Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza arejea CCM

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza arejea CCM

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Habari Wakuu

Wakati tukielekea kwenye UKUTA katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza aachia ngazi na kurejea CCM.

Updates zinakuja wakuu........

=======

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, John Nzwalile amejivua nyazifa zake tatu pamoja na uanachama wa chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa na ubabaishaji.


Mbali na ukatibu wa mkoa, Nzwalile alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Mwanza, Nzwalile amesema Chadema kimekuwa kikiwachonganisha wananchi na Serikali, jambo ambalo amesema halikubaliki.

“Nimefikia uamuzi huu mgumu wa kujivua nyadhifa zangu zote na uanachama wa Chadema baada ya kuchoshwa na siasa za uchochezi, majungu na uchonganishi zinazofanywa na chama hiki kikubwa cha upinzani nchini,” amesema Nzwalile

Amesema imefika hatua viongozi wa Chadema wakijifungia ndani kwenye vikao vyake vinahusu maandamano na uchochezi pekee, kwanini “tusifanye shughuli za maendeleo badala ya kuhamasiha vurugu na uvunjifu wa amani,” amehoji Nzwalile.


Chanzo: Mwananchi
 
Bei kaka, bei kaka!!! Hali yenyewe ngumu ivi then mpunga mezani aaaah tuheshimiane!!!
 
Mimi nasema huyu Magufuli analazimisha watu wampende yeye na chama chake kwa kutumia nguvu ya dola. Ajaribu kuruhusu wapinzani kufanya mikutano aone watanzania watakavyounga mkono maazimio, mipango, mikakati na hata matamko mbalimbali yatakayo tolewa na viongozi hao wa upinzani. Kama watanzania wangekuwa wanafurahishwa na utawala wake kamwe asingetumia polisi kukamata kila anayemkosoa (Rais) na kumwita mchochezi. Hii ni fedheha kwa watawala wetu.
 
Wamemkata mkia?, mkuu hebu leta taarifa kamili ili tujuwe kama ameingia kwenye zizi na mkia wake
 
Habari Wakuu

Wakati tukielekea kwenye UKUTA katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza aachia ngazi na kurejea CCM.

UPdates zinakuja wakuu........
Huyo alistahili kuachai ngazi soon after uchaguzi mkuu! Mwanza ilikuwa ni moja ya mikoa ambayo CHADEMA walitarajia si tu kwamba wangepata wabunge wa kutosha bali kura za EL zingetoka nyingi sana pande hizo! Matokeo yakawa kinyume chake... thanks to utamaduni wetu wa kutopenda kuwajibika! How did he come to lose the whole of Mwanza?!
 
Hata hivyo amechelewa sana kung'oka mana ilibidi awe ametoka muda mrefu sana..
 
Mimi nasema huyu Magufuli analazimisha watu wampende yeye na chama chake kwa kutumia nguvu ya dola. Ajaribu kuruhusu wapinzani kufanya mikutano aone watanzania watakavyounga mkono maazimio, mipango, mikakati na hata matamko mbalimbali yatakayo tolewa na viongozi hao wa upinzani. Kama watanzania wangekuwa wanafurahishwa na utawala wake kamwe asingetumia polisi kukamata kila anayemkosoa (Rais) na kumwita mchochezi. Hii ni fedheha kwa watawala wetu.
The obvious
 
Huwa mnajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe......FYI you stomach Thinkers & Seekers boys CHADEMA siyo man alone kama ilvyo huko CCM kuheshimu mawazo ya Mwenyekiti huku hakunaga.
 
Mimi nasema huyu Magufuli analazimisha watu wampende yeye na chama chake kwa kutumia nguvu ya dola. Ajaribu kuruhusu wapinzani kufanya mikutano aone watanzania watakavyounga mkono maazimio, mipango, mikakati na hata matamko mbalimbali yatakayo tolewa na viongozi hao wa upinzani. Kama watanzania wangekuwa wanafurahishwa na utawala wake kamwe asingetumia polisi kukamata kila anayemkosoa (Rais) na kumwita mchochezi. Hii ni fedheha kwa watawala wetu.
Sio kweli...msipende propaganda kwenye kila jambo,mengine yanafanyika kwa utashi.
 
Back
Top Bottom