Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.Mhe Rais John Pombe Magufuli tunakuomba na kukushauri kuwa UTENGUE wadhifa wa Katibu Tawala wa Dar es Salaam - Theresia Mmbando. Kwanza amekuaibisha mbele ya umma na kusema uongo wa mchana dhidi ya Serikali yako. Iweje Katibu Tawala mzima ashindwe kupitia nyaraka alizopewa na wa chini yake na kusema kuwa alipewa tu kuisoma na hakuipitia. Kama ndiyo staili yake ya kazi HAFAI KUWA KATIBU TAWALA na hawa ndiyo mmojawapo wa majipu yanayotakiwa kutumbuliwa haraka.