Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Lubinga ampa Nape Nnauye makavu live: Atuambie kama ana Ajenda ya Siri

Mbona
Tatizo linakuja pale muhamaji hajakili kuacha itikadi iliyompa ubunge huko atokako pale anapoonekana akiongea kwenye press. Ni wachache wanaokili ideological shift.
Watakaohama tena waambiwe wake wawazi zaidi wasitoe sababu za juujuu.
Mbona Lowassa alipohama ccm hajarudisha kadi ya ccm, tuseme naye hajaacha ideology ya ccm japo yupo chadema?
 
Chama chenu hakitaki maendeleo ...mwanachadema anayetaka maendeleo na kuisifia Ccm anaitwa msaliti na kufutwa chama sasa unataka wabunge na madiwani hao wafanyeje?
Acha wahame na kujiunga kwenye chama chenye lengo,nia na utekelezaji wa maendeleo ya kweli.
Baada ya karibu miaka sitini ya uhuru Tanzania bado ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani na chama ni kile kile miaka yote. Sasa kuna ni nini cha kujivunia hapo.
 
Mbona
Mbona Lowassa alipohama ccm hajarudisha kadi ya ccm, tuseme naye hajaacha ideology ya ccm japo yupo chadema?
inawezekana. watafutwe wahojiwe na waandishi wa habari wanaweza kueleza vizuri.
huko ndiko kuhama chama ninakokuelewa. Ideological shift powered by public confession.
 
mimi mafikili nape alikua na maana kwamba,
watu wananunuliwa wakisha hama na kabla hajafundishwa tamaduni za huko anakohamia ,tayari anapewa au anapitishwa kua mgombea wa cheo kilekile tena kwa ubabe hata kwa kunyofoa moyo wa mtu wanahakikisha mgeni huyo anatangazwa mshindi.
sasa kwa shida yote hiyo ya nini?
si mtu huyo ahame na cheo chake.
ukweli ccm wamekua wa hovyo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama chenu hakitaki maendeleo ...mwanachadema anayetaka maendeleo na kuisifia Ccm anaitwa msaliti na kufutwa chama sasa unataka wabunge na madiwani hao wafanyeje?
Acha wahame na kujiunga kwenye chama chenye lengo,nia na utekelezaji wa maendeleo ya kweli.
KWa hiyo kutumia mabilioni ya fedha kununua wapinzani then kuitisha uchaguzi uchwara huku mkitumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi ndio unayaita maendeleo sio?!
 
Sioni kibaya alichoongea nape!

Nchi ambayo wananchi wake hata maji safi ya kunywa shida Eti inatumia mabilioni kurudia uchaguzi kisa Watu wanaunga mkono juhudi za rais!

Halafu huyo raisi anajigamba rais wa wanyonge Mara ana bana matumizi huku anafurahia huu upuuzi!

Nape kaliona hilo ndo maana anasema; Hakuna haja ya kwenda kuwatesea watu juani huku mkijua kuwa aliyekuja huku ndiye mtapitishia ushindi iwe iwavyo. Sasa, kuna haja gani kuangamiza mamilioni huku shule hazina madarasa, hospitali hazina dawa na vijiji husika hawana maji safi ya kunywa??
Nape anatamani tujielekeze kwenye kuleta maendeleo sio kuleta wapinzani ndani ya chama mfu. Nimuunga Nape mkono
 
Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Ngemela Lubinga, akizungumza na Mwananchi juu ya Kauli ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kuwa mtu anayehama Chama ahame na ubunge wake; amemtaka Nape aweke wazi kama ana ajenda nyingine ya siri ili ifahamike wazi. Kanali Lubinga alidai kuwa, "haiwezekani hata kubadilisha sheria kwa sababu suala hilo lina mkanganyiko."
Kanali Ngemela alifafanua kuwa, "Itikadi ya Chama ndiyo inakifanya kishinde Uchaguzi, hivyo kuhama na uwakilishi ni kuwanyima haki wapiga kura waliomchagua kwa itikadi ya Chama chake."
Kwa hali hiyo, "Atuambie kama ana ajenda ya Siri."

View attachment 842058

Je, wamemchoka ama?
Je, Nape anajua hana chake ndani ya CCM come 2020, so anatamani ahame sasa hivi na ubunge wake?
Je, bado Bashiru atamlinda na ukosoaji wake huo unaopinga Chama kupata wafuasi wapya na wenye ushawishi?
Hivi bado wapiga kura wa nchi hii wana haki ya kumchagua kiongozi au wana haki ya kuchaguliwa kiongozi?
Kwani wanapohamia wanapotaka wamepewa ridhaa na wananchi au wamehama kwa kuwadharau wale waliwachagua?
Ningemwomba kanali Ngemela Lubinga ajibu hayo maswali!!!!!!!!

Wangetuacha bana!Wasione watanzania wamekaa kimya akadhani wao ndio wamewashikilia akili zao hivyo hawawezi kufikiri hata kama wanatuzuia kuhoji!!!
 
Back
Top Bottom