Katibu wa Tume ya Utumishi na Nidhamu ya Walimu Wilaya ya Muleba ajinyonga

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Katibu wa Tume ya Utumishi na Nidhamu ya Walimu (TSD ) Wilaya ya Muleba, Manase Mkumbo amekutwa amejinyonga shambani kwake.

========================

Katibu wa Tume ya Utumishi na Nidhamu ya Walimu (TSD ) Wilaya ya Muleba, Manase Mkumbo amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga shambani mwake katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Francis Isack amesema Mkumbo alijinyonga usiku kuamkia leo.

Amesema kabla ya tukio hilo alituma ujumbe wa maandishi kwa simu akimjulisha mwanae aliye masomoni kuwa amekata tamaa na maisha.

Isack amesema Mkumbo aliondoka Muleba kwenda kukagua mashamba yake kijijini ambako aliandika ujumbe huo na kununua kamba ya katani na kujinyonga.

Ujumbe huo ulipomfikia mtoto wake aliutuma tena nyumbani katika Kitongoji cha Bugombe wilayani Muleba ndipo wakaanza kufuatilia kwa kuwa alikuwa amewaaga kuwa anaelekea shambani ambako walikuta mwili wake umetundikwa.

“Inasikitisha mtu alibakiza mwaka mmoja astaafu na kupata mafao yake lakini anaamua kujiondoa na kuacha hasara na simanzi kwa familia,” amesema Isack.

Amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kwao mkoani Singida zinaendelea.


Chanzo: Mwananchi
 
Umefika wakati sasa mafisadi wawe wanapigwa rirsasi, wasipewe nafasi ya kujiua au kujinyonga wenyewe maana huyu jamaa sasa ataonekana shujaa
 
Kwahiyo familia imeridhika kabisa kuwa huo ujumbe wa simu aliuandika marehemu kabla ya kifo?
What if ujumbe umeandikwa na mtu mwingine kabisa baada ya kumning'iniza marehemu?
Au kwakuwa sote tumeandikiwa ukomo wa kuishi basi ndo ufuatiliaji wa vyanzo vya vifo tata kama hivi tupotezee??
 
Kwahiyo familia imeridhika kabisa kuwa huo ujumbe wa simu aliuandika marehemu kabla ya kifo?
What if ujumbe umeandikwa na mtu mwingine kabisa baada ya kumning'iniza marehemu?
Au kwakuwa sote tumeandikiwa ukomo wa kuishi basi ndo ufuatiliaji wa vyanzo vya vifo tata kama hivi tupotezee??
Ataenda kufanyiwa postmortem mkuu na majibu yatatolewa
 
AfisaELimu wilaya na hapohapo ni katibu wa TSD?Anavyeo vyote viwili?Inawezekana kumbe kuwa na vyeo hivyo kwa wakati mmoja?

R.I.P katibu
 
Nadhani kuna kitu behind the scene ya tukio hilo ni vyema uchunguzi zaidi ukafanyika

Mkuu;
Tuseme afisa Elimu (W) hawezi kujinyonga? Mbona matajiri wengi tu wamejitupa kutoka ghorofani na kufa hamsemi wachunguzwe? Mbona matajiri wengine wamejitupa kwenye treni iendayo kasi wakafa, Wengine wakajilipua na ndege zao. Jamani, kila mtu aweza kujinyonga kama hana Yesu ndani yake. Yeye ndiye faraja ya wote. Msinichukie, sihubiri dini nasema ukweli tu
 
Nchi inahitaji wataalamu wa saikolojia, tunakoelekea haya matatizo yabazidi. Maisha yamezidi kubana, wengi sasa wana msongo wa mawazo unaohitaji washauri wa afya ya akili kuwasaidia.
 
Ataenda kufanyiwa postmortem mkuu na majibu yatatolewa
Mathalani marehemu alikamatwa na njemba mbili wakamtia kitanzi kabla hajafa then mmoja akapanda juu ya mti na kurushiwa kamba huko mtini kisha wakamning'iniza huku akirusharusha miguu hadi umauti ukamtokea wakachukua simu na kuandika ujumbe kwa jamaa wa marehemu. je, postmortem itaonesha dhahiri vitendo vyote vya kabla ya kifo?

Ufafanuzi tafadhari...
 
Back
Top Bottom