Katiba ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JACADUOGO2., Aug 7, 2012.

 1. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza naomba itambulike wazi kuwa watanzania wengi wamekubali mabadiliko na wanahitaji pa kupatia mabadiliko na matumaini ya kweli.

  Watu wengi sana sasa wanahitaji Katiba za CHADEMA kwa udi na uvumba lakini cha kusikitisha ni kwamba katiba za CHADEMA hazipatikani mpaka kudownload kwenye internet wakati watanzania walio wengi hasa maeneo ya kule kwetu kijiji cha Ochuna watu hawana habari na mambo ya internet.

  Ombi langu ni kuwa chama kitafute kampuni ili itengeze katiba nyingi ili ziuzwe kwa wadau kwani zinahitajika kwa gharama yoyote. Kwa mfano Mwanza na Musoma katiba hazipatikani kabisa! Naomba kutoa hoja.

  Jacaduogo - Diwani mtarajiwa wa kata ya Nyahongo (CHADEMA)!
   
 2. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwani JF ndio uongozi wa CDM? Nenda makao makuu au wapigie simu uwaeleze na sio kutuletea ***** wako hapa.
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hao watu wanaotaka katiba waambie kama wanataka kujiunga wajiunge tu, wasingoje katiba, kwa sababu maamuzi ya CHADEMA yanafanyika kimagumashi bila kufuata katiba, si umeona matawi yanafunguliwa nje ya nchi? hakuna sehemu kwenye katiba inaruhsu hilo jambo. Si umeona watu wanakatazwa kugombea uenyekiti kwasababu "they are from nowhere", hilo jambo halipo kwenye katiba etc
   
 4. m

  mamajack JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu,bado kunatatizo la upatikanaji wa vifaa vya chama,na personally nimeenda makao makuu nikauziwa katiba chache kuliko nilizokuwa nataka.i hope wahusika wanasikia.vifaa vya cdm viko highly demanded,ila pia ni kuwa makini kwenye utoaji maana jeshi la nape lipo kazini kuharibu.
   
 5. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Rudi dampo mapema; matembezi ya inzi ni mchana.
   
 6. m

  mob JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  mkuu kwenye website yao kuna kila kitu,kwa kuwa unataka kuelimisha watu na ninaamini chama hakina fedha za kutosha download then make copy za kutosha the samabaza kwa watu.mbona unatoaaga raundi za bia kibao fanya na kutoa copy.ili kupata maendeleo na sisi tunatakiwa tuchangie fedha zetu mda wetu na nguvu kazi zetu
   
 7. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Diwani mtarajiwa asiyetaka hata kujifunza namna ya kuwasiliana na chama anachotaka kukitumia kama chombo cha kupata nafasi ya kuwatumikia watu!!!!! Du!
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Chadema hichi Chama ni cha magumashi kimetumia miaka 50 lakini reli iliyowekwa na wakoloni hawajaiongeza hata kipande lazima 2015 chadema iondoke madarakani kwasababu imeshindwa kutumia government printers kuprint katiba yake
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  kwa namna chama kinavyozunguka nchi nzima kutafuta wanachama wapya, na maoperation kibao, sikutegemea jibu kama hili kutoka kwa afisa habari wa cdm! Umeona ugumu gani kumwelekeza namna rais ya kuzipata hasa ukizingatia ni mwanachama tena anayetegemea kuwa kiongozi? Kama ni njia ya mawasiliano, mbona tumekuwa tukiwasiliana na viongozi wengi tu wa ngazi za juu wa vyama ikiwemo cdm? Very dissappointing answer from a right person!
   
 10. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tumaini Makene,

  Sijakuelewa na sijui unamaanisha nini? Nimeenda kwenye ofisi za CHADEMA kuanzia ngazi ya wilaya hadi Mikoa (Mwanza na Musoma) sijapata Katiba! Sasa naomba unipe hiyo njia rahisi ya mawasiliano ili nipate nakala za Katiba na UZINGATIE kuwa niko kijijini Shirati Rorya naendelea na ujenzi wa chama.

  Nafahamu vizuri nafasi yako Mr. Makene katika chama lakini unaponishangaa badala ya kujibu tatizo langu nashindwa kukuelewa. Jaribu kusoma hoja yangu kwa umakini sana na utambue mazingira niliyopo kamanda.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...