Katika awamu hii ya ujenzi wa Stiegler's Gorge ni aibu mteja wa TANESCO kucheleweshewa kuunganishiwa nishati ya umeme kwa sababu ya uhaba wa nguzo

Biloba

Member
Dec 28, 2018
43
27
Tokea kuingia madarakani Novembe 2015, Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejikita katika utatuzi wa changamoto mbali mbali zilizokuwa zikiikabili tasnia ya uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme. Ndani ya kipindi kifupi cha miaka 3 tu changamoto za taifa kutegemea uzalishaji wa umeme wa dharura ambao uzalkishaji wake ulikuwa ni wa gharama kubwa zenye atrhari kubwa kwa uchumi wa tifa limekuwa ni jambo la kihistoria, kwa kushuhudia kukamilika na kuzinduliwa kwa miradi ya uzalishaji umeme ikiwemo Kinyerezi 1 na 2, lengo ikiwa ni kuuongeza uwezo wa ndani wa uzalishaji umeme wa gharama nafuu.

Aidha tunashuhudia msukumo mkubwa sana katika utekelezaji wa miradi ya REA-Usambazaji Umeme Vijijini ambapo hivi sasa ukizunguka katika wilaya mbali mbali za vijijini hapa nchini wakandarasi wako mbioni kujenga miundombinu ya usambazaji umeme na kuwaunganisha wakazi wa maeneo ya vijijini; lengo ikiwa ni kuongeza idadi ya watanzania waliounganishwa na nishati ya umeme. kwakuwa kigezo hicho ni moja ya vipimo vya maendelo na ukuaji wa uchumi wa nchi na wananchi wake, lakini pia kadri wananchi wengi zaidi wanavyounganishwa na nishati ya umeme ndivyo uwezo wao wa uzalishaji mali na kuchangia kukua kwa pato la taifa unavyoongezeka.

Kama hiyo haitoshi tunashuhudia Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli iko mbioni kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa maji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Katika uitwao Stiegler"s Gorge. Ujenzi huu ambao unatekelezwa kwa fedha zetu wenyewe, utakapokamilika unatarajiwa kuzalisha Mw 2000 za umeme zitakazoingizwa kati gridi ya taifa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya ukuaji wa uchumi wetu, kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa zetu za viwandani, uongezaji thamani mazao yetu n.k kwakuwa uzalishaji wake ni wa gharama nafuu kuliko vyanzo vingine vyote vinavyotumika hapa nchini kuzalisha nishati ya umeme hivi sasa.

Itakumbukwa kuwa ujenzi wa mrdai huu ulianza kuasisiwa na Serikali ya awamu ya kwanza zaidi ya ,miaka 40 iliyopita. Lakini kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo taifa letu kupigwa vita vyta kiuchumi, ujenzi wake haukuweza kuanza. Aidha awamu tatu za uongozi wa taifa letu zilizofuata kutokea 1985 hadi 2015 pia hazikuweza kuanza ujenzi wa mradi huu kutokana na figisu figisu za kiuchumi kutoka kwa mabeberu wasioitakia nchi yetu mema.

Kutokana na jitihada zote nilizozieleza hapo juu za Serikali ya awamu ya Tano kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya uzalishaji, usambazaji nishati ya kwa lengo la kuongeza idadi ya watanzania waliounganishwa na nishati hiyo, nilitegemea watumishi wa umma wanaohuduma katika tasnia hii wangebadilika na kuacha kuendelea kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wangekwenda na kasi ya serikali hii kutimiza shabaha zilizotajwa hapo juu.

Kinyume chake bado baadhi ya watumishi wa Tanesco wamechapa usingizi wa pono na kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya watanzania inaunganishwa na umeme kadri wanavyokuwa tayari na kuhitaji huduma hiyo muhimu kwa uboreshaji viwango vya maisha, uzalishaji na ukaji wa uchumi wa nchi. Kwa watumishi wa aina hii kwao ni jambo la kawaida kabisa kumchelewesha mteja kuunganishhiwa umeme kwa visingizo mbali mbali ikiwemo "uhaba wa nguzo".

Kwa hakika ni aibu kubwa sana kwa Tanesco na watumishi wake wasio na maadili ya kutimiza wajibu wao ipasavyo kutafuta visingizio vya ina yeyote kwa lengo la kuhalalisha ucheleweshaji wa aina yeyote wa kuwauunganishia wateja nishati ya umeme, ikizingatiwa kuwa Serikali inawekeza kiwango kikubwa cha raslimali katika ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme, fedha ambazo zinatarajiwa kurejeshwa kwa idadi kubwa ya wananchi kulipia gharama za kuunganishwa na huduma hii na pia kulipa matumizi yake. Aidha pia mapato ya Tanesco pia yanategemea uwepo wa idadi kubwa ya watumiaji huduma ya umeme.

Vilevile haiingi akilini kabisa sababu mojawapo inayotolewa na baadhi ya watumishi wa Tanesco wasio wa waadilifu kwa mteja kucheleweshwa kuunganishwa umeme inapokuwa ni "uhaba wa nguzo". Ikizingatiwa kuwa nguzo zinazalishwa hapa hapa nchini.

Ninajiuliza ikiwa ndani ya miaka 3 tu akiwa madarakani Mhe Rais Mhe John Pombe Magufuli ameweza kutatua changamoto za taifa kutegemea umeme wa dharura wa gharama kubwa na athri kubwa kwa uchuni wa tifa letu na pia kupangua vikwazo vyote vilivyokuwa vikikwamisha ujenzi wa mradi wa Stigler"s Gorge kwa takribani miaka 40 ikiwemo kuwagaragaza mabeberu waliokuwa wakitumia visingizio mbali mbali kukwamisha ujenzi huo, Iweje wasaidizi wake ndani ya tasnia ya nishati ya umeme washindwe kukabiliana na changamoto ndogondogo kama vile uhaba wa nguzo, mita na vifaa vinavyohitajika kuwaunganishia wateja huduma ya umeme?

Nmelazimika kujiulkiza maswali haya kwa sabbu nina Imani kuwa Tanesco inayo idara ya ugavi tokea matawi ya wilaya, mikoa hadi makao makuu inayoongozwa na wakurugenzi, mameneja na maafisa wa kada mbali mbali, waliohitimu vyema fania ya ugavi; ambapo moja ya majukumu yao ni kufanya makisio sahihi ya idadi ya wananachi watakaohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme katika maeneo ya utendaji na kuwasilisha taarifa hizo ngazi za juu kwa uagizaji/ununuzi na uwasilishaji vifaa vinapohitajika kwa wakati. Ni Imani yangu pia kuwa wahusika hwa wote wanalipwa mishahara na marupurupu kila mwezi.

Sasa iweje katika awmu hii ambayo inatarjia idaqdi kubwa zaidi ya watanzania waunganishwe na nishati ya umeme wawepo baadi ya watumishi wqa Tanesco wazembe wanaotafuta visingizio visivyo vya maana kuwachelewesha pasipo sababu za msingi watanzania walio tayari kuitikia wito wa serikali wa kubadilika kutoka matumizi ya nishati zisizo na tija kama vile kuni, mkaa, vibatari n.k na kujiunga na mtandao wa nishati ya umeme uliowekezwa na Serikali kwa gharama kubwa za walip kodi?

Kwakuwa natambua kuwa watumishi wa aina hii wanatambua kuwa fedha zinaozowekezwa katika miundombinu ya uzalishaji na usambazji wa umeme zinatakiwa kurejeshwa kwa idadi kubwa ya watanzania kuunganishwa na mtandao wa nishati ya umeme kwa malipo na pia kulipia matumizi ya nishati hiyo, Aidha pia wanatambua kuwa mwajiri wao Tanesco pia inategemea uwepo idadi kubwa ya wateja waliounganishwa na huduma hii ili kupata mapato zaidi; sichelei kuwaita watumishi hawa wanaoshondwa kutimiza wajibu wao kuhakikihsa uwepo wa idadi ya kutosha ya nguzo, mita na vifaa vya kuwaunganishia wateja nishati ya umeme ni wahujumu uchumi.

Umefika wakati sasa Wizara ya Nishati ikawatupia macho watumishi wa iana hii wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya watanzania inaunganishwa na huduma ya nishati ya umeme kadri wanavyohitaji. Aidha nitoe ni rai kwa Waziri wa Nishati apige marufuku watumishi wa Tanesco kuwapatia wateja sababu zisizo za msingi kama vile uhaba wa nguzo, mita na vifaa wanapowachelewesha kuwaungainishia wateja nishati ya umeme.

Makazi yangu yapo mita 52 kutoka nguzo ya mwisho ya miundombinu iliyojengwa na REA kwa fedha nyingi sana. Safari yangu ya kuomba umeme ilianza mwezi Julai 2018, ambapo ilichukua zaidi ya miezi mitatu kumpata mthamini toka Tanesco kuja kunifanyia thathmini ya kiwango cha gharama ninazo stahili kulipa. Hii ilikuwa baada ya ufuatiliaji mkubwa wa zaid ya safari 6 katika ofisi za Tanesco Vwawa Mkoa wa Songwe. Nilifanya malipo tarehe 13 Novembe 2018 jumla Shs 337,739.80. Hadi sasa ninakimbilia mwezi wa pili sijaungiwa huduma ya nishati ya umeme ilihali miundombinu iliyowekezwa na Serikali ikiwa imekaa pasipo kuwa na wateja wa kutosha. Niiombe Tanesco inipatie maelezo ya kutosha ni kwanini sijaunganishiwa huduma hii ilihali nilishafanya malipo stahiki na miundombinu iliyowekezwa na serikali kwa fedha nyingi ikiwa haina wateja wa kutosha?
 
Tatizo la nguzo za Umeme Stiegler’s Gorge ina ingiaje hapo.......au ndo mambo ya kujaza booklet?
 
Hivi unapoitaja KINYEREZI 1 and 2, NA WAKATI HUO HUO HABARI YA GESI UMEITUPILIA MBALI, WHAT DO YOU EXPECT AFTER FOUR YEARS?

Maana siku hizi gesi kimyaa ni "stiglazi goji" tu... To me hiyo "stigla goji" ni hydropower generation kama mtera tu... Tusubiri kuambiwa bwawa limejaa tope... HALAFU TUJE KUITAJA WACHAWI..!!
 
Waache wahusika watafute linkages. haya yameizidi IQ yako kwa kiwango kikubwa
Haya bhana Mr IQ kubwa......issue ni ukosefu wa nguzo na ulikuwa na hoja ya msingi ukashindwa ku address tatizo ukabakia una sifia sifia tuu......TZ kumekuwa na kizazi cha kinafiki mno.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Back
Top Bottom