Monasha
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 561
- 422
KATIBU kata wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Iringa Vijijini, Patrick Ngara (40), mkazi wa kijiji cha Ilandutwa, ameuawa kinyama kwa kucharangwa mapanga akiwa nje ya nyumba yake usiku wa kuamkia jana.
Mauwaji hayo ya kinyama kwa kiongozi huyo wa CCM kata ya Mgama yamekuja siku moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa upande wa Tanzania Bara, John Chiligati, kuelezwa wazi wazi na diwani wa kata hiyo ya Mgama, Denis Lupala, kuwa hafai ndani ya CCM na ni mmoja wa waliotakiwa kuvuliwa gamba Dodoma.
Mjane wa marehemu Tumain Ndendia (36) alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 2.45 usiku wakati katibu huyo akitoka katika vikao vya chama.
Alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea yeye na mtoto walikuwa ndani wakijiandaa kulala na ghafla alisikia sauti ya kishindo nje mfano wa kitu kuanguka chini na baada ya kutaka kutoka alisikia sauti za watu wakishauriana kuingia ndani kufanya mauwaji.
Mtu kauawa kisa??????????????
Source: TANZANIA DAIMA.