Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 9,359
- 15,089
Hii Katiba ya Marekani kwa kweli kwangu mimi ni moja kati ya Katiba mbovu sijapata kuona na huwa nashangaa sana nchi nyingi masikini wanavyoiiga.
Hivi majuzi nilipigwa na butwaa pale nilipoona raisi wa nchi ya Marekani hana cha kufanya na kubaki kujitetea tu kwenye vyombo vya habari pale ambapo Bunge la nchi hiyo lilivyoamua kumualika na kumruhusu Mkuu wa nchi ya Israeli, Bw. Netanyahu kuhutubia Bunge la Marekani ingawaje raisi wa nchi Bw. Obama alikataa na hakuhusishwa.
Hii hali imenishangaza sana kwa kweli sasa huyu Rais wa Marekani kazi yake ni ipi? Je hana nguvu yoyote? Ni nani alimpa VIZA huyu Netanyahu? Na je waliompa VIZA ni nani Bosi wao? Na je nguvu yake ni kuongea tu kwenye vyombo vya Habari?
Kwa kweli tuige yote lakini Katiba kama hii hapa Bongo nasema HAPANA KUBWA, sipati picha yaani Bunge la TZ limualike Rais Kagame kuja kulihutubia bila kumwambia raisi wa JMT na hilo lifanyike na Rais wa JMT asiwe na la kufanya, hii kwangu ni HAPANA.