Katibu mkuu asalimu amri

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, hatimaye amesalimu amri na kurejesha gari, mali ya Serikali alilojimilikisha akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa, Kanda ya Mbeya.

Gari hilo – Toyota Land Cruiser VX V8 – lenye namba STK 8299, ni mali ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, lakini Dk. Ulisubisya, akijua halina tatizo lolote la kiufundi, alijimilikisha kinyume cha maadili na kanuni za uhamishaji mali za umma kwenda kwa mtu binafsi.

Hata hivyo, vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Waze na Watoto, zinasema kuna mikakati mahsusi imeandaliwa, ikiwa ni pamoja na kughushi nyaraka, ili ionekane kuwa gari hilo halikuwa mkononi mwa Dk. Ulisubisya, isipokuwa lilikuwa kwenye matengenezo jijini Dar es Salaam.

Transport Officer ni ndugu yake, wanahaha ili ionekane gari lilikuwa gereji, jambo ambalo ni uongo. Gari alishafanya taratibu zote za kulimiki na ndiyo maana likaondolewa Mbeya na kuletwa hapa Dar es Salaam,” kimesema chanzo hicho.

Katika hatua nyingine,Dk. Ulisubisya, anaelezwa kuwa hajakata tamaa kulitwaa gari hilo; na kwamba ndiyo maana limerejeshwa Mbeya, lakini limezuiwa lisitumiwe.

Gari hilo ambalo liko katika hali nzuri, lilinunuliwa mwaka 2012 kwa ufadhili wa asasi ya Walter Reed Program ya nchini Marekani. Thamani yake ilikuwa zaidi ya Sh milioni 280, lakini taarifa ambazo bado zimefanywa siri zinasema Dk. Ulisubisya alilipata kwa kiwango kisichozidi Sh milioni 15.

Chanzo cha habari kimesema: “Taarifa kuhusu gari hilo zilighushiwa kwa kushirikiana na Transport Officer wa Wizara ya Afya na kuonesha kuwa gari hilo ni chakavu na bovu kabisa.

“Ofisi ya Rais, Idara Kuu ya Utumishi imeidhinisha alinunue kwa mkopo baada ya kudanganywa kuwa ni chakavu. Alilinunua huku akiacha Hospitali ya Mbeya ikiwa haina gari mbadala, wafadhili wamesikitishwa mno na kitendo hicho,” kimesema chanzo cha habari.

Chanzo: Jamhuri
 
Haya yoote ni muendelezo wa LUGUMI tu majipu makubwa yaliyoiva vizuri hayaguswi wala kuapasuliwa, mpasuaji anaimba nyimbo nyingine za kushughulikia vicpele,.
 
Mwacheni Dokta apate naye gari hilo...hamtosheki kwa kazi alizofanya hapo Mbeya (Hospital Imependeza)
 
Kwa jinsi ulivyoleta mada na sharia hizi za mtandao, naamini ulichoandika ni kweli, huwezi kuja kupakazia. SASA HII ITAGUSWA na hata ikisemwa bungeni tutaisikia au wamefunga mapazia. Kuisikia baadae haina utamu MANA ITAKUWA IMEKATWA kwa kisingizio cha muda. Hapa tumenyimwa KITU
 
Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka hivyo hatua stahili zichukuliwe dhidi yake.
 
Back
Top Bottom