Dkt. Bashiru: Kuanzia sasa CCM haitatumia wasanii wa Bongo Fleva kwenye mikutano yake tutabaki na bendi yetu ya TOT

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
230ECD7A-2FF5-4359-8C38-EF29FDBFEBFC_w1200_r1_s.jpg




Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa chama hicho hakitawatumia wasanii tofauti na bendi ya TOT na Vijana katika shughuli zote za chama hicho.

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza kuu la vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) jijini Dodoma ambapo amesema kuwa watafanya hivyo ili kupunguza gharama zinazokigharimu chama hicho pindi inapowalipa wasanii.

"Kuanzia sasa CCM haitatumia wasanii wa Bongo Fleva kwenye mikutano yake tutabaki na bendi yetu ya TOT. Tukienda mikoani tutawakuta wasanii wa nyimbo za asili, tunafanya hivi kupunguza gharama", amesema Dkt. Bashiru

Bendi ya TOT ilijizolea umaarufu kutokana na aliyekuwa mtunzi na muimbaji wake Kapteni John Komba ambaye kwasasa ni marehemu kuwa na mashairi yanayovutia na kuhamasisha wanachama pindi CCM inapokuwa kwenye kampeni.
 

Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally akifungua kikao cha Baraza kuu la UVCCM jijini Dodoma amesema "Kuanzia sasa CCM haitatumia wasanii wa Bongo Fleva kwenye mikutano yake tutabaki na bendi yetu ya TOT''.

> Tukienda mikoani tutawakuta wasanii wa nyimbo za asili, tunafanya hivi kupunguza gharama".
Yatamtokea puani huyu..... Hawajui fisiemu vizur

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally akifungua kikao cha Baraza kuu la UVCCM jijini Dodoma amesema "Kuanzia sasa CCM haitatumia wasanii wa Bongo Fleva kwenye mikutano yake tutabaki na bendi yetu ya TOT''.

> Tukienda mikoani tutawakuta wasanii wa nyimbo za asili, tunafanya hivi kupunguza gharama".
Katika kitu kigumu ambacho CCM hawawezi kukikwepa ni wasanii, kwani bila wasanii mikutano ya CCM hakuna muhudhuliaji
 
naweza kusema wengi wa hao wasanii ni 'wajinga kweli kweli' wakati wa chaguzi huwa wanajipendekeza pendekeza kwa ccm, nayo ikisha watumia kama condom inawa tupilia mbali mwisho wa siku wanamuomba Sugu atete maslahi yao bungeni, ***** zao!
 
Katika Chaguzi za Marudio ,Baada ya mbinu zao za Kupita bila kupingwa na Kuiba kura Kufanikiwa kwa 100% sasa ni Wazi hawahitaji Bongo fleva..
2020 Wanauhakika wa Kushinda.Majimbo yote wanayoshikilia na Ziada.
 
Back
Top Bottom