KATIBA: Wazee wa CCM wampongeza JK

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Tanzania kweli kuna mambo, yaani hilo linchi sijui ni laana???????


Wazee wa CCM wameza shubiri ya katiba!


ccmwazeekatiba.jpg

Source: Hapa

Tuesday, 04 January 2011 21:15



Katibu mtendaji wa baraza la wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mtulia (kulia), akisoma tamko la baraza hilo jijini Dar es Salaam jana kuhusu kuunga mkono tamko la Rais Kikwete la kuanza kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Athumani Mwinyimvua. Picha na Said Powa

Raymond Kaminyoge
BARAZA la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, limempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kukubali kuandikwa upya kwa katiba ya Tanzania, huku wakilaani nguvu kubwa iliyotumika kumshinikiza akubaliane na suala hilo.
Wazee hao, wengi wakiwa ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walieleza msimamo wao huo jana jijini Dar es Salaam walipokutana na waandishi wa habari.
Tamko hilo lililojaa shutuma dhidi ya makundi ya watu yaliyomshinikiza Rais Kikwete hadi kufikia hatua hiyo, lilisomwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo ambaye pia ni mwanachama wa CCM, Mohamed Mtulia.

Kitendo cha baraza hilo kuwabeza kwa kuwalaani wale walioongoza mjadala wa kudai katiba mpya, kinatafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya siasa kuwa ni wazee hao kwa upande mwingine kutofurahishwa na hatua Rais Kikwete kukubali suala hilo. Baadhi ya vyombo vya habari (siyo Mananchi) tayari vimeripoti kuwepo wahafidhina ndani ya CCM ambao hawakufurahishwa na hatua ya rais kuruhusu kuanza kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Katika mkutano huo wa jana, Mtulia alianza kusoma tamko hilo kwa kumwagia sifa Rais Kikwete akisema kama baraza, wamefurahishwa na hatua aliyoichukua kuhusu mjadala wa katiba. “Baraza la wazee kwa niaba ya wazee wenzetu tumeamua kutamka hadharani kuwa tumefurahishwa na uamuzi wa Rais Kikwete kwa kukubali kuandikwa katiba mpya,”alisema Mtulia.

Mbali na kumpongeza Rais Kikwete kwa hatua hiyo, Mtulia akaonya kuwa katika kufikia suala hilo, isitumike jazba, kejeli, wala viherehere. “Tunawasihi watanzania wenzetu kusukumwa na utaifa, utu na ustaarabu katika kuitafuta na kuipata katiba mpya , jazba, kejeli viherehere na vitisho haviwezi kutupatia Katiba mpya,” alisema. Baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao ni makada wa CCM ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Massaburi, Waziri wa zamani, Iddi Simba na Mwenyekiti zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Hemed Mkali.

Alisema kuwa katika harakati za kushinikiza katiba mpya dalili zinazoonyesha kuwepo kwa baadhi ya makundi ya watu wanaodhani kwamba wao wanaihitaji zaidi kuliko wengine. "Pia wapo wengine wanaodhani mawazo na matakwa yao pekee ndiyo yanayostahili kuingia kwenye katiba bila hata kujua katiba iliyopo.

"Zote ni dosari zinazoweza kupelekea kazi yetu ya katiba mpya isiwe na mafanikio. Sisi wazee tunaomba ieleweke kuwa katiba siyo pembejeo ya kilimo ambayo inamhusu mkulima pekee na kutomhusisha mvuvi bali katiba ni mwongozo wetu Watanzania wote. Mtulia aliwageukia viongozi wa dini na kusema: “Hakuna sababu ya kulifanya suala la Katiba mpya kuwa suala la kidini, kiasi cha kuligeuza kuwa ndiyo mahubiri au mawaidha ya msingi katika ibada kwa kuwa hata wenye imani tofauti au wasio na dini na wao inawahusu,” alisema.

Hakuwaacha kando wanasiasa ambao walikuwa mstari wa mbele katika vuguvugu hilo akiwakemea kwa kusema: "Hakuna sababu ya kusukumwa na jazba wala kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuwa hata wasio wanasiasa wanaguswa na katiba mpya." Kama lengo ni kupata katiba mpya, Mtulya ambaye wakati wote alikuwa akishangiliwa na wazee waliofika kuunga mkono azimio hilo, alisisitiza: "Njia bora ya kufikia lengo (la katiba mpya) ni kuwa pamoja, kuweka mbele utu, maslahi ya taifa na haki ya kila mmoja wetu.

Kauli hiyo ya wazee imekuja wakati ambao viongozi wa dini na vyama vya siasa vikipongezana kwa mafanikio waliyoyapata baada ya kuongoza mjadala wa kudai katiba mpya hadi Rais Kikwete kutangaza kwamba mwaka 2011 mchakato wake utaanza. Desemba 31 mwaka jana Rais Kikwete alitangaza kukubali kuandikwa kwa katiba mpya na kuahidi kuunda tume itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea ili kuongoza mchakato wa katiba mpya.

Hatua hiyo aliichukua baada ya vyama vya siasa vya upinzani, CUF, Chadema, TLP kutamka hadharani malengo yao ya kutaka katiba mpya. Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) alikuwa tayari ametangaza nia yake ya kupeleka Bungeni hoja binafsi ya kutaka katiba mpya.

Hata hivyo, hivi karibuni aliliambia gazeti hili kwamba amesitisha nia hiyo ili kuona matokea ya mchakato uliotangazwa na Rais Kikwete. Katika kushinikiza katiba mpya, wanachama wa CUF waliandamana kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Komban licha ya polisi kukataa kuyaidhinisha na kusema ni batili. Wasomi na wanasheria nchi nao walijiingiza katika vuguvugu hilo na kuishauri serikali kukubali mkakati huo wa katiba mpya kwa sababu iliyopo imepitwa na wakati na haikidhi matakwa ya sasa.
 
Sasa wanamuunga mkono kwa kukubali then wanawashutuku walioshinikiza?? Haiingii akilini?? Hawa wazee wanyamaze maana wako kwenye pension watuachie nchi yetu. Siku zao ziko numbered wanasubiri zamu zao tu kwenye fail la Israel.
 
Sasa wanamuunga mkono kwa kukubali then wanawashutuku walioshinikiza?? Haiingii akilini?? Hawa wazee wanyamaze maana wako kwenye pension watuachie nchi yetu. Siku zao ziko numbered wanasubiri zamu zao tu kwenye fail la Israel.

Yaani ni kichekesho mkuu na hao ndiyo haswaaa mtaji wa CCM, ukisikia akina Makamba, JK wanaongelea watanzania wanawazungumzia hawa.......Shame on them!
 
Zamani nikuwa naaminishwa nami nikaamini kuwa Uzee ni hekima. Ila sasa imani hiyo nimeizika kabisa kutokana na watu kama hawa.
 
....they are not even sure of what they are saying......God help them, they can't help themselves to R.I.P!
 
Sasa wanamuunga mkono kwa kukubali then wanawashutuku walioshinikiza?? Haiingii akilini?? Hawa wazee wanyamaze maana wako kwenye pension watuachie nchi yetu. Siku zao ziko numbered wanasubiri zamu zao tu kwenye fail la Israel.

Ni kweli kabisa mzee, nashangaa sana kusikia watu wanatumia jina la wazee wa Dar es salaam wakati si wote, ni kundi tu la wazee wa CCM. Suala la katiba Tanzania halijaanza na Kikwete wala hao walioshinikiza jana, it is over a decade uliza kina Shivji, uliza kina Chris Maina, uliza Sengondo Mvungi, uliza kina Marando, hii si issue ya Kikwete.

Kumsifu au kumpongeza JK kwa mambo ambayo si yake ni sawa na kumdhalilisha.

Let him be himself, apongezwe kwa anayoanzisha yeye na si ya wengine.
 
.......aliyesema 'adui muombee njaa' hakukosea,bana. Njaa mbaya....unauza utu wako hivi hivi!!! hapo washakula elfu kadhaa na kukodishiwa Hiace kwisha kazil.
 
Ni kweli kabisa mzee, nashangaa sana kusikia watu wanatumia jina la wazee wa Dar es salaam wakati si wote, ni kundi tu la wazee wa CCM. Suala la katiba Tanzania halijaanza na Kikwete wala hao walioshinikiza jana, it is over a decade uliza kina Shivji, uliza kina Chris Maina, uliza Sengondo Mvungi, uliza kina Marando, hii si issue ya Kikwete.

Kumsifu au kumpongeza JK kwa mambo ambayo si yake ni sawa na kumdhalilisha.

Let him be himself, apongezwe kwa anayoanzisha yeye na si ya wengine.

Halafu kwa mawazo na matendo ya namna hii tunashangaa kwa nini nchi yetu inazidi kuwa masikini
 
.......aliyesema 'adui muombee njaa' hakukosea,bana. Njaa mbaya....unauza utu wako hivi hivi!!! hapo washakula elfu kadhaa na kukodishiwa Hiace kwisha kazil.
Wanafiki wakubwa hao.Mbona hatukuwasikia kuzungumzia yaliyowafika wazee wenzao wastaafu wa iliyokuwa EAC??!
 
Hao hamna kitu umri ulishawatupa wameibeba sana CCM na kutumika bila kujijua waache wamelize uzee wao kwa kujikomba ndio maana hata matibabu hawapewi na CCM, vijana kazi yetu ni kubadili kutoka muelekeo wa wazee hawa na kwenda muelekeo sasa wa kujenga nchi na kufaidi matunda yake
 
Zamani nikuwa naaminishwa nami nikaamini kuwa Uzee ni hekima. Ila sasa imani hiyo nimeizika kabisa kutokana na watu kama hawa.

hawa wazee si ndo wa kwanza kulala bararani kudai pensheni zao....? Bac kama sio hawa..hawa wanaomsapoti jk ni wanafiki,wafitini wasiokuwa na utu na wazee wenzao. Pia hawana utu wala uzalendo na taifa..,
halafu hakuna wazee dsm wazee wameishia chalinze hawa ni matapeli......
 
Hawa wazee nawaheshimu tu kwa sababu ni watu wazima lakini sipendi na sikubali jinsi wanavyotumia njaa zao kushadidia mambo wasiyojajua ipasavyo.
Kuunda tume ya katiba ni kitu kimoja, lakini kuwa na katiba inayokidhi matakwa ya watanzania wote ndicho tunachokililia wote. Kikwete anataka zaidi kulinda masilahi yake na chama chake kuliko kutuletea katiba tunayoitaka, katiba ambayo itamnyima yeye na chama chake mamlaka ya kisheria kuvuruga chaguzi zetu, na kwa hiyo sidhani kwamba yuko tayari kuharakisha zoezi hili ili kuhakikisha kuwa tunaingia kwenye uchaguzi wa 2015 tukiwa na katiba mpya inayokubalika na wengi
 
Na hasa ukiwa mzee wa CCM!

Njaa tu inawasumbua Wazee hawa wa CCM, hekima zao wameweka pembeni kabisa na kutumiwa na mafisadi kila wanapoona umuhimu wa kuwatumia Wazee hawa.

 
inawezekana hata hilo tamko wameandaliwa wakapewa walitoe. Hivi kwenye hilo kundi kuna mstaafu yeyote wa iliyokuwa jumuiya ya afrika Mashariki? na ambaye bado anadai kiinua mgongo chake?
 
Njaa tu inawasumbua Wazee hawa wa CCM, hekima zao wameweka pembeni kabisa na kutumiwa na mafisadi kila wanapoona umuhimu wa kuwatumia Wazee hawa.


Wananikumbusha siku ile alipokuwa akihutubia na kuchimbia mkwara TUCTA yaanai walikuwa wakishangilia hata kabla hawajasikia point, yaani ilikuwa kila JK akianza kuongea wasikia makofi tu.

Sasa wampongeza alafu waponda papohapo duh.
 
Back
Top Bottom