikwisha kumwambia jinsi ninavyojisikia juu yake akasema siku nikimwacha tu anajiua..Je katika mazingira kama haya naweza kuvunja kila kitu?je upande wa wazazi wetu pande zote mbili itakuwaje?best wangu anasema nijipe moyo mambo yatakuwa powa baadaye lakini naona kama napoteza mda na huyu dada..na nikitaka kumwacha nimwache katika mazingira gani ambayo roho yake itabaki salama?
 
Kuna mdau ashawahi kuleta mada kama hii humu ndani,kama sikosei Mwanajamii1 alimshauri kwamba katika mapenzi haya mambo huwa yako ni kama kakiwingu kanakufunika uso kidogo kwa muda na baadae penzi linarudi.Stay put ni hali ya muda tu itapita na penzi lenu litaendelea kama kawa.
 
Jamani, usimuache wewe kuwa na uvumilivu you never know hata ukimuacha huyo dada, utakuja kuregret hapo baadae, unaweza ukakosa chance kama hyo,( wanasema, Golden chance never come twice,) na ukija kumfuata tena inatakua too late! So take easy n you hv 2 thnk twice b4 that action brother..!! TAKE CARE!
 
kakaka kuwa muazi ili tuweze kusaidia na naomba useme tu nini kinakufanya ukimuona tu unamchukia sisis wote humu niwatu wazima
 
Hakuna alichonifanyia kitu kibaya huyu Dada..na hata ndugu zangu wanamfagilia kinoma,hasa mother ni balaa anapiga naye story utadhani yeye ndiyo mtoto,ila mie ndiyo habari sina.Alafu balaa jingine brother zake huyu dada tumekwisha kuwa mabest tunapiga story nibalaa sometimes tunatoka wote weekend,sababu wamekwisha kuwa watu wazima basi huwa wananipigia story za ndoa si mchezo ila wangejua niliyobeba moyoni du hata sijui..
 
Inatokea sana, usimwache baada ya muda utagundua unampenda sana, kwenye mahusiano kuna hali kama hiyo unaipotezea tu kwa muda utaona inarudia kawaida
 
Huyo ni satan mshinde kiume..kuna kitu katika mapenz kinaitwa siku kama hizi"itafika kipind utaona upendo unakuja wenyewe kama zamani...hukufanya makosa kumchagua umuoe ila unafanya makosa kutaman wengine,UPENDO UTARUDI PINDI HUYO UNAYEMTAMANI NJE YA NDOA utapomuona na mwanaume mwingine kwani hawara huwa na wapenz weng..TULIA NA WAKO
 
ok,kusitisha sio vibaya.
Wewe piga magoti muombe Mungu,mwambie kama ni yeye amua wewe umuoe huyo dada basi na iwe hivyo na kama ni mpamgo wake mwambie Mungu akuamulie,ikiwezekana sindikiza maombi haya kwa kufunga Mungu atakujibu na hata kama ni kuivunja itavunjiaka na najua yeye huyo dada atakua na hali gani na kama ni kujiua utakua ndio wakati wake umefika mana wewe huwezi zuia kufo chake hata kama mtakua ndoani.
Ni bora ivunjwe kama hujiskii tena kuliko mkishaifunga na yeye ndio mwanamke kuivunja itakucost sana.
BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA
 
mapenzi ndo yalivo.tulia upigwe PINGU ya Maisha ukae nae.hilo pepo la kumchoka mapema likutoke katika jiina la....
 
Sogeza mbele tarehe ya harusi; kama waweza chukua likizo uwe mbali naye kwa muda. Tengeneza Mazingira ya kummiss mapenzi yatarudi.

Mimi nafikiri ni uoga tu, na hiyo huwatokea wengi tu! Pia shetani yupo, kama ni muumuni sali sana!
 
Usingekuwa mpango wa mungu naamin tungekuwa tumeachana toka zamani..bado nilipitia kipindi kigumu cha maisha nilipoteza kazi na biashara zikawa mbaya bado huyu dada alivumilia na kunisaidia na kunipa moyo kuliko maelezo..sasa kwa nini hari kama hii itokee hatua za mwishoni?

Kaunga
KAUNGA..Kuhusiana na kusogeza arusi mbele bwana nilimshirikisha bro.wangu ebwana alinitukana kama mtoto vile hadi nikakata na cim..hatujaongea mpaka leo tena ilikuwa Juzi.hahahahaha
 
wanasema mapenzi ni kama nyumba hivi....

kuna nyumba unaiona nzuri mno but huipendi.....

nyingine ya kawaida but unaitamani mpaka basi.......

chukua likizo ya kwako binafsi kama wiki moja hivi,ukirudi utajua nini ufanye
 
Usingekuwa mpango wa mungu naamin tungekuwa tumeachana toka zamani..bado nilipitia kipindi kigumu cha maisha nilipoteza kazi na biashara zikawa mbaya bado huyu dada alivumilia na kunisaidia na kunipa moyo kuliko maelezo..sasa kwa nini hari kama hii itokee hatua za mwishoni?

Kaunga
KAUNGA..Kuhusiana na kusogeza arusi mbele bwana nilimshirikisha bro.wangu ebwana alinitukana kama mtoto vile hadi nikakata na cim..hatujaongea mpaka leo tena ilikuwa Juzi.hahahahaha
Kwa maelezo uliyotoa ya uvumilivu woote huo sasa sijui unataka mke wa aina gani, shauri yako makurumbembe yapo tena yatakudaka kwa mikono miwili...angalia sana pia sali huwezi jua ya dunia
 
wanasema mapenzi ni kama nyumba hivi....

kuna nyumba unaiona nzuri mno but huipendi.....

nyingine ya kawaida but unaitamani mpaka basi.......

chukua likizo ya kwako binafsi kama wiki moja hivi,ukirudi utajua nini ufanye
We unachukuaga likizo, na ukimaliza likizo unakuwa kawaida?
 
kwani ukimuoa hata kama humpendi una hasara gani???mie naonaga kwa mwanaume haisumbui,sie wanawake ndio baada ya muda na tukishaolewa na kuachika ndio taabu kusettle tena na mtu, ila mwanaume yeye saa zote katika umri wowote akiamua kuoa anaweza kuoa,so wewe muoe hivyo hiyo hata kama humpendi with time mapenzi yatakuja na yasipokuja huna hasara unamwacha tu ukijisikia.
 
Back
Top Bottom