Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,348
- 26,144
Kumekuwa na mijadala isiyokoma kuhusu uchaguzi mkuu ndani ya CHADEMA. Lakini,mijadala mingi imejaa ushabiki,'unazi' na upofu wa sheria inayosimamia uchaguzi huo ndani ya chama. Kama mtanzania mpenda demokrasia nisiye na chama chochote,nimeona heri kudurusu Ibara za Katiba ya sasa ya CHADEMA (humu nitaiita Katiba) inayogusia muda wa uongozi ndani ya chama hicho.
Kwanza, kuna Ibara ya 6.3.2 ya Katiba inayotoa kipindi cha miaka mitano kwa uongozi unaochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu. Ibara husika inasomeka hivi:
6.3.2 Muda wa Uongozi
[FONT=Arial,Arial][FONT=Arial,Arial](a) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Chama utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano.
Pili, Ibara hiyo hiyo ya 6.3.2, katika kifungu (d) inatoa mwanya kwa Mamlaka iliyochhagua au kuteua Uongozi uliopo madarakani kufupisha muda wa uchaguzi. Hapa,kadiri ya uelewa wangu, kuna maana kuwa uchaguzi Mkuu waweza kuitishwa kabla ya miaka mitano husika. Kifungu husika (d) cha Ibara ya 6.3.2 kinasomeka:
(d) Muda wa uongozi unaweza kufupishwa kama mamlaka iliyochagua au kuteua itaamua hivyo.
Hii ina maana kuwa Mamlaka iliyoteua Kamati Kuu,kwa mfano, yaweza kufupisha muda wa Kamati Kuu. Hatahivyo, taratibu nyingine za kawaida za kichama kama vikao husika na sababu za kufanya hivyo lazima ziwepo. Ieleweke kuwa, Ibara ya 6.3.2 (d) inaruhusu Mamlaka fulani inayohusika na uchaguzi au uteuzi wa uongozi fulani ndani ya chama,kufupisha muda wa uongozi huo tu. Si vinginevyo.
Tatu, kuna Ibara ya 6.3.3 ya Katiba. Hii inazungumzia kurekebishwa kwa tarehe ya Uchaguzi ndani ya chama. Hapa,hasa, panazungumziwa kurefusha/kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi ndani ya chama. Kamati Kuu ya chama ndiyo iliyopewa mamlaka ya kurekebisha tarehe ya uchaguzi. Kwa uelewa mzuri,naweka hapa Ibara ya 6.3.3 kama ilivyo.Hatahivyo,Ibara ya 6.3.3 (a) na (b) ni muhimu zaidi. Inasomeka:
6.3.3 Kurekebisha tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Chama
[FONT=Arial,Arial][FONT=Arial,Arial](a) Tarehe ya uchaguzi mkuu wa Chama inaweza kurekebishwa kwa kusogezwa mbele kwa muda usiozidi mwaka mmoja toka mwisho wa uhalali wa uongozi uliopo.
(b) Mamlaka ya kufanya marekebisho haya yameachiwa Kamati Kuu
(c) Kamati Kuu ndiyo itapanga tarehe ya uchaguzi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee wa Chama.
Itoshe kusema kuwa mijadala na matamko yote yahusuyo uchaguzi ndani ya CHADEMA yaongozwe na uelewa wa Ibara hizo zilizotajwa hapo juu. Kinyume na hapo,ni kujadili na kutamka kwa upofu na upotofu .
[/FONT][/FONT]
[FONT=Arial,Arial][FONT=Arial,Arial][/FONT][/FONT]