PreGE2025 Katibu wa CHADEMA Bariadi na wengine 83 wajiunga na CCM

PreGE2025 Katibu wa CHADEMA Bariadi na wengine 83 wajiunga na CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,780
Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Bwana Charles Nduhi Lyaganda amejiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM akiambatana na Wanachama wengine 83 wa Chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Kadi ya CCM, Lyaganda amewaambia wananchi kuwa Amezaliwa kwenye familia ya wanachama wa CCM, hivyo ameamua kurudi nyumbani,akieleza kwamba imekuwa ikimuhia vigumu kuendelea kuwa ndani ya Chadema, akiwarai wagombea wa nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kumtumia kwaajili ya kampeni zao.

Lyaganda amejiunga na CCM wakati huu ambao Viongozi wakuu wa Chadema wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti John Heche na Katibu Mkuu John Mnyika wapo Mkoani Simiyu kwaajili ya muendelezo wa ziara za kichama za kueneza azimio la No reforms, No election lenye kutaka mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi ili kuruhusu usawa na haki.

 
Mjinga huyo.
Sasa ukizaliwa kwenye familia ya wqchawi nawe unakuwa mchawi
 
Back
Top Bottom