GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Katika hali inayoonyesha kuwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mtafaruku mkubwa kama siyo uadui mkubwa baina ya Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF ) na Klabu ya Yanga.
Muda si mrefu katika Kipindi cha michezo cha Clouds fm cha leo Jumapili mchana huu huu Mtangazaji alianza kumuhoji Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga kuwa nini kilitokea hadi Yanga ikashindwa kusikilizwa na CAF huku TFF ikiwepo? Majibu ya Katibu Mkuu wa TFF yalikuwa kama yafuatavyo nayanukuu " Ndugu Mwandishi wa Habari sijui mnataka sisi TFF tufanye nini ili hivi Vilabu viridhike. Tuliwataarifu Yanga mapema sana juu ya taratibu za CAF na hadi tukaenda mbele kuwataka Viongozi wa Yanga na hasa kupitia Msemaji wao waende kuhudhuria Kozi za Uongozi na Mawasiliano ambazo huandaliwa na kuratibiwa na CAF lakiki Yanga hawakuenda. Ni suala la aibu sana Mtu ambae hata hajafanya utafiti wa kutosha na hana ufahamu wa kutosha kukurupuka kwenda kubwabwaja katika vyombo vya habari kuonyesha umbumbumbu wake " mwisho wa kumnukuu Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga.
Baada ya Mtangazaji huyo kumalizana kumuhoji Katibu Mkuu wa TFF alimgeukia Msemaji wa Yanga Jerry Muro ambae leo alikuwa studioni juu ya hili na majibu ya Jerry Muro yalikuwa hivi namnukuu " Ndugu Mtangazaji kwanza nianze kwa masikitiko makubwa kwa kusema kuwa ni jambo la aibu na la kukera sana kumsikia Mtu mzima kama Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga akionyesha jinsi gani yeye sasa alivyo mbumbumbu. Kwanza nimwambie tu kuwa Mimi nina Masters Degree tena ya kutoka USA, Sweden na South Africa na sijasoma na kupata Vyeti vyangu katika hivi Vyuo vyenu vya Manzese. Na si tu kwamba nimesoma sana lakini pia kama Mwesiga anaweza alete hapa Vyeti vyake na Mimi nitoe vyangu kisha tuviweke na muweze kuona Mimi Jerry Muro na yeye Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga nani ana akili kumzidi mwenzie na tena anikome kwani naweza kuzidi kumuumbua zaidi ya haya kwani siogopi chochote kwakuwa Yanga ni Timu ya Wananchi na ni wa Kimataifa " mwisho wa kumnukuu Jerry Muro.
Kuna wale ambao huwa mnadhani nakurupuka hivyo basi kwa yoyote aliyesikiliza Kipindi cha Michezo cha Clouds fm cha kila Jumapili ambacho kimemalizika muda si mrefu atakuwa ni shahidi yangu kwa haya niliyoyaorodhesha hapa ila kwa atakayetaka kujiridhisha zaidi anaweza kwenda Clouds fm wakampe audio insert ya Kipindi hicho na haya maneno yao ya shombo yalianza kusikika Saa saba ( 7 ) na dakika 37 na kumalizika Saa saba ( 7 ) na dakika 43 na ukiona bado mgumu kuamini nenda TCRA ambao huwa wanarekodi hivi Vipindi wakupe " mzigo " kamili.
Kituko kikubwa cha aibu ambacho Msemaji wa Yanga amekifanya leo na ambacho hata Watangazaji wa zamu waliokuwepo studioni walikishangaa ni pale ambapo Jerry Muro aliposema kuwa Klabu ya Yanga ni kubwa kuliko Shirikisho la Soka barani Afrika ( CAF ) na kwamba wao Yanga kama Yanga hawatishwi kwa lolote na CAF hivyo basi maamuzi ya Yanga lazima yaheshimiwe na CAF.
Vituko vingine alivyovifanya ni vya kawaida kama vile:

- Alikuwa anang'ang'ania kuongea bila hata mpangilio hadi kuboa kipindi chote.
- Alikuwa anapata ugumu sana kuyatamka maneno ya Kiingereza japo yeye ni wa Kimataifa.
- Amelowesha sana Mic za Studio za Clouds fm hadi sasa wanahangaika kuzikausha japo hawajafanikiwa kwani alikuwa " anapovuka " sana.
- Kila akiongea alikuwa akiwasukuma na kuwapigapiga wenzie hadi kuwa " kero " kwao.