MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na timu yake wabisha hodi katika vijiji vya Jimbo la Nachingwea
Kinana akizungumza na mmoja wa wananchama waasisi wa TANU, aliyejiunga mwaka 1957, Asha Kanduru (89), alipokuwa akitoka kushiriki kulima shamba kwa trekta katika shamba la Umoja Rika katika Kijiji cha Mkotokuyana, Nachingwea
Wananchi wa Kijiji cha Naipanga wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Kinana wakati akitoa hotuba fupi baada ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Serikalai ya Kijiji hicho, wilayani Nachingwea
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kulima shamba na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawekwa kutumia trekta katika shamba la Umoja Rika katika Kijiji cha Mkotokuyama katika ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wilayani, Nachingwea, Lindi
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisaidia kung'oa visiki katika shamba la Umoja la Rika baada ya kushiriki kulima kwa kutumia trekta katika Kijiji cha Mkotokuyana, wilayani Nachingwea
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akisaidia kung'oa visiki katika shamba la Umoja Rika, Nachingwea
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisaidia kuweka zege katika jengo la Ofisi ya Kijiji cha Naipanga wilayani Nachingwea.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na baadhi ya madereva wa malori waliokuwa wakilalamikia kitendo cha kucheleweshwa upakuaji wa korosho katika maghala hayo.
Wananchi wakishangilia huku wakiwa na picha ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa Mashujaa, mjini Nachingwea
Katibu Mkuu wa CCM-Taifa, Ndugu Abrahmani Kinana ameitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waliobinafshiwa viwanda nchini sanjali ili wanyang'anywe viwanda hivyo na kurudishwa kuwa mali ya umma.
Hatua hii imekuja mara baada ya Kinana kutembelea na kujionea mlundikano wa korosho na msururu wa magari ya kisubili kupakuliwa, huku moja ya kiwanda cha kubangua korosho na ufuta kikigeuzwa ghala la kuifadhia vifaa vya kusambazaia umeme.
Ndugu Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nachingwea Mkoani Lindi, ameitaka serikali kuwawajibisha viongozi au watumishi wa umma ambapo amesema serikali haipaswi kusua sua na kuogopa watu wachache hasa wenye fedha na kuwaacha mamilioni ya watanzania waliowaweka madarakani wakitaabika kupata huduma ambayo wanaitegemea baada ya kuipatia CCM ridhaa ya kuongoza nchi.
Aidha, amewataka viongozi na watendaji, kukubali kukosolewa, kukosoa na kukosoana ili kukiimarisha chama na utendaji ndani ya serikali.
Alisema ni vyema viongozi wakajenga utaratibu huo, ambao utasaidia kukijenga na kukiimarisha chama , pamoja na serikali.
Hakuna chama ambacho kimejitosheleza, hivyo mnapaswa kukosoana na kurekebishana na yule anayekosolewa asikasirike, hata mimi ninakosolewa ninapokosea, faida ya kukosoana ni kuondoa maovu ndani ya chama, hivyo, kikubwa zaidi muwe na mmeshikamana, alisema Kinana.
Alisema, CCM kinaweza kuwa chama bora duniani kutokana na kukiimarisha kwa kukosoana
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mashujaa, mjini Nachingwea, pamoja na mambo mengine, aliwahimiza wananchi kujiandikisha na kwenda kupiga kura ili wawachague viongozi wao wanaowataka kupitia CCM katika kuwaletea maendeleo.
Nape Nnauye, amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kufanya maamuzi sahihi kwa kukiweka chama hicho madarakani kuanzia ngazi za chini ili kuweza kumalizia miradi waliyoianzisha au ina tija katika maendeleo yao ya baadae.
Nape aliwaambia wananchi kuwa, vyama vya upinzani vilificha maradhi wakati wananchi walikuwa wakivieleza kuwa, vina ugonjwa wa kutokuwa na uwezo wa kupambana na Sera na Ilani za Uchaguzi za CCM kwa sababu kuanzia mwaka 1995, wananchi wengi wamekuwa wakivikataa katika sanduku la kura.
Kushindwa kwa vyama hivyo Katika chaguzi mbali mbali kulisababisha matatizo ndani ya vyama vyao ambayo yalipelekea viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kukimbia vivuli vyao na kuunda kikundi wanachokiita UKAWA.
Nape alisema, kwa sasa wameanza kuzungukana. Kuna wengine wamesambaza waraka unaowahimiza viongozi wao mikoani kuhakikisha kila nafasi ya kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Desemba 14, mwaka huu kuhakikisha wanawekwa wanachama wa chama hicho tofauti na makubaliano waliyowekeana na vyama vilivyo kwenye kikundi cha umoja huo.