Katibu Tawala Makungu, hivi Nzega Mji kuna nini?

Nazi embe

Senior Member
Sep 20, 2016
105
123
Tunaweza kusema hii ndio halmashauri ambayo boss wake ajali kabisa maslaahi ya watumishi wake kati ya halmashauri zote za mkoa wa Tabora na haya malalamiko na manunguniko tunaimani katibu tawala makungu na mkuu wa mkoa Ally hapi mshayapata maana tunajua wewe makungu ni mtu wa usalama una njia nyingi za kupata tarifa ila hapo nzega mji mbona kama huoni mfano.

1. Hii ndio halmashauri ambayo watumishi wake wanapata uhamisho wakubadilishana vituo vya kazi na watumishi kutoka halmashauri nyingine ila ajabu yule wa mbali anakwenda nzega, ila yule wa nzega aondoki hao wamejaa kibao nakifutilia hakuna majibu mazuri wanayopewa wanaishia nungunika tu na kufanya kazi bila morali.

2. Likizo hapa napo tatizo watumishi kulipwa pesa za likizo mtihani mpaka unajiuliza halmashauri nyingine wanatoa wapi pesa za likizo maana kama nzega dc wanalipwa pesa za likizo hata kabla hawajaondoka ila nzega tc mtu ataenda atarudi na akadai ila bado halipwi ajabu wao kwaa wao idarani umo kila mwaka wanaenda likizo na wanalipana ila watumishi uku wakiomba ishirini kwa mwaka basiwataliwa watatu wengine wanambiwa pesa zimeisha subilieni zike kila mwaka tatizo nini.

3. Haya Uhamisho wa vituo vya kazi hili ndio tatizo sugu tena sugu kweli maana watumishi Wanabadilishiwa vituo vya kazi wakiandika barua za kudai malipo yao kama waraka wa kudumu wa utumishi wa umma unavyofafanua, mkurugenzi anawaajibu uhamisho wa mjini huana malipo anatumia waraka wa utumishi wa umma na 2 wa mwaka 2018 kifungu cha 3. 2(i) yani hiki kifungu imekuwa kama fimbo kwake kudhurumu stahiki za watumishi yani hata Ile busara hatumii kuwa hawa watumishi wangu ngoja niwape hizi haki zao iwe motisha ya ufanyaji kazi yeye haoni ni ubaya ubaya tu kuna kundi kubw la walimu wa shule msingi na sekondari wamehamishwa mpaka leo hawajalipwa yupo kuwambia kifungu kinakataza yani mpaka unashangaa kifungu kinazungumzia mjini tena ajirizishe ina maana mamuzi yapo kwake akubali au akatae ajabu anakataa tu hata ambao kifungu hakitamki yeye kisa ni nzega mji ataki tu anasahau kuwa wapo watumishi ambao kimuundo halmashauri ya mji wa nzega ina kata kumi na katika hizo kata kumi kuna kata mbili tu ndio kisheria zipo mjini kuna nzega mjini magharibi na Nzega Mjini mashariki kwingine kote uko ni kata ambazo zinaundwa na vijiji na vitongozi ila yeye anahamisha watumishi uko anawambia uhamisho huu wa mjini mwajiri kajirizisha uhamisho aujathiri makazi yani unabaki unashangaa ujasiri huu anautoa wapi hivi katibu tawala unajua hilo huu uhuni upo na hawa walimu wanaodai wapo uliza chama cha walimu wanajua, ajabu watumishi wake pale pale wanasema mapesa ya uhamisho yapo mengi tu hayajatumika Sasa unajiuliza kama pesa zipo anakatalia nini, katibu na mkuu wa mkoa futilieni hili ni tatizo.

4. Sulaa la kutofautiana na watumishi wake ambao kafanya nao kazi kwa sitofahamu zoa wenyewe ambazo takukuru wanajua vyombo vya usalama wanajua ila kwakua yeye boss anawatoa vijana hawa kafala amekuwa ni bigwa wakuwatoa katika idara zao nakuwapeleka idara nyingine na hao watumishi wakisema waatafute uhamisho amawagomea wapitilishia barua zao yani ubabe ubabe tu kwanini hili linafanyika nzega tu.

Haya si majungu ni Mambo ya ajabu ambayo yanaendelea fanyika eneo ambalo kama vile haku uongozi tumekaa kimya pengine atajirekebisha ila wapi kwakua katibu umeaishwa leo kaanze nayo.

Haya ni machache tu yapo ya afisa utumishi wake aliyeondoka na mwanasheria wake alieenda masomoni tukiona ukimywa unazidi tunayaleta hapa.

Tunajua mkurugenzi ni kiburi atapata ujumbe huu atasema ababaishwi na Mambo ya mitandaoni sawa ila katibu tawala saidia hapa kuna tatizo maslahi ya watumishi hayapewi kipaiambele.

Hivi ujenge hospital, mashule nk alafu watumishi una wanyanyasa ina maana gani hiyo miradi ya maendeleo.
 
Hii ni kweli kama wewe ni dereva na unataka uhamisho hupati kabisa sijui wengine huko.
 
ukweli mtupu MAGESA ni kiboko
Aache ubabe halmashauri siyo mali yake au ya baba yake Ile ni mali ya umma atafanya kazi ataondoka ataicha kwaiyo asinyime maslahi ya wengine Kama vile anatunza mali ya familia yake kuwa akiondoka familia itabakije
 
Nzega kama Nzega.............ile stand mpya imeshamalizika kujengwa?
Nilisikia ofisi za Halmashauri zitahamia huko stand mpya?
Nzega pako poa sana kuna usafiri wa kwenda sehemu yeyote Tanzania hadi nje ya Nchi.
 
Aache ubabe halmashauri siyo mali yake au ya baba yake Ile ni mali ya umma atafanya kazi ataondoka ataicha kwaiyo asinyime maslahi ya wengine Kama vile anatunza mali ya familia yake kuwa akiondoka familia itabakije
Mabadiliko Mabadiliko Mabadiliko!!!
 
Back
Top Bottom