Mkuu Salary Slip,
You have a point. Naona mgawanyiko mkubwa kwa mlengo wa kisiasa kati ya ccm na vyama upinzani kwa upande mmoja, na Tanzania bara (soma Tanganyika) na Zanzibar (soma Unguja na Pemba) kwa upande mwingine. Wabunge katika kikao kinachoendelea sasa wana nafasi kubwa sana ya kuhahakikisha kuwa tunavuka salama katika hili.
Lakini, kwa hali ilivyo katika serikali yetu na mawaziri wake 'wanaopenda' majibu mepesi kwa maswali magumu, mbwembwe na kejeli nyingi kwa wapinzani wao, ushabiki wa wabunge wa ccm kwa serikali hata pale ambapo iliyo mezani ina maslahi mapana ya taifa bila kujali itikadi za vyama, nakubaliana na wewe kwa 100% kuwa muda sio mrefu harakati hizi zitahamia uraiani ambako madhara yake yanaweza kuwa makubwa zaidi.
Chonde chonde madam spika na timu yako, hii ndio nafasi pekee ya kulitendea haki taifa hili kwa kutokuchezea muswada wa sheria ya kura ya maoni ulio mbele ya bunge lenu tukufu sasa.