Katibu mkuu wa ACT-TANZANIA aukumbusha umma juu ufutiliaji wa bunge

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
883
337
TUFUATILIE KIKAO HIKI CHA BUNGE

Ni jinsi gani rahisi tutaonyesha uzalendo wetu?

Ndugu watanzania wenzangu, Jana Jumanne Januari 27, 2015 mkutano wa Bunge umeanza mjini Dodoma. Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huo iliyotolewa na ofisi ya bunge, mbali na maswali na majibu kwa mawaziri na waziri mkuu mkutano huo pia utajadili miswaada miwili.

Miswaada itakayojadiliwa ili hatimaye iwe sheria ni mswaada wa sheria ya takwimu na mswaada wa sheria ya usimamizi wa kodi. Lakini pia Bunge litapokea na kujadili ripoti za mwaka za Kamati za Bunge. Kamati zitakazosoma ripoti ni zile za hesabu za serikali na za kisekta.

Ndugu wananchi, kwa nini ni muhimu sisi watanzania wote kufuatilia mijadala itakayokuwa inaendelea bungeni? Kwanza kabisa ni muhimu tukakumbuka kwamba wabunge wanatuwakilisha sisi. Kimsingi Bunge ni wananchi. Lakini kwa kuwa watanzania wote milioni 45 hatuwezi kukusanyika ndani ya ukumbi mmoja, ndo maana tumeçhagua wawakilishi.

Kwa sababu hiyo chochote anachokisema mbunge bungeni ni wananchi wote anaowawakilisha wamesema. Hii maana yake ni kwamba mbunge wa Mwibara kwa mfano,-akisema misamaha ya kodi ifutwe kwa manufaa ya taifa letu, hiyo inakuwa ni kauli ya wanamwibara wote.

Hivyo ni muhimu kila mtanzania akajua mbunge wake amesema nini kwa niaba yake. Kama mbunge anaongea mambo ambayo hatukumtuma na mambo yasiyo na manufaa kwetu kama Jamii, mwezi Oktoba tumweke pembeni. Hatuwezi kumjua mbunge wa namna hiyo kama hatutafuatilia mijadala yao bungeni.

Lakini pili, mambo yanayokwenda kujadiliwa yote ni mazito na muhimu kwa ustawi wa taifa letu. Wabunge watajadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha mswaada wa sheria ya takwimu. Ndungu zangu mipango yote ya maendeleo lazima itumie takwimu. Bila takwimu hakuna kitu kinaweza kupangwa na serikali kikafanikiwa, iwe ni Bajeti ama mpango wowote wa maendeleo.

Kuna mswaada wa usimamizi wa kodi. Ndugu watanzania wenzagu hili ni eneo nyeti sana. Kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2014 misamaha ya kodi imefikia trilioni 1 na bilioni 800. Hiki ni kiwango kikubwa sana cha pesa na zingekusanywa zingeweza kujenga miradi mikubwa ya maji 7,200 kama ule wa ziwa victoria unaopeleka maji mpaka Shinyanga na Kahama. Lakin pia pesa hiyo ingeweza kujenga kilometa zaidi ya laki 3 na sitini elfu nchi nzima.

Aidha Ripoti za Kamati zitatuonyesha hali ya utendaji ktk wizara, idara, wakala wa serikali serikali za mitaa na mashirika ya umma. Ni muhimu tukajua serikali yetu inafanya nini kwa ajili yetu.

Nawaalika wote tufuatilie mijadala ya mkutano huu wa Bunge tujue wawakilishi wetu wanafanya nini kwa niaba yetu.

Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania,

Samson Mwigamba,
 -KATIBU MKUU, ACT-TANZANIA
 
mmh mada mbili tofauti kwenye uzi mmoja! anyway karibia wiki inaisha nilikuwa cjaona uzi wa Act-bongo tunashukuru uwe unaiandika andka maana tutaisahau sasa tuna mambo mengi ya muhimu kushugulikia kuelekea october!
 
Back
Top Bottom