Katibu Mkuu TFF na Msemaji wa Yanga warushiana maneno mazito na ya kashfa Clouds fm

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,536
Katika hali inayoonyesha kuwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mtafaruku mkubwa kama siyo uadui mkubwa baina ya Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF ) na Klabu ya Yanga.

Muda si mrefu katika Kipindi cha michezo cha Clouds fm cha leo Jumapili mchana huu huu Mtangazaji alianza kumuhoji Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga kuwa nini kilitokea hadi Yanga ikashindwa kusikilizwa na CAF huku TFF ikiwepo? Majibu ya Katibu Mkuu wa TFF yalikuwa kama yafuatavyo nayanukuu " Ndugu Mwandishi wa Habari sijui mnataka sisi TFF tufanye nini ili hivi Vilabu viridhike. Tuliwataarifu Yanga mapema sana juu ya taratibu za CAF na hadi tukaenda mbele kuwataka Viongozi wa Yanga na hasa kupitia Msemaji wao waende kuhudhuria Kozi za Uongozi na Mawasiliano ambazo huandaliwa na kuratibiwa na CAF lakiki Yanga hawakuenda. Ni suala la aibu sana Mtu ambae hata hajafanya utafiti wa kutosha na hana ufahamu wa kutosha kukurupuka kwenda kubwabwaja katika vyombo vya habari kuonyesha umbumbumbu wake " mwisho wa kumnukuu Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga.

Baada ya Mtangazaji huyo kumalizana kumuhoji Katibu Mkuu wa TFF alimgeukia Msemaji wa Yanga Jerry Muro ambae leo alikuwa studioni juu ya hili na majibu ya Jerry Muro yalikuwa hivi namnukuu " Ndugu Mtangazaji kwanza nianze kwa masikitiko makubwa kwa kusema kuwa ni jambo la aibu na la kukera sana kumsikia Mtu mzima kama Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga akionyesha jinsi gani yeye sasa alivyo mbumbumbu. Kwanza nimwambie tu kuwa Mimi nina Masters Degree tena ya kutoka USA, Sweden na South Africa na sijasoma na kupata Vyeti vyangu katika hivi Vyuo vyenu vya Manzese. Na si tu kwamba nimesoma sana lakini pia kama Mwesiga anaweza alete hapa Vyeti vyake na Mimi nitoe vyangu kisha tuviweke na muweze kuona Mimi Jerry Muro na yeye Katibu Mkuu wa TFF Mwesiga nani ana akili kumzidi mwenzie na tena anikome kwani naweza kuzidi kumuumbua zaidi ya haya kwani siogopi chochote kwakuwa Yanga ni Timu ya Wananchi na ni wa Kimataifa " mwisho wa kumnukuu Jerry Muro.

Kuna wale ambao huwa mnadhani nakurupuka hivyo basi kwa yoyote aliyesikiliza Kipindi cha Michezo cha Clouds fm cha kila Jumapili ambacho kimemalizika muda si mrefu atakuwa ni shahidi yangu kwa haya niliyoyaorodhesha hapa ila kwa atakayetaka kujiridhisha zaidi anaweza kwenda Clouds fm wakampe audio insert ya Kipindi hicho na haya maneno yao ya shombo yalianza kusikika Saa saba ( 7 ) na dakika 37 na kumalizika Saa saba ( 7 ) na dakika 43 na ukiona bado mgumu kuamini nenda TCRA ambao huwa wanarekodi hivi Vipindi wakupe " mzigo " kamili.

Kituko kikubwa cha aibu ambacho Msemaji wa Yanga amekifanya leo na ambacho hata Watangazaji wa zamu waliokuwepo studioni walikishangaa ni pale ambapo Jerry Muro aliposema kuwa Klabu ya Yanga ni kubwa kuliko Shirikisho la Soka barani Afrika ( CAF ) na kwamba wao Yanga kama Yanga hawatishwi kwa lolote na CAF hivyo basi maamuzi ya Yanga lazima yaheshimiwe na CAF.

Vituko vingine alivyovifanya ni vya kawaida kama vile:

  • Alikuwa anang'ang'ania kuongea bila hata mpangilio hadi kuboa kipindi chote.
  • Alikuwa anapata ugumu sana kuyatamka maneno ya Kiingereza japo yeye ni wa Kimataifa.
  • Amelowesha sana Mic za Studio za Clouds fm hadi sasa wanahangaika kuzikausha japo hawajafanikiwa kwani alikuwa " anapovuka " sana.
  • Kila akiongea alikuwa akiwasukuma na kuwapigapiga wenzie hadi kuwa " kero " kwao.
Ni hayo tu na naomba kuwasilisha.
 
Masters moja inatolewa na nchi 3?

Hata Mimi nimeshangaa na kujiuliza maswali " lukuki " Mkuu. Labda nyie Wasomi wenzake mtusaidie kutufumbua hapo kuwa Je kuna Masters Degree inayotolewa katika nchi tatu? Mimi nafurahi tu anavyotenda kwani namtumia kama reference kwa Wanafunzi wangu WEREVU, WATIIFU na WAAMINIFU wa Mass Com and Journalism kuwa wasije kukosea na wao wakawa HOPELESS kama huyu Mswahili wa Yanga na nashukuru Mwenyezi Mungu kuwa wamenielewa.
 
udhaifu huu TFF imejitakia yenyewe kwa kuruhusu yanga iwe zaidi ya TFF, Yanga waliamuaru uchaguzi na yanga wakaweka wa kwao ukafanyika na wakaubariki kwa pongezai tena kupitia kwa Raisi Malinzi

mie nampongeza Murro kwa kuutumia vizuri udhaifu wa TFF

Halafu mkumbuke hapo alieanza kum- provoke mwenzie ni Katibu Mkuu Mwesiga..............
 
Aliniacha hoi aliposema eti"hatuna shida ya kucheza mechi, ila CAF wametulazimisha!" Hatujaenda kwenye kikao cha CAF kwasababu hatukubaliani na utaratibu wa mambo unavyoendeshwa!" Kwahiyo timu zote zilizohudhuria zinaendeshwa na vilaza sio?! Kichwa chwa kina walakin, na wasipoangalia kitawaingiza matatizoni!!
 
mwanzo nilianza kukuelewa. ila ulivyo maliza ni kama una uadui na MURO.

Majibu kama yako haya niliyategemea na ningeshangaa kama " msingepovuka ". Ila siku zote principle yangu itabaki kuwa ni ile ile tu ya kusema ukweli bila uwoga hata kama huo ukweli au uwazi wangu utanigharimu. Kubali kataa Jerry Muro ni TATIZO LA UELEDI na WANATAALUMA hivyo basi tuache UNAFIKI na pengine Mimi kumsema kwangu mara kwa mara nikawa namsaidia ajitafakari upya kuliko nyie mnaojifanya KUMPENDA kumbe MNAMPONZA.
 
Ulianza vyema ila ume maliza na bias kubwa sana

Writer mzuri wa hasa maoni lazima akiwa anamalizia aonyeshe upande wake. Nenda shule kajifunze vizuri rules za a good opinion writer kisha urudi tena kwangu uniambie kama nipo sahihi au nimekosea. Hivi huko Universities huwa mnakwenda kufanya nini kama jambo dogo tu hili la Kiuandishi linakutesa na kukusumbua hadi " unapovuka " hivi?
 
Nimemdharau Jerry Muro pale aliposema TFF wameuza kinyemela haki za tv, wakati haki za matangazo ziko chini ya CAF
 
Majibu kama yako haya niliyategemea na ningeshangaa kama " msingepovuka ". Ila siku zote principle yangu itabaki kuwa ni ile ile tu ya kusema ukweli bila uwoga hata kama huo ukweli au uwazi wangu utanigharimu. Kubali kataa Jerry Muro ni TATIZO LA UELEDI na WANATAALUMA hivyo basi tuache UNAFIKI na pengine Mimi kumsema kwangu mara kwa mara nikawa namsaidia ajitafakari upya kuliko nyie mnaojifanya KUMPENDA kumbe MNAMPONZA.
kwaiyo umeona wakiwa wanafuta mc huko studio?
 
Majibu kama yako haya niliyategemea na ningeshangaa kama " msingepovuka ". Ila siku zote principle yangu itabaki kuwa ni ile ile tu ya kusema ukweli bila uwoga hata kama huo ukweli au uwazi wangu utanigharimu. Kubali kataa Jerry Muro ni TATIZO LA UELEDI na WANATAALUMA hivyo basi tuache UNAFIKI na pengine Mimi kumsema kwangu mara kwa mara nikawa namsaidia ajitafakari upya kuliko nyie mnaojifanya KUMPENDA kumbe MNAMPONZA.
Punguza bias kumbe umekuwa uki deal naye mara kwa mara ee!!?

Waajiri wake wakiona hafai wata mtoa, huna haja ya kumpinga kias hko

Ulianza vema ila ume maliza kwa bias kubwa sanaa na ndo ulipo haribu
 
Aliniacha hoi aliposema eti"hatuna shida ya kucheza mechi, ila CAF wametulazimisha!" Hatujaenda kwenye kikao cha CAF kwasababu hatukubaliani na utaratibu wa mambo unavyoendeshwa!" Kwahiyo timu zote zilizohudhuria zinaendeshwa na ****** sio?! Kichwa chwa kina walakin, na wasipoangalia kitawaingiza matatizoni!!

Nikisema Mimi humu JF naonekana nina CHUKI nae labda sasa umesema Wewe wanaweza kuelewa. Jamaa ni TATIZO na AIBU mbele ya Wastaarabu.
 
87.5. The television and broadcasting rights, as well as the revenues from publicity belong exclusively to CAF and shall be distributed as follows:

- 50% for the eight finalist countries,
- 30% for the organising country,
- 20% for CAF,

87.3. The television, broadcasting and publicity rights of the draw ceremony of the final tournament belong to CAF. They shall be subject to a separate contract and freely 35 negotiated between CAF and the various specialized agencies.

87.4. The organising associations shall see to it that the commitments taken by CAF in the contracts signed with the specialized agencies are fully observed on its territory. The organising association must present the consent of its Government in this respect. The organising association is bound to facilitate the task of the specialized agencies all through the Tournament.

Article 89 The organising association shall see to it that the commitments taken by CAF as indicated in the contracts concluded between the Confederation and the agencies are fully observed in its territory
Nimemdharau Jerry Muro pale aliposema TFF wameuza kinyemela haki za tv, wakati haki za matangazo ziko chini ya CAF
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom