Katika kile kinachoonekana ni kukataliwa CCM kwenye jamii kutokana na ugumu wa hali ya maisha, jana mchana Katibu wa CCM Tawi Kishanje Bukoba Vijijini anayejulikana kwa Jina la Peter Zelamula alipigwa na vijana aliowakuta wakipata kinywaji huku wakitafakari ukali wa maisha. Aliwaambia kuwa tarehe 19.07.2013 kuna wajumbe wa Wilaya toka CCM watafika kijijini kutoa mafunzo ya kuikataa RASIMU YA KATIBA MPYA.
Kwa mujibu wa mtoa habari vijana hao walimuuliza katibu huyo mambo yanayowasibu wakaazi wa kijiji hicho kwa muda mrefu huku CCM wakiangalia bila kujali shida zao za muda mrefu kama zifuatazo.
1. Sheria ya kuwazuia kuvua samaki wakati wao ni wavuvi wa asili, sheria inawalinda wavuvi wakubwa tu wanaovua samaki na kuwapeleka viwandani wananchi wakiambulia mapanki.
2. Juzi walikuwepo maofisa wa samaki kijijini wakawapiga na kuwajeruhi vijana huku wakipora fedha za baadhi ya wananchi kati ya 50,000.00- 200,000.00 kila waliyekutana naye njiani na kumshuku kuwa ni mvuvi, walipasua mitumbwi na kuleta hasara kubwa wa vijana hao.
3. Walitaka awaambie mbona CCM Tawi la kijijini halijachukua hatua zozote kulaani vitendo viovu vya maafisa samaki wanapomkuta na mtu amebeba samaki mmoja huulizwa kampata wapi, na kuchukua hatua za kuwapiga au kuwafungulia mashtaka kwa kupatikana na kitoweo cha samaki.
4. Baada ya katibu kokosa majibu wakati yeye nyumba yake ipo ufukweni mwa ziwa victoria kitongoji Bweza wakaamua kumpa kichapo lakini akaja kuokolewa na jamaa wapita njia.
Kuanzia Alhamis wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya wilaya kutoka kata zote za Wilaya Bukoba wameitwa Bukoba mjini kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kuikataa RASIMU YA KATIBA MPYA wakati mabaraza yatakapoanza vikao vyao.
Hayo ndiyo yanayojiri huku Kishanje Bukoba Vijijini.