Katibu CWT: Ndalichako anapaswa ashitakiwe haraka

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
Katibu CWT amjia juu Prof Ndalichako

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Ezekiel Olouch amesema upangaji matokeo ya kidato cha nne kwa mfumo wa divisheni uliofanywa na Wizara ya Elimu, ni batili na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako anatakiwa kushtakiwa.

Mwalimu Olouch aliitoa kauli hiyo juzi kwenye kongamano la walimu Kitengo cha Wanawake Manispaa ya Dodoma kuwa, Profesa Dk Ndalichako anapaswa kushtakiwa.
 
kivipi??huyo naye kachanganyikiwa???....aende zake huko..wao ndo wanatakiwa washitakiwe kwa kula pesa za walimu bila kuhojiwa.....
 
alikuwa wapi muda wote huo wakatik ndalichako anatoa siku 7 kwa baraza kueleza ni kwanini walibadili mfumo wa utoaji matokeo??walipo kaa kimya ndo akaagiza watoe kwa division kama hawakuwa na sababu..kwa nini asinge wasaidi baraza kutoa hizo hoja kwa ndalichako..mbafuuuuuuuuuuuuu
 
Ashitakiwe kwa kosa gani?
Kama mlikuwa hamfundishi mtaaibika tu
Tumefurahi magufuli kumweka huyu mama hapa, hata mitihan hatutasikia kuvuja sasa
 
Huyu mzee bana, ngoja waje hapa watueleze mapungufu yake maana alikuwa mjumbe wa bodi ya NHIF iliyovunjwa
 
mbona umeleta habari nusu?,habari yote hii hapa " Mwalimu Olouch aliitoa kauli
hiyo juzi kwenye kongamano la
walimu Kitengo cha Wanawake
Manispaa ya Dodoma kuwa,
Profesa Dk Ndalichako anapaswa
kushtakiwa.
Habari
SUNDAY, MARCH 6, 2016
Katibu CWT amjia juu
Prof Ndalichako
 0.8k   0  0
 0  0  0  0.8k
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce
Ndalichako.
By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
Dodoma. Naibu Katibu Mkuu wa
Chama cha Walimu Tanzania (CWT),
Mwalimu Ezekiel Olouch amesema
upangaji matokeo ya kidato cha nne
kwa mfumo wa divisheni uliofanywa
na Wizara ya Elimu, ni batili na
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
anatakiwa kushtakiwa.
Mwalimu Olouch aliitoa kauli hiyo
juzi kwenye kongamano la walimu
Kitengo cha Wanawake Manispaa ya
Dodoma kuwa, Profesa Dk
Ndalichako anapaswa kushtakiwa.
Pia, alipinga suala la kutumbua
majipu kwani linakwenda kinyume
na haki za binadamu.
“Mambo mengi yanafanywa kwa
pupa hasa yanayofanywa na
manaibu waziri, na baadhi ya wakuu
wa wilaya nchini,” alisema Mwalimu
Olouch.
Kuhusu matokeo ya kidato cha nne
yaliyotangazwa Februari, alisema
kitendo cha waziri kuamua kufuta
mfumo wa GPA na kurudisha
divisheni, kilikuwa kizuri lakini
aliufanya kwa kukurupuka.
Mapema mwaka huu akiwa mjini
Dodoma, Profesa Ndalichako
alitangaza kubadilisha mfumo wa
matokeo kutoka GPA kurudi wa
zamani wa divisheni ikiwa ni wiki
chache kabla ya kutangazwa kwa
matokeo hayo.
“Hapa tuelezane ukweli kwamba
Ndalichako amevunja sheria na mimi
ningekuwa na mtoto aliyemaliza
kidato cha nne mwaka jana, lazima
ningemfikisha mahakamani
haiwezekani kuwa na elimu ya
kukurupuka, kitaaluma ni matokeo
feki lakini kisiasa ni matokeo halali,”
alisema Mwalimu Oluoch.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo,
Waziri anaruhusiwa kubadilisha
lakini lazima aaandike kanuni na
mwongozo jambo alilodai
halikufanyika.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa
Dodoma, Augustino Njamasi alimtaka
chama kuendelea kupigania masilahi
ya walimu ikiwamo madeni.
 
Hao watu wa kawambwa acheni mama apige kazi mlikua mnatudanganya mwanao kafaulu eti kapata credt mara sijui merit cjui nn mnatuficha tu ni bora wafaulu wachache ambao umma unaamini kua kweli wamefaulu sio kufichaficha tu. Huyu bilashaka alinufaika na vikao vya kupongezana na kawambwa kwamba brn imetekelezw
 
Hakuna kitu, hakuna hata cha maana alichoongea huyo mwl. Inawezekana madai yake yakawa ya msingi ila kashindwa kuweka point za maana
 
HUYU JAMAA WIKI HIZI MBILI TATU VYOMBO VYA HABARI VINAMPA AIRTIME YA KUTOSHA
 
Hivi huyo Ezekiel Olouch amechanganyikiwa nini?Wamwache apige kazi Waziri wetu Ndalichako kanyaga tender!!!
 
Ni jirani yangu Kinyerezi Dar es salaam...namjua vizuri huyu bwana. Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa ikitumika kwake hasa kifungu kinachohusu kumiliki mali zisizoelezeka chanzo chake.... Atakufa kwa presha kabla ya kufika mahakamani
 
Ni ukweli usiopingika waziri amekurupuka coz hayo mabadiliko ameyafanya wakati mtihani umeshafanyika, kweli mfumo wa GPA ulikuwa sio mzuri lkn angefanya mabadiliko hyo may be mwakani hicho alichokifanya ni uonezi kwa wahitimu mm naona katibu wa cwt yuko sahihi ameharibu mwelekeo haya matokeo ni batili kabisa! mfumi wa division ni mzuri lkn angetulia kwanza co kukurupuka!
 
lakini mbona waziri ndalichako alitoa Siku 7 za kwann mfumo wa G.P.A uendelee badala ya Division, mbona hakujitokeza??
 
CWT wezi wakubwa, hiyo ndo kazi yao? aubwanajisahaulisha majukumu yao?
 
Back
Top Bottom