Katibu Mkuu CCM, Abdurahman Kinana, kimya kimezidi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Tuna kila sababu ya kujua afya ya viongozi wetu ikiwa ni pamoja na kuwaombea dua kwa afya na hekima katika kutuongoza.

Imekuwa ni muda sasa toka mtukufu rais amtume katibu mkuu wa CCM kwenda kutibiwa India kwa muda wa siku 14, hakuna taarifa ya afya yake toka amekwenda, tupenda kujua taarifa za afya yake ili kuonyesha mshikamano kwa viongozi wetu wanapokuwa wagonjwa au wazima pia.

Hivyo basi tunakishauri chama kuweka utamaduni wa kujua afya za viongozi wetu ukizingatia tuliambiwa ametumwa kwa siku 14 na sasa zimekwisha pita hatujapata taarifa.
 
Waitakia nini?? Alipoondoka kwa kutii kutumwa India aliaga?? Kama hakuaga pia akirudi hatatangaza. Amini viongozi wako weye, hali ingelikuwa mbaya tungeambiwa
 
Waitakia nini?? Alipoondoka kwa kutii kutumwa India aliaga?? Kama hakuaga pia akirudi hatatangaza. Amini viongozi wako weye, hali ingelikuwa mbaya tungeambiwa
Kwa nini tusimuulizie ilhali ni kiongozi aliyethubutu kusema ukweli na kuitoa CCM kwenye kiza kinene!
 
Kwa nini tusimuulizie ilhali ni kiongozi aliyethubutu kusema ukweli na kuitoa CCM kwenye kiza kinene!

Mkuu;
Kama ni ukweli, mbona tena imekuwa fumbo?? Utaje ukweli alousema kuwa ulikuwa ni hivi na hivi. Hamkosi cha kuchokonolea hoja
 
Ni kweli alitumwa na M/kiti wake kwenda kutibiwa India kwa siku 14 lakini zimezidi ndiyo maana tunaulizia afya yetu
 
Aah jamani kuna india huko canada au kwa sababu wahindi wengi wako canada ndio mnafikili kuna mji unaitwa india no,kama alikuwa na tikiti ya india basi alionekana canada huko akipiga self huko mitaani hata hivyo hatukuona umuhimu wa kuwambia amerudi kwa sababu tulijua tu mtauliza hehehe!!
 
Ukisikia kukurupuka ni hivi ufanyavyo.

WATANZANIA ewe MUUMBA hebu tupe busara ya kuweza kufikiria na kusema wenye, bila kuendeshwa kama gari la remote. tuepushe na ujinga huu wa kuendeshwa kwa remote control tena zilizo kwisha charge.

Pole sana ndugu yangu, wiki ya jana alikuwa pale Lumumba na aliwaambi watu hakwenda India wala Canada bali alikuwa uingereza .

Sasa kama huko totally mentali controlled basi utaamini la zivyo endelea kugonga miamba.
 
Lengo la kutumwa ni kwenda kutibiwa na kwa kuwa tulitaarifiwa kutumwa kwake na kama kweli amerudi watuambie kuwa amerudi na majibu yake ni haya,huo ndiyo uungwana
 
Back
Top Bottom