Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Vicent Mashinji jiuzulu kwa maslahi ya Upinzani Tanzania

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vicent Mashinji Ajiuzulu kwa maslahi ya Upinzani Tanzania.

Ni takriban miaka miwili sasa tangu Dr Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa zamani CHADEMA ajiuzulu wadhifa wake na kujitoa kwenye siasa za majukwaani.

Ni ukweli usiopingika kwamba wengi wa wananchi hususan CHADEMA walikasirishwa na uamuzi ule na kuonekana si wa kizalendo kwa chama chake hasa ikizingatiwa sababu aliyotoa 'eti' hakufurahishwa na ujio wa Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa ndani ya chama hicho.

Ukweli utaendelea kuwa ukweli kwamba Dr Slaa hakuutendea haki umma wa wanamageuzi Tanzania na mpaka leo dhambi ile itamwandama.

Hata hivyo kinachosababisha leo Dr Slaa aendelee kukumbukwa na CHADEMA na wanamageuzi nchini ni udhaifu mkubwa uliovuka mipaka wa Katibu Mkuu wa sasa Dr Vicent Mashinji. Ni ukweli ulio dhahiri kwamba Dr Mashinji anafaa walau kuwa Katibu wa chama mkoa lakini si nafasi aliyo nayo ya mtendaji mkuu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Dr Vicent Mashinji ameonyesha udhaifu mkubwa wa kutoa walau kauli za kisiasa za kiuongozi pale mambo makubwa yanapotokea hususan manyanyaso ya wabunge wake bungeni, kununuliwa kwa madiwani wa chama chake, kupigwa marufuku kwa shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani, kukamatwa hovyo kwa viongozi na wanachama wake nk.

Wapo wanaodhani anayepaswa kutoa sauti na kauli za kisiasa ni Mwenyekiti Freeman Mbowe lakini ukweli ni kwamba Mwenyekiti si mtendaji wa kila siku wa chama bali ni kazi ya Katibu Mkuu.

Itakumbukwa jinsi Dr Wilbroad Slaa alivyokuwa anatema cheche kukemea matendo ya serikali na serikali ilikuwa inaogopa sana. Dr Slaa anakumbukwa alivyokuwa anakutana na mabalozi mbalimbali nchini wanaowakilisha nchi zao kuelezea maovu ya serikali na habari zinaandikwa vyombo vya kimataifa.

Kwa aina ya utawala uliopo sasa CHADEMA inapaswa kuongozwa na Katibu Mkuu ambaye kila siku atakuwa anakimbia huku na huko kupigania haki ya demokrasia kwa upinzani nchini.

Wapo wanaodai Katibu mkuu huyu siyo maarufu kwa hiyo akifanya jambo hasikiki. Hilo si kweli nalo.Hii ni kwa sababu hakuna mtu aliyezaliwa akiwa maarufu. Umaarufu unaujenga mwenyewe. Tundu Lissu aliujenga umaarufu. Lema aliujenga umaarufu. Mdee anaujenga umaarufu.Mashinji akiutaka umaarufu ataupata tu hata kwa wiki moja. Amuombe Lema na Lissu wamsaidie.

Katibu Mkuu akiwa kama mtendaji mkuu wa Chama ameshindwa kutatua migogoro inayoangamiza CHADEMA katika halmashauri nyingi tunazoongoza. Kama Hajui aende kule Serengeti. Ameshindwa kusimamia pia utendaji wa Halmashauri tunazoongoza kiasi kwamba kila meya anafanya holelaholela ama anafuata Ilani ya CCM.

Ni aibu na Fedheha kubwa leo hii ngome kuu ya CHADEMA kule Arusha Inasambaratishwa. Ni aibu kuu ngome hii inasambaratishwa huku Dr Mashinji akiwa kakaa ofisini bila hata kuwajulisha wanachama akiwa kama mtendaji mkuu kuna nini kinaendelea kwenye Ngome yetu.Wanachama wamekata tamaa. Ogopa mtu aliyekata Tamaa.

Nidiriki kusema kama kuna kosa alilotenda Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe katika maisha yake ya kisiasa basi ni uteuzi wa Dr Vicent Mashinji kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA. Wapo watu waliokuwa na uwezo wa kuvaa viatu vya Dr Slaa tena wengine ni vijana wadogo tu na walau watu walishaona utendaji wao.Mfano mmoja tu ni John Heche.

Inawezekana Dr Vicent Mashinji anafaa kwa nafasi nyingine ya chini lakini si hii.Hii ya Katibu Mkuu pamoja na kwamba ni ya utendaji lakini ni ya kisiasa zaidi.Kama ameshindwa kujenga nafasi yake tangu amekabidhiwa nafasi hii basi hawezi tena. Dr Mashinji labda anafaa kuwa Katibu Mkuu wa chama kinachotawala lakini si chama cha harakati kinachotafuta kukamata dola.Labda Dr Mashinji anaogopa kufunguliwa makesi kadhaa..Lakini akumbuke Katibu mkuu makini wa upinzani jela ndiyo nyumbani kwake.

Kama Dr Vicent Mashinji akifanikiwa kusoma andiko hili basi ninalo ombi moja tu kwake. Ajiuzulu nafasi hii kwa heshima yake na heshima ya upinzani Tanzania. Ataonekana shujaa na atakumbukwa. Ila CHADEMA na upinzani ukimfia mikononi dhambi hii haitamwacha.Itamtafuna milele.
 
Naunga mkono hoja huyu Katibu Mkuu kuondolewa.
Dr Vicent Mashinji ameonyesha udhaifu mkubwa wa kutoa walau kauli za kisiasa za kiuongozi pale mambo makubwa yanapotokea hususan manyanyaso ya wabunge wake bungeni,kununuliwa kwa madiwani wa chama chake,kupigwa marufuku kwa shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani,kukamatwa hovyo kwa viongozi na wanachama wake nk.
 
Naunga mkono hoja huyu Katibu Mkuu kuondolewa.
Dr Vicent Mashinji ameonyesha udhaifu mkubwa wa kutoa walau kauli za kisiasa za kiuongozi pale mambo makubwa yanapotokea hususan manyanyaso ya wabunge wake bungeni,kununuliwa kwa madiwani wa chama chake,kupigwa marufuku kwa shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani,kukamatwa hovyo kwa viongozi na wanachama wake nk.
Huyu Mashinji amabye mlileta hoja humu kuwa ndiye katibu mkuu msomi kuliko wote duniani?
 
Huyu Mashinji amabye mlileta hoja humu kuwa ndiye katibu mkuu msomi kuliko wote duniani?
Ndiyo ni Msomi kuliko Makatibu Wakuu wote duniani lakini
Inawezekana Dr Vicent Mashinji anafaa kwa nafasi nyingine ya chini lakini si hii.Hii ya Katibu Mkuu pamoja na kwamba ni ya utendaji lakini ni ya kisiasa zaidi.Kama ameshindwa kujenga nafasi yake tangu amekabidhiwa nafasi hii basi hawezi tena.Dr Mashinji labda anafaa kuwa Katibu Mkuu wa chama kinachotawala lakini si chama cha harakati kinachotafuta kukamata dola.Labda Dr Mashinji anaogopa kufunguliwa makesi kadhaa..Lakini akumbuke Katibu mkuu makini wa upinzani jela ndiyo nyumbani kwake.
 
Ndiyo ni Msomi kuliko Makatibu Wakuu wote duniani lakini
Inawezekana Dr Vicent Mashinji anafaa kwa nafasi nyingine ya chini lakini si hii.Hii ya Katibu Mkuu pamoja na kwamba ni ya utendaji lakini ni ya kisiasa zaidi.Kama ameshindwa kujenga nafasi yake tangu amekabidhiwa nafasi hii basi hawezi tena.Dr Mashinji labda anafaa kuwa Katibu Mkuu wa chama kinachotawala lakini si chama cha harakati kinachotafuta kukamata dola.Labda Dr Mashinji anaogopa kufunguliwa makesi kadhaa..Lakini akumbuke Katibu mkuu makini wa upinzani jela ndiyo nyumbani kwake.
Mbona Mbowe haingii mtaani? Marehemu Mtikila alikuwa Mwenyekiti wa DP,hakuwa na wanasheria lakini aliingia front,jela alilala,akaishinda serikali kesi ya mgombea binafsi. Mwenye maamuzi ya chama sasa ni Lowassa,hivyo Mashinji hayupo huru kama Dr.Slaa. Kila afanyalo lazima lipewe kibali na ofisi ya mikocheni mkuu.
 
Akijiuzulu atakuja nani na atawezaje kubadili aliposhindwa huyu?

Maana siyo timu inafungwa kwa sababu lishe mbovu, mnataka kutoa utatuzi wa kubadili kocha.

Kama lishe itaendelea kuwa mbovu hata mkibadili makocha mia mtafungwa tu.

Huoni mfano tu.
 
Back
Top Bottom