Katibu CUF Arumeru ajivua uanachama

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika hatua nyingine, mpasuko ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umezidi kuendelea baada ya katibu wa chama hicho wilaya ya Arumeru, Hamis Juma Kieni kujiengua katika chama hicho na kujiunga na NRA na jana, alirejesha fomu ya kugombea.

Akizungumza na Mwananchi, Kieni alisema ameamua kujiondoa CUF na kujiunga na NRA baada ya kuona chama hicho, kinatangaza kutosimamisha mgombea bila kuwasiliana na uongozi wa wilaya.

"Mimi nilikuwa nimeweka nia ya kugombea ubunge ila ghafla chama changu kikatangaza kutosimamisha mgombea, nikaona chama sasa kinapoteza mwelekeo na kinaelekea kufa sasa kwanini hawakuwasiliana na sisi na hivyo nikajivua uanachama,"alisema Kieni.

Source:Mwananchi
 
Yaani wewe John Mrema, hiyo ndio Feasibility Study uliyotumia 19M?
Kama huna kazi ya maana rudi nyumbani tu!
 
kahamia NRA?yaani badala ya kujizika tu yakaisha, ameamua kujichoma moto kabisa, sasa CDM si ipo jamani kwa nini ajiongezee tress
 
Back
Top Bottom