Rais Samia ametangaza leo Januari 29, 2026, kumteua Dkt. Rahma Salim Mahfoudh kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo atasimamia masuala ya utawala na udhibiti wa ndani wa Benki Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt Rahma Mahfoudh alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ikiwa ni takribani miezi miwili toka ateuliwe na Rais Hussein Mwinyi, November 22, 2025.
Dkt Mahfoudh anakuwa mwanamke wa tatu kushika wadhifa wa Naibu Gavana katika historia ya BOT, ambapo uteuzi wake umefuata uteuzi wa Sauda Msemo aliyeteuliwa na Rais Samia kuwa Naibu Gavana mnamo Juni 01, 2022.
Muungano unazidi kuwa imara, Rais anajitahidi kupanga vyeo katika namna inayo balance vizuri Muungano kwa pande mbili Bara na Zanzibar.