Katibu Mkuu (Mifugo) okoa maisha ya wana UDOM

Katibu Mkuu (Mifugo) okoa maisha ya wana UDOM

maseyu

Member
Joined
Oct 31, 2016
Posts
39
Reaction score
64
Wadau poleni na majukumu na pongezi kwa ufanisi. Kuna jambo ambalo sidhani kama mamlaka zinazousika zipo makini na afya za wananchi wa hali ya chini!

Katika eneo la kata ya Ng'ong'ona ambayo ipo katika jiji la Dodoma karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Dodoma kuna machinjio ambayo kama mamlaka zinazohusika hazitachukua hatua mapema ipo siku tutaweka matanga.

Machinjio hii ni chafu sana na mbaya zaidi ipo kwenye makazi ya watu, harufu kali inayotoka katika machinjio hii inaishia kwenye nyumba za wananchi walala hoi, simply kwa sababu mwenye machinjio ni dawani wa kata husika.

Katika machinjio hii ndipo ambapo nyama zinazopikwa katika eneo la wajasi zinatoka, ni kawaida hata wakati wa mchana kushuudia ng'ombe wakichinjwa,swali ni je utaratibu wote wa kitaalum kuhusu nyama unafuatwa? Jibu ni no.

Katibu Mkuu (Mifugo) ingilia kati jambo hili ili kuokoa maisha ya wana chuo na wananchi kwa ujumla.

20190812_171940.jpeg
20190812_171813.jpeg
20190812_171745.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri hii moja ya machinjio bora sana nchi hii na safi. Nafikiri hujazunguka kuona hali ya machinjia zetu
Niliwahi kwenda Vingunguti kabla ya ujenzi wa Sasa...aisee,niliwahurumia wale eanajidai wananunua nyama mabucha ya Masaki,
 
Poleni sana,Ni vingi tunavyokula ni Mwenyezi Mungu ndio anayetunusuru
 
Back
Top Bottom