Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk.Joyce Ndalichako Wanafunzi wengi wanaoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk.Joyce Ndalichako Wanafunzi wengi wanaoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Mar 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk.Joyce Ndalichako


  Wanafunzi wengi wanaomaliza elimu ya msingi mwaka huu, inahofiwa kuwa wengi wanaweza kufeli mitihani yao ya

  darasa la saba, kutokana na mfumo mpya wa usahihishaji kwa njia ya kompyuta kuwa ni mpya.
  Wakizungumza na NIPASHE, baadhi ya walimu wamesema mfumo huo mpya wa teknolojia ujulikanao kwa kama Optical Mark Reader (OMR) utafelisha wanafunzi wengi .

  Walisema kuwa masharti ya karatasi hiyo ya kujibia mtihani watatakiwa kutumia penseli maalum zijulikanazo kwa jina la (HB) na hazitakiwi kukunyika wala kuchafua kwa kuwa mtahiniwa asipofuata utaratibu wakati wa usahihishaji kompyuta haitatambua mtihani wake.

  “Kabla ya kuanza kutumia mfumo huo mpya ingebidi wanafunzi wafanye mazoezi ya kutumia karatasi hizo sisi wenyewe kwa kuwa ni walimu tulipoletewa karatasi hizo tulichemka kujibu sembuse wanafunzi inabidi utaratibu huu uangaliwe upya,” alisema Mwalimu Neema Minja wa shule ya Msingi Uwanja wa Ndege kijini Dar es Salaam.

  Ofisa elimu mmoja wa wilaya moja ya jijini Dar es Salaam alikiri kuwa mfumo huo kwa mwaka huu utasumbua wanafunzi wengi na kushauri kuwa kabla ya kutumia kwa mwaka huu wanafunzi wangetakiwa kutumia karatasi hizo wakiwa angalao darasa la sita kwa majaribio ili waweze kuzizoea kabla ya kujibu mtihani wa darasa la saba.

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala, alipongeza utaratibu huo na kusema mabadiliko hayo yanaendana na kipindi hiki cha sayansi na teknolojia na kusema siku zote mfumo mpya unapoanza kunakuwa na kasoro zake.

  Hivi karibuni, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk. Joyce Ndalichako, alisema lengo la kutumia mfumo huo ni kupunguza muda wa kusahihisha mitihani pamoja na gharama.

  Akizungumza na NIPASHE kuhusu malalamiko ya mfumo huo mpya, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema watakaa na Katibu Mtendaji waNecta kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto hiyo.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...