mbona umeleta habari nusu?,habari yote hii hapa " Mwalimu Olouch aliitoa kauli
hiyo juzi kwenye kongamano la
walimu Kitengo cha Wanawake
Manispaa ya Dodoma kuwa,
Profesa Dk Ndalichako anapaswa
kushtakiwa.
Habari
SUNDAY, MARCH 6, 2016
Katibu CWT amjia juu
Prof Ndalichako
0.8k 0 0
0 0 0 0.8k
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce
Ndalichako.
By Habel Chidawali, Mwananchi
hchidawali@mwananchi.co.tz
Dodoma. Naibu Katibu Mkuu wa
Chama cha Walimu Tanzania (CWT),
Mwalimu Ezekiel Olouch amesema
upangaji matokeo ya kidato cha nne
kwa mfumo wa divisheni uliofanywa
na Wizara ya Elimu, ni batili na
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
anatakiwa kushtakiwa.
Mwalimu Olouch aliitoa kauli hiyo
juzi kwenye kongamano la walimu
Kitengo cha Wanawake Manispaa ya
Dodoma kuwa, Profesa Dk
Ndalichako anapaswa kushtakiwa.
Pia, alipinga suala la kutumbua
majipu kwani linakwenda kinyume
na haki za binadamu.
“Mambo mengi yanafanywa kwa
pupa hasa yanayofanywa na
manaibu waziri, na baadhi ya wakuu
wa wilaya nchini,” alisema Mwalimu
Olouch.
Kuhusu matokeo ya kidato cha nne
yaliyotangazwa Februari, alisema
kitendo cha waziri kuamua kufuta
mfumo wa GPA na kurudisha
divisheni, kilikuwa kizuri lakini
aliufanya kwa kukurupuka.
Mapema mwaka huu akiwa mjini
Dodoma, Profesa Ndalichako
alitangaza kubadilisha mfumo wa
matokeo kutoka GPA kurudi wa
zamani wa divisheni ikiwa ni wiki
chache kabla ya kutangazwa kwa
matokeo hayo.
“Hapa tuelezane ukweli kwamba
Ndalichako amevunja sheria na mimi
ningekuwa na mtoto aliyemaliza
kidato cha nne mwaka jana, lazima
ningemfikisha mahakamani
haiwezekani kuwa na elimu ya
kukurupuka, kitaaluma ni matokeo
feki lakini kisiasa ni matokeo halali,”
alisema Mwalimu Oluoch.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo,
Waziri anaruhusiwa kubadilisha
lakini lazima aaandike kanuni na
mwongozo jambo alilodai
halikufanyika.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa
Dodoma, Augustino Njamasi alimtaka
chama kuendelea kupigania masilahi
ya walimu ikiwamo madeni.