uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 2,087
- 2,993
Habarini za leo wadau,
Kwa kawaida bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,linafanya kazi ya kutuwakilisha wananchi
kwa sababu hatuwezi watu wote kwa ujumla wetu kwenda kutunga sheria za nchi au majukumu mengine yanayo fanywa na bunge.Tunahusika kwa njia ya kuchagua wawakilishi wetu ambao ni wabunge.
Swali langu linakuja kwenye utaratibu mzima uliotumika kuandaa katiba mpya. Wajumbe walitumia pesa nyingi
wakatembelea mikoa yote kukusanya maoni ya kuwekwa au kutengeneza katiba mpya.Kwa mantiki hiyo
maoni yaliyotolewa na wananchi wa mikoa yote ni uwakilishi wao wa nini wanakitaka na nini hawakitaki. Tume iliratibu na kuandika hayo maoni kama katiba pendekezwa. Ni kwanini baada ya hapo liliundwa bunge la katiba?
Kwa maoni yangu naona hapo ndo ulikuwa mwanzo wa kutufanya hadi leo tusipate katiba mpya.
Napendekeza,kwa vyovyote inavyoweza kutokea,katiba ile ya jaji Warioba,ambayo ndio mapendekezo ya wananchi ambapo walipewa nafasi ya kujiwakilisha wenyewe,iheshimike iwe katiba ya Tanzania,kama ilivyoratibiwa na tume.
ile iliyoandikwa na bunge la katiba itupiliwe mbali kwani hakukuwepo na haja ya kuongeza/kupunguza maneno juu ya maneno ya wenye nchi.
Nawasilisha.